Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w95 3/15 uku. 31
  • Yehova Ataokoa Dunia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yehova Ataokoa Dunia
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
w95 3/15 uku. 31

Yehova Ataokoa Dunia

UWANJA WA NDEGE uliopo katika kisiwa cha Maldives hufungwa kwa muda wa saa kadhaa kila siku. Kwa nini? Kwa sababu barabara ya ndege kutua hufurikwa wakati wa kujaa kwa maji, jambo linalofanya isiwe salama kwa ndege kutua. Wanasayansi fulani wahofu kwamba usawa wa bahari katika visiwa vya Maldives waweza kuinuka angalau kwa meta moja katika karne ijayo. Ingawa hicho chaonekana kuwa kiasi kidogo, ongezeko kama hilo laweza kufutilia mbali kabisa mataifa saba ya visiwa. Kwa kweli, kulingana na UN Chronicle, mwinuko wa meta mbili waweza kufunika karibu kikundi chote cha visiwa hivyo vipatavyo 1,200!

Ni nini kinachosababisha kuinuka kwa usawa wa bahari? Kulingana na Shirika la Mazingira la UM, uchafuzi wa hali-anga ya dunia unaofanywa na ‘gesi za kuongeza ujoto’ hufanya bahari katika sehemu za joto kufura, mapande makubwa ya barafu pamoja na migando ya barafu kuyeyuka, na hivyo kuinua usawa wa bahari. Taasisi ya Panos yenye makao makuu London yasema kwamba uchafuzi “huenda ulianzisha msiba wa duniani kote unaokuja polepole na ambao unabadilisha mipaka ya bara na bahari.”

Kuwapo kwa joto la dunia linalozidi kuongezeka kungali kunajadiliwa miongoni mwa wanasayansi. Hata hivyo, twaweza kuwa na hakika kwamba matatizo ya kimazingira hayataharibu kusudi la Mungu. “Ardhi yenye rutuba imefanyizwa imara,” yasema Biblia. “Haitatikisika kamwe.” (1 Mambo ya Nyakati 16:30, NW) Yehova ana udhibiti juu ya mazingira ya dunia, nasi twaweza kushangilia kwamba karibuni yeye ataokoa dunia pamoja na wanadamu wasiangamie.—Zaburi 24:1, 2; 135:6; 2 Petro 3:13.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

Mchoro uliotegemea picha ya NASA

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki