Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w96 1/1 kur. 2-4
  • Je, Amani Yaweza Kupatikana?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Amani Yaweza Kupatikana?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Nani Wanaosababisha Tisho la Vita vya Nyuklia?
    Amkeni!—2004
  • Amani na Usalama Ndio Uhitaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Tisho la Nyuklia Halijaisha
    Amkeni!—1999
  • Bado Kuna Tisho la Vita vya Nyuklia?
    Amkeni!—2004
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
w96 1/1 kur. 2-4

Je, Amani Yaweza Kupatikana?

“SIKUZOTE kutakuwa na vita mahali fulani. Huo ndio ukweli wenye kuhuzunisha kuhusu wanadamu.” Maoni hayo ya kutazamia msiba yalitokea hivi majuzi katika barua moja iliyotoka kwa msomaji fulani katika gazeti la Newsweek. Je, wakubaliana nayo? Je, vita haviwezi kuepukika na amani haiwezi kupatikana? Tukiamua kutokana na mambo ya kihistoria, ni rahisi kujibu ndiyo kwa maswali hayo yote mawili. Tangu rekodi zianze kuwekwa, wanadamu wamepigana katika vita moja baada ya nyingine, na mapambano yakawa yenye uharibifu zaidi na zaidi watu walipositawisha njia zenye mafanikio zaidi za kuuana.

Karne ya 20 vilevile haijakuwa tofauti. Kwa kweli, imeshuhudia vita vyenye ukatili zaidi ya vyote, lakini nayo imeshuhudia jambo fulani jipya. Miaka 50 iliyopita Marekani ilianzisha kipindi cha nyuklia kwa kuiangushia Japani mabomu mawili ya atomu. Katika miongo mitano tangu wakati huo, mataifa yameweka marundo makubwa sana ya silaha za nyuklia ambazo zina uwezo wa kuharibu uhai wa kibinadamu mara nyingi zaidi. Je, kuwapo kwa silaha za nyuklia hatimaye kutawaogopesha watu wasipigane vita? Mambo ya hakika yatoa majibu. Tangu 1945 mamilioni mengi ya watu wamekufa katika vita—ingawa mpaka sasa hakuna mabomu mengineyo ya nyuklia ambayo yameangushwa.

Kwa nini jamii ya kibinadamu inapenda vita sana hivi? Encyclopedia Americana yataja mambo fulani ya jamii ya kibinadamu ambayo kihistoria yametokeza vita. Hayo yatia ndani kutovumilia kidini, ubaguzi wa jamii, tofauti za kitamaduni, malengo tofauti-tofauti (kama vile Ukomunisti na ubepari), utukuzo wa taifa na fundisho la enzi ya taifa, hali za kiuchumi, na kupendwa kwa mambo ya kijeshi. Usomapo orodha hiyo, je, waona jambo lolote ambalo laelekea litabadilika karibuni? Je, mataifa yatapunguza bidii yao ya kuhifadhi enzi zayo? Je, watu watapunguza ubaguzi kijamii? Je, wanadini wenye siasa kali watapunguza ushupavu? Ni kama haiwezekani.

Basi, je, hakuna tumaini lolote kwamba siku fulani mambo yatakuwa afadhali na kutakuwa na amani ya kudumu? Ndiyo, kuna tumaini. Japo mvurugo wa ulimwengu huu, hata leo yawezekana kupata amani. Mamilioni wameipata. Ebu tukueleze kuhusu wachache kati ya watu hawa ili uone yale ambayo maono yao yaweza kumaanisha kwako.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 2]

Background cover and page 32: Reuters/Bettmann

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

Reuters/Bettmann

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki