Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 12/1 uku. 31
  • ‘Matendo Yake Yamfuata’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Matendo Yake Yamfuata’
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 12/1 uku. 31

‘Matendo Yake Yamfuata’

SAA 2:50 asubuhi ya Alhamisi, Julai 28, 1994, George D. Gangas alimaliza mwendo wake wa kidunia. Alikuwa na umri wa miaka 98. Akiwa mmoja wa watiwa-mafuta, George Gangas amekuwa mshiriki wa Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova tangu Oktoba 15, 1971.

Wote waliomfahamu binafsi Ndugu Gangas walijua juu ya upendo wake wa uadilifu na jinsi alivyochukia uovu. Wao wanakumbuka vizuri sana jinsi alivyokuwa akimfafanua Shetani mara kwa mara kuwa mwongo, mbaya sana, wa kuchukiza mno, mwovu, na mwenye kukirihisha. Kinyume cha hayo, alizungumza juu ya Yehova kuwa mwenye upendo, fadhili, huruma, mwororo, na Baba mwenye kujali. Wengi pia wanakumbuka jinsi alivyopenda kuuliza maswali ya Biblia. Kwa kila mazungumzo, hangekosa kuuliza maswali—mengine yakiwa rahisi, mengine yakiwa magumu. Kwa kweli, alipenda kweli za Biblia.

Ndugu Gangas alibatizwa katika Julai 15, 1921. Alianza kazi yake ya maisha katika huduma ya kuhubiri wakati wote (upainia) katika Machi 1928. Kwa hiyo, alikuwa katika utumishi wa wakati wote kwa jumla ya miaka 66. Akawa mshiriki wa wafanyakazi katika makao makuu ya Brooklyn ya Watch Tower Bible and Tract Society katika Oktoba 31, 1928.

Masimulizi ya maisha yake yalitokea katika toleo la Mnara wa Mlinzi la Oktoba 15, 1966, la Kiingereza. Linaonyesha mtu wa Mungu aliye wa kiroho kwelikweli. Katika makala hiyo, alisema maneno haya yafuatayo yenye kuchangamsha moyo: “Naupenda uhai na nataka ndugu zangu wapate uhai. Pamoja na mtume Paulo, nayahesabu, mambo mengine yote kuwa ‘hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu.’”—Wafilipi 3:8.

Ndugu Gangas alionyesha kwa matendo yake kwamba kwa kweli, aliupenda uhai, na kwa bidii alishiriki ‘ujuzi wa Kristo Yesu’ pamoja na wengine. Tutamkosa, lakini twafurahi kama nini kwamba sasa amekwisha kupokea thawabu yake ya kimbingu! Sasa, ‘atapumzika baada ya kazi yake, kwa kuwa matendo yake yamfuata’.—Ufunuo 14:13, New International Version.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki