Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w85 10/15 kur. 3-4
  • Amani na Usalama Ndio Uhitaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Amani na Usalama Ndio Uhitaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Habari Zinazolingana
  • Vita ya Ulimwengu ya Kwanza na Mwanzo wa Huzuni Mbalimbali
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Ni Nani Awezaye Kuleta Amani Yenye Kudumu?
    Amkeni!—1996
  • Ni Nani Wanaosababisha Tisho la Vita vya Nyuklia?
    Amkeni!—2004
  • “Vita Vya Kukomesha Vita Vyote”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
w85 10/15 kur. 3-4

Amani na Usalama Ndio Uhitaji

“Vita katika karne ya ishirini imeendelea pole kwa pole kuwa ya ukatili zaidi, yenye uharibifu zaidi, yenye kushuka zaidi heshima katika pande zote zayo. . . . Makombora yaliyoangushwa juu ya Hiroshima na Nagasaki yalimaliza vita moja. Pia yalifahamisha wazi kabisa kwamba hatupaswi kamwe kuwa na vita nyingine. Hilo ndilo somo ambalo mwanadamu na viongozi kila mahali lazima wajifunze, nami naamini kwamba watakapojifunza somo hilo watapata njia ya kufikia amani yenye kudumu. Hakuna uchaguzi mwinginewo wote.”​—Henry L. Stimson, katika makala “The Decision to Use the Atomic Bomb” (Uamuzi wa Kulitumia Kombora la Atomi), Harper’s Magazine, Februari 1947.

ULIKUWA ni mwaka mmoja tu baada ya kuundwa kwa Umoja wa Mataifa kwamba Bw. Stimson, aliyekuwa katibu wa vita wa United States tangu 1940 mpaka 1945, akasema maneno yaliyoandikwa juu. Basi, je! baada ya karibu miaka 40, mwanadamu amejifunza “somo”? Je! Umoja wa Mataifa umekuwezesha kufurahia maisha katika “amani yenye kudumu”? Ebu fikiria gharama kubwa sana ambayo wanadamu wamepata kwa sababu ya vita na matayarisho ya vita tangu Vita ya Ulimwengu ya Pili.

GHARAMA YA KIBINADAMU: Ni gharama gani ya kibinadamu imeletwa na vita tangu Vita ya Ulimwengu ya Pili, ijapokuwa Umoja wa Mataifa umefanya jitihada za kuleta amani? “Tangu wakati wa ule uharibifu mkubwa ulioletwa na Vita ya Ulimwengu ya Pili, kumekuwa na vita vikubwa-vikubwa 105 ([vinavyohesabiwa kwa kutegemea] vifo vya watu 1,000 au zaidi kwa mwaka) ambavyo vilipiganwa katika nchi na maeneo 66. . . . Vita ambavyo vimekuwako tangu 1945 vimeua watu milioni 16, wengi zaidi wakiwa ni kati ya watu wa kawaida kuliko waliokuwa katika majeshi. (Hesabu, hasa ya watu wa kawaida, si kamili; vita vilivyo vingi haviwi na maandishi rasmi yaliyowekwa kuvihusu.)”​—Kichapo World Military and Social Expenditures 1983 cha Ruth Sivard.

Kwa kweli amani na usalama inaendelea kusonga mbali zaidi​—ukawaida wa kutokea kwa vita umeongezeka. Sivard anaeleza hivi: “Katika miaka ya kuanzia 1950 wastani [hesabu ya vita] ilikuwa 9 kwa mwaka; katika miaka ya kuanzia 60, 11 kwa mwaka; na katika miaka ya kuanzia 70 . . . , 14 kwa mwaka.”

GHARAMA INAYOHUSU MAONI YA AKILINI: Tangu wakati wa Hiroshima, mwanadamu ameishi akiogopa vita ya nyukilia. Silaha za nyukilia za 1945 zilikuwa zimeongezeka zikawa 50,000 ulimwenguni pote kufikia mwaka wa 1983. Na bado nyingine zaidi zinatengenezwa! Kwa wazi, kadiri hesabu ya silaha za nyukilia na mataifa yaliyo nazo inavyozidi kuongezeka, ndivyo na hatari ya kutokea kwa vita ya nyukilia. Ingawa hivyo, kunakuwa na matokeo gani akilini kwa sababu ya woga wa kwamba vita ya nyukilia inaweza kutokea?

Kitabu Preparing for Nuclear War​—The Psychological Effects kinajibu: “Uchunguzi zaidi unahitajiwa kwa haraka ili ionekane watoto na watu wazima wamepatwa na matokeo gani katika tamaa zao za kutaka sana kutimiza mambo na katika mwenendo wao kwa sababu ya kuishi wakijua kuna silaha za nyukilia . . . Hii inaweza kuwa gharama kubwa sana na yenye kuendelea kwa jumuiya zetu, yenye kuendelea kuongezeka kadiri vizazi vinavyoendelea kukomaa. Hiyo ni hasara iliyoje kwa mambo ambayo mtoto mdogo alitazamia angefanya wakati ujao?”

Kwa kweli, vijana hasa ndio rahisi kuumizwa zaidi na ukosefu wa wakati ujao salama. Uchunguzi wa hivi majuzi uliofanywa kati ya watoto wa Australia wa kuanzia miaka 10 mpaka 12 ulifanya maelezo kama haya yatolewe: “Nafikiri wakati mimi nitakapokuwa mtu mzima kutakuwa na vita na kila mtu katika Australia atakufa.” “Ulimwengu utakuwa kitu kilichoharibika​—kutakuwa na viumbe waliokufa kila mahali, na United States italipuliwa itoke usoni pa dunia.” Zaidi ya asilimia 70 ya watoto hao “waliitaja vita ya nyukilia kuwa jambo linaloelekea litaweza kutokea.” “Wachunguzi wa hali za kijamii wanaogopa kwamba huenda ikawa ukosefu wa wakati ujao salama ndio kwa kiasi fulani unaowafanya vijana wengi wawe na mwelekeo wa kuishi kwa ajili ya leo, matokeo yakiwa kwamba wanatafuta-tafuta mambo yenye kuwapa raha.

GHARAMA YA KIUCHUMI: Kabla ya miaka ya karibu na 1935, gharama za matumizi ya kijeshi ulimwenguni zilikuwa karibu dola bilioni 4.5 (za U.S) kwa mwaka. Lakini mwaka 1982 tarakimu hiyo ilikuwa imepanda ikafikia dola bilioni 660. Na, kama unavyojua, imeendelea kupanda juu. Ili kusaidia kujulisha namna hasa gharama hizo zilivyo, kichapo World Military and Social Expenditures 1983 kinaeleza hivi: “Kila dakika watoto 30 wanakufa kwa kukosa chakula na kukosa chanjo za bei ndogo, na kila dakika kiasi kinachopangiwa matumizi ya kijeshi ulimwenguni kinakula dola milioni 1.3 kutoka hazina ya pesa za umma.” (Italiki ni zetu.) Na sasa, katika muda wa miaka zaidi ya miwili, kiasi hicho kimefika dola milioni 2 kila dakika.

Unapofikiria hasara kubwa ambayo mwanadamu amepata kwa sababu ya vita na matayarisho ya vita, jambo moja ni hakika: Kwa kujitegemea mwenyewe, mwanadamu hajapata “amani yenye kudumu.” Lakini, jiulize hivi: Je! kuna njia ya kupata amani na usalama ulimwenguni pote katika muda wa maisha yetu? Inaweza kuja kutoka chanzo gani? Je! inakupasa utegemee Umoja wa Mataifa? Ikiwa sivyo, amani na usalama itapatikanaje?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki