Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 10/15 uku. 32
  • ‘Msihuzunike Kama Wengine’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Msihuzunike Kama Wengine’
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 10/15 uku. 32

‘Msihuzunike Kama Wengine’

UMEWAHI kuona jinsi ua huonekana limeinamishwa chini baada ya dhoruba? Kwa njia fulani hiyo ni hali yenye kugusa moyo sana. Kwani mngurumo wa mawingu huenda ukawa ulifanya wanyama na watu wengi—viumbe vyenye nguvu kuliko ua lolote—kukimbilia usalama. Hata hivyo, ua lilisimama papo hapo, likiwa limeshikwa hapo, likikabiliana na hali ngumu ya hewa. Sasa, halijaharibika, limeinamishwa lakini halijavunjwa, likionyesha uweza lijapokuwa laonekana halina nguvu. Waweza kushangaa, unapolitazama kwa kupendezwa, ikiwa litapata nguvu tena na kuinua kichwa chake kuelekea mbingu mara nyingine.

Hivyo ndivyo ilivyo na watu. Katika nyakati hizi zenye msukosuko, tunakabiliana na aina zote za dhoruba. Hali ngumu ya kifedha, mshuko wa moyo, afya mbaya, kupoteza mpendwa katika kifo—hali kama hizo hutujia sisi sote wakati mmoja au mwingine, na wakati mwingine hatuwezi kuyaepuka kama vile ua haliwezi kujing’oa na kukimbilia usalama. Ni jambo la kutia moyo kuona watu mmoja-mmoja waonekanao kuwa dhaifu wakionyesha uwezo wenye kushangaza na kuvumilia hali kama hizo zenye kukatisha tamaa. Wao hufanyaje? Mara nyingi ufunguo ni imani. Ndugu-nusu wa Yesu Kristo Yakobo aliandika: “Mwajua ya kwamba wakati imani yenu imeshinda katika kukabiliana na majaribu kama hayo, matokeo ni uwezo wa kuvumilia.”—Yakobo 1:3, Today’s English Version.

Ufunguo mwingine ni tumaini. Kwa mfano, kifo kinapompata mpendwa, tumaini laweza kufanya tofauti kubwa sana kwa waliobaki. Mtume Paulo aliandikia Wakristo katika Thesalonike: “Hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.” (1 Wathesalonike 4:13) Ingawa Wakristo bila shaka huhuzunikia kifo, kuna tofauti. Wana ujuzi sahihi kuhusu hali ya wafu na kuhusu tumaini la ufufuo.—Yohana 5:28, 29; Matendo 24:15.

Kujua hivyo huwapa tumaini. Na tumaini hilo, kwa upande mwingine, polepole hupunguza huzuni yao. Huwasaidia kuvumilia, na zaidi. Baada ya muda, kama ua baada ya dhoruba, waweza kuinua vichwa vyao juu kutoka kwenye hali ya huzuni na kupata furaha na uradhi katika maisha mara nyingine tena..

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki