Miungu ya Kike ya Uzaaji na Vita
WAKATI wa kampeni ya kiakiolojia katika Ebla, Siria, kikumbushi chenye picha ya Ishta, mungu wa kike Mbabiloni wa uzaaji na vita kilipatikana. Mwakiolojia Paolo Matthiae akifafanua kuwa “kifuniko cha mviringo chenye mandhari ya kiibada ikionyesha kuhani-mke mwenye shela akiwa mbele ya sanamu moja ya kimungu . . . kichwa chayo kikiwa kimeshikamanishwa na nguzo nyembamba ndefu.”
Uvumbuzi huo ni wa maana, kwa kuwa sanamu hiyo ni ya tangu mwanzo wa karne ya 18 K.W.K. Kulingana na Matthiae, jambo hilo hutoa “ithibati ya mwisho” kwamba ibada ya Ishta iliendelea kwa miaka 2,000 hivi.
Ibada ya Ishta ilianza Babiloni na katika karne zilizofuata ikaenea katika Milki yote ya Roma. Yehova aliwaamuru Waisraeli kuondolea mbali kila namna ya dini bandia katika Bara Lililoahidiwa, lakini kwa sababu walikosa kufanya hivyo, ibada ya Ashtorethi (kifani cha Ishta cha Kikaanani) ikawa mtego kwao.—Kumbukumbu la Torati 7:2, 5; Waamuzi 10:6.
Ingawa Ishta na kifani chake Ashtorethi hawapo tena, tabia walizowakilisha—ukosefu wa adili na jeuri—zimeenea. Twaweza kwa kufaa kuuliza ikiwa jamii ya kisasa kwa kweli ni tofauti sana na staarabu hizo za kale zilizoabudu hiyo miungu ya kike ya uzaaji na vita.
[Picha katika ukurasa wa20]
Watoto pia walitolewa dhabihu kwa Tanit
[Hisani]
Ralph Crane/Bardo Museum