Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w93 8/15 uku. 32
  • Je! Alimmeza Yona?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Alimmeza Yona?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
w93 8/15 uku. 32

Je! Alimmeza Yona?

Biblia hutuambia kwamba Yona, nabii wa Yehova katika karne ya tisa K.W.K., alipanda meli, akitoroka mgawo fulani. Katika safari hiyo yenye dhoruba katika Bahari ya Mediterania, mabaharia walimtupa baharini. “BWANA [Yehova, NW] akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule muda wa siku tatu, mchana na usiku.”—Yona 1:3-17.

Wengine husema, ‘Haiwezekani! Hakuna kiumbe baharini ambaye angeweza kummeza mtu.’ Lakini ama nyangumi-shahawa ama papa-mweupe mkubwa sana angeweza kummeza mtu. Jarida National Geographic (Desemba 1992) lilidokeza uwezekano mwingine—yule papa-nyangumi. Ambaye ni papa mkubwa zaidi anayejulikana, anaweza kukua kufikia urefu wa meta 20 na uzito wa tani 70.

“Muundo wa umeng’enyaji wa papa-nyangumi huyo wapatana na masimulizi ya Yona. Ni rahisi kujiwazia ukifyonzwa kwa ghafula ndani ya kinywa cha papa-nyangumi, ambacho ni kikubwa mno . . . Kinywa chenye vibweta vya tishu-kifereji cha hata papa-nyangumi kijana kingeweza kwa urahisi kutoshea Yona wawili.”

Papa-nyangumi hula planktoni (vimea na vinyama vya majini) na krili (aina ya samaki) wadogo sana, “wanaopitia umio kwa maji kuingia lile jumba nyumbufu la karamu yaani sehemu ya juu ya tumbo.” Hata hivyo, mtu angeweza kutokaje? National Geographic lasema: “Papa wana njia ya upole ya kuondoa vitu wanavyomeza ambavyo si rahisi kumeng’enya . . . Papa anaweza kuondoa polepole chakula chote kutoka kwenye sehemu ya juu ya tumbo lake kwa kulipindua ili sehemu ya ndani iwe nje na kulisukuma kupitia kinywa. . . . Kwa hiyo, ungeweza kutoka nje kwa kuteleza kwenye zulia lenye kufunikwa uteute, ukiwa mwenye utelezi zaidi lakini mwenye hekima zaidi kutokana na ono hilo.”

Leo papa-nyangumi hawapatikani katika Bahari ya Mediterania, ingawa wamepatikana kaskazini ya mbali kufikia New York City. Je! walikuwamo katika Bahari ya Mediterania wakati wa Yona? Ni nani ajuaye kwa hakika? Biblia haitaji kimahususi aina ya kiumbe cha baharini ambacho Yehova alitumia, lakini Yesu mwenyewe alihakikisha kwamba simulizi la Yona ni la kweli.—Mathayo 12:39, 40.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]

Norbert Wu/Peter Arnold Inc.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki