Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 10/15 uku. 31
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 10/15 uku. 31

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hawa, na baadaye Adamu, walipokula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya, je, walikula tofaa?

Hatujui. Watu wengi wamefikiri kwamba ‘tunda lililokatazwa’ lilikuwa tofaa, na katika karne zilizopita wachoraji wameonyesha hivyo. Lakini Biblia haitaji mti huo wala tunda lao. Hawa alilirejezea kuwa tu “matunda ya mti ulio katikati ya bustani.”—Mwanzo 3:3.

Makala ya “Tofaa” iliyo katika Insight on the Scriptures lapendeza sana kwa habari hiyo:

“Kuna dhana nyingi sana kuhusu jina la mti na tunda lililotajwa kwa neno la Kiebrania tap·puʹach. Neno hilo lenyewe laonyesha kile kinachotofautishwa na manukato, au marashi. Neno hilo latokana na neno la msingi na·phachʹ, limaanishalo ‘puliza; hema; kukuta.’ (Mwa 2:7; Ayu 31:39, NW; Yer 15:9, NW) Kuhusu jambo hili, M. C. Fisher aliandika hivi: ‘Uhusiano [na na·phachʹ] wa kwanza wa kilugha waonekana kuwa mbali, lakini mawazo ya “pumzi” na “toa harufu” yahusika. Neno jingine pia puah lamaanisha maneno yote mawili “puliza” (la upepo) na “kutoa harufu nzuri, kuwa manukato.”’—Theological Wordbook of the Old Testament, kilichohaririwa na R. L. Harris, 1980, Buku 2, uku. 586.

“Matunda kadhaa yamedokezwa badala ya tofaa, kutia ndani chungwa, balungi, pera la ulaya, na aprikoti. . . . Hata hivyo, neno la Kiarabu tuffah linalohusiana na hilo kwa msingi lamaanisha ‘tofaa,’ na ni jambo la kufikiriwa kwamba majina ya Kiebrania ya mahali-mahali kama Tappuah na Beth-tappuah (labda zikiitwa hivyo kwa sababu ya wingi wa tunda hilo katika eneo hilo) yamehifadhiwa kwa majina yao ya Kiarabu kwa kutumia neno hilo. (Yos 12:17; 15:34, 53; 16:8; 17:8) Sehemu hizi hazikuwa katika nyanda za chini lakini katika eneo lenye milima-milima, ambapo hali ya hewa kwa ujumla huwa ya kiasi. Kwa kuongezea, kuna uwezekano wa kuwako kwa mabadiliko fulani ya hali ya hewa. Mitofaa hukua katika Israeli siku hizi na hivyo yaonekana inapatana na ufafanuzi wa Biblia ifaavyo. William Thomson, aliyekuwa Siria na Palestina kwa miaka mingi katika karne iliyopita, hata aliripoti kupata mashamba ya mitofaa katika eneo la Ashkeloni katika Nyanda za Filistia.—The Land and the Book, kilichosahihishwa na J. Grande, 1910, kur. 545, 546.

“Mtofaa (Pyrus malus) watajwa hasa katika Wimbo Ulio Bora, ambapo maneno ya mapenzi ya mwenzi mchungaji wa Mshulami yalinganishwapo na kivuli kizuri cha mtofaa na utamu wa tunda lao. (Wim 2:3, 5, NW) Naye alinganisha pumzi ya msichana huyo na manukato ya matofaa. (Wim 7:8; ona pia 8:5, NW.) Katika Mithali (25:11, NW) usemi ufaao, kwa wakati mzuri wafananishwa na ‘matofaa katika vichongo vya fedha.’ Rejezo jingine la pekee kwa mtofaa liko kwenye Yoeli 1:12. Mapokeo ya kawaida ya kwamba tofaa ndilo tunda la Edeni lililokatazwa kamwe halina msingi wowote wa Kimaandiko. Vivyo hivyo, maneno ‘tofaa la macho’ lapatikana katika King James Version (Zab 17:8; Mit 7:2; na mengine) lakini hayo si maneno ya Kiebrania, tafsiri halisi likiwa ‘mboni ya jicho [la mtu].’”—Insight on the Scriptures, Buku 1, kur. 131-2, kilichotangazwa katika 1988 na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki