Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w95 3/15 uku. 32
  • Biblia Ina Thamani ya Kiasi Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Biblia Ina Thamani ya Kiasi Gani?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
w95 3/15 uku. 32

Biblia Ina Thamani ya Kiasi Gani?

HIVI karibuni British Library ilikubali kulipa karibu dola 1,600,000 kwa nakala ya tafsiri ya Kiingereza ya Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo ya William Tyndale. Iliyochapishwa miaka 468 iliyopita, ndiyo toleo kamili la pekee la Biblia ya Tyndale iliyookoka jitihada zenye nguvu za kuiangamiza. Biblia hii imekuwa ikionyeshwa peupe katika London.

Biblia ya Tyndale ilinunuliwa kutoka Bristol Baptist College katika Uingereza, ambapo ilikuwa imewekwa tangu 1784. Dakt. Roger Hayden, naibu wa mwenye kiti wa halmashauri ya chuo hicho, alisema hivi: “Hii ni hati ya kitaifa, kitamaduni na ya Kikristo yenye umaana sana nasi tulitaka ipatikane zaidi kotekote, kwa kuwa tumeihifadhi akibani.”

Kwa karne nyingi Biblia ilikuwa ikipatikana hasa kwa Kilatini nayo ingeweza kusomwa na makasisi na matajiri wenye elimu pekee. Kama vile John Wycliffe kabla yake, Tyndale alitaka kuwe na Biblia ambayo ingeweza kusomwa na kueleweka kwa wote. Wakati mmoja alimwambia kasisi mmoja aliyempinga hivi: ‘Ikiwa Mungu ataniruhusu niishi kwa miaka mingi, nitamfanya kijana mkulima ajue Maandiko kuliko ujuavyo.’

Hii ilikuwa kazi hatari, kwa sababu makasisi walipinga vikali jitihada yoyote ya kufanya Maandiko yapatikane kwa watu wa kawaida. Kama tokeo, Tyndale akakimbia kutoka Uingereza kwenda Ujerumani. Huko akatafsiri ile “Testamenti Mpya” kutoka Kigiriki cha awali. Nakala kama 3,000 zilichapishwa na kusafirishwa kwa siri hadi Uingereza. Askofu wa London akanunua kila nakala ambayo angeweza kupata na kuzichoma peupe katika ua wa kanisa la St. Paul. Mwishowe, Tyndale alishikwa, akajaribiwa, na kuhukumiwa kuwa mzushi. Katika 1536 alinyongwa na kuchomwa juu ya mti. Jinsi lilivyo jambo la kupendeza kwamba Biblia iliyochukiwa sana na makasisi sasa ni yenye thamani sana!

Mashahidi wa Yehova hujitahidi kwa bidii kuwapa ujuzi sahihi wa Biblia wote wanaoutafuta. Zaidi ya kuchapisha na kugawa tafsiri nyinginezo, wametafsiri kutoka lugha za awali tafsiri ya Biblia nzima iliyo sahihi na rahisi kusomeka. Kufikia 1995 nakala zaidi ya 74,000,000 za hii New World Translation of the Holy Scriptures zilikuwa zimechapishwa katika lugha 12. Bila shaka, thamani ya kweli ya Biblia yoyote ni ujumbe wayo wenye kutokeza uhai.

[Picha katika ukurasa wa 32]

William Tyndale

[Hisani]

Kutoka kwenye mchoro wa zamani katika Bibliothèque Nationale

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki