Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w93 3/1 kur. 30-31
  • Wamishonari wa Mikronesia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wamishonari wa Mikronesia
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
w93 3/1 kur. 30-31

Wamishonari wa Mikronesia

INGAWA wametenganishwa na sehemu kubwa-kubwa za Bahari ya Pasifiki inayoonekana kutokuwa na mwisho, wamishonari wa Mikronesia huweza bado kukusanyika kila mwaka kuwa na “muungano wa familia.” Na waeneza evanjeli hao wote kutoka visiwa vya mbali hukutania wapi? Kwa kufaa, ni mahali ambapo serikali ya mahali hapo pamepaita Barabara ya Yehova—mahali pa ofisi ya tawi ya Guam ambayo wanatumikia chini yayo.

Katika Juni 1992, wamishonari 56 walikutana kwenye tawi ili kuhudhuria “Wachukuaji Nuru” Mkusanyiko wa Wilaya. Kicheko na mazungumzo yenye uchangamfu yalijaza hewa walipofanya upya urafiki mbalimbali wa zamani na kuanzisha urafiki mpya. Kama vile sikuzote, walijipanga wenyewe juu ya ngazi za Jumba la Ufalme ili kupigwa picha wakiwa kikundi na kisha wakaketi kwenye meza ndefu tatu za karamu kushiriki mlo wa mishonari wa kila mwaka, uliofanywa wenye kutokeza mwaka huu kwa ziara ya Albert Schroeder, mshiriki wa Baraza Linaloongoza.

Kwa wengi wa wamishonari, kikusanyiko hicho cha kila mwaka katika Guam ni fursa yao pekee ya kuondoka makao yao madogo ya kitropiki. Nayo ni madogo sana. Kisiwa cha Ebeye, kimojapo Visiwa vya Marshall, ni cha hektari 32 tu. Kao la mishonari katika Kisiwa cha Majuro cha Marshall na kao la Kiribati katika Visiwa vya Gilbert yote mawili yako kwenye visiwa virefu vyembamba vya matumbawe vyenye upana unaopungua kilometa 0.8. Kwa hiyo wamishonari hufurahia kadiri wawezavyo safari yao yenye kusisimua ya kwenda Guam.

Ingawa wazo la kuhubiri katika kisiwa cha mbali cha kitropiki lasikika kuwa jambo la kusisimua, kwa uhalisi hilo ni jambo gumu ambalo ni wachache walio tayari kukabili. Kwa kupendeza, ni wamishonari 7 tu kati ya wale 56 wanaotoka Watchtower Bible School of Gilead. Wengi walitoka Hawaii au Ufilipino walikokuwa wahudumu mapainia waliozoea tayari maisha katika tropiki, na walienda moja kwa moja kutoka nchi za kwao hadi migawo yao ya mishonari.

Kwa sababu visiwa vya Mikronesia viko karibu sana na ikweta, wamishonari hupambana na joto jingi na unyevu mwingi ili kuwafikia wakaaji kwa habari njema. Uwasiliano waweza kuwa jambo lililo gumu hata zaidi. Kila kisiwa au kikundi cha visiwa kina lugha yacho chenyewe—nyingine zisizojulikana kabisa hivi kwamba haziko katika kamusi—na huenda ikachukua miaka mingi kabla ya mgeni kuweza kuinena kwa ufasaha. Ili kuwasaidia watu katika tamaduni hizo tofauti-tofauti za visiwa waelewe Biblia, tawi la Guam huchapisha fasihi katika lugha 11, ambazo 9 kati yazo zinanenwa katika Mikronesia tu.

Visiwa vingine vimetengwa sana hivi kwamba vyaweza kufikiwa kwa mashua tu. Kao la mishonari la Tol katika Chuuk (Truk) liko kwenye kisiwa cha jinsi hiyo, na wamishonari wa huko hutegemea vyombo vya kunasia mianga ya jua ili kuandaa nguvu za umeme kwa muda wa saa chache tu kila siku.

Kwa ujumla, kuna makao ya mishonari 14 kotekote Mikronesia, inayotia ndani eneo lililo karibu ukubwa wa bara la United States. Kati ya wale watu zaidi ya 400,000 wanaoishi katika mkoa huo, 1,000 ni wahubiri wa habari njema, waliopangwa kitengenezo katika makundi 20 na vikundi 3 vya mbali.

Ingawa kwa kawaida watu wa Mikronesia ni wenye urafiki sana, desturi za kidini za mahali hapo na mbano wa familia huwavunja moyo wengi wasikubali kweli ya Ufalme wa Mungu. Kwa hiyo ingawa kazi ya kuhubiri inasitawi kwa ujumla (wale wahubiri wa Ufalme 1,000 wanaongoza mafunzo ya Biblia yanayozidi 2,000), makundi na vikundi vingine vinabaki vikiwa vidogo. Kwa mfano, kuna wahubiri 5 tu kwenye kisiwa cha Tinian, wahubiri 7 tu kwenye kisiwa cha Nauru, na makundi katika Yap, Kosrae, na Rota yana wahubiri wanaopungua 40 katika kila moja. Hata hivyo, baadhi ya wamishonari wamebaki katika migawo yao kwa miaka zaidi ya 20. Yenye kutokeza ni kwamba, wote sita kwenye kisiwa cha Belau wamekuwa hapo kwa angalau miaka 12.

Kwa wale wanaovumilia, thawabu ni nyingi. Kuna fursa za kila siku za kustaajabia uzuri wa uumbaji wa Yehova. Visiwa vya Mikronesia vyenye majani mabichi vimetawanyika kama vito vidogo vya chanikiwiti kutoka upande mmoja hadi mwingine katika mandhari ya buluu ya Pasifiki. Kilometa nyingi za fuo zisizojaa watu na za vizingiti vya matumbawe vyenye samaki wengi wa rangi-rangi huwavutia wale wenye idili ya kupiga mbizi na kuogelea chini ya maji wachunguze-chunguze baadhi ya mahali pazuri zaidi ulimwenguni pa kupigia mbizi. Na mwisho wa kila siku, kuna ile mandhari nzuri ajabu ya mshuko wa jua juu ya bahari.

Hata hivyo, thawabu iliyo kubwa zaidi ni lile pendeleo la kumtumikia Yehova kwa kuwaambia wengine juu ya ahadi zake nzuri ajabu kwa wakati ujao. Kwa sababu wamishonari wa Mikronesia huendelea kufikilia thawabu hiyo, wanatimiza maneno ya Isaya 42:12: “Na wamtukuze BWANA [Yehova, NW], na kutangaza sifa zake visiwani.”

[Ramani/Picha katika ukurasa wa 31]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Barrigada, Guam

Santa Rita, Guam

Koror, Belau

Chuuk (Truk) Islands

Tarawa, Kiribati

Kosrae

Ebeye

Marshall Islands

Majuro

Kolonia, Pohnpei

Songsong, Rota

Saipan

Yap

MICRONESIA

MELANESIA

CAROLINE ISLANDS

PACIFIC OCEAN

PHILIPPINES

NEW GUINEA

EQUATOR

[Picha]

Wamishonari wakusanyika katika Guam, Juni 1992

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki