Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w08 4/1 kur. 3-4
  • “Vita Vya Kukomesha Vita Vyote”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Vita Vya Kukomesha Vita Vyote”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Habari Zinazolingana
  • Amani na Usalama Ndio Uhitaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Vita ya Ulimwengu ya Kwanza na Mwanzo wa Huzuni Mbalimbali
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Vita Ambayo Itavimaliza Vita
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Bado Kuna Tisho la Vita vya Nyuklia?
    Amkeni!—2004
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
w08 4/1 kur. 3-4

“Vita Vya Kukomesha Vita Vyote”

‘Nawaahidi kwamba hivi ndivyo vita vya mwisho, vita vya kukomesha vita vyote.’ —WOODROW WILSON, RAIS WA MAREKANI (1913-1921).

HAYO ndiyo yaliyokuwa matarajio mazuri ya kiongozi wa nchi moja miaka 90 hivi iliyopita, Vita vya Kwanza vya Ulimwengu vilipokwisha. Mapambano hayo ya ulimwenguni pote yalikuwa yenye kutisha sana hivi kwamba washindi walitaka na walihitaji kuamini kuwa mambo mengi waliyodhabihu yangeleta faida za kudumu. Lakini mara nyingi, vita vya wanadamu havisuluhishi matatizo wala hata kuondoa chanzo chenyewe cha vita.

Miaka 20 hivi iliyopita baada ya Rais Wilson kutoa ahadi hiyo bila kufikiri, Vita vya Pili vya Ulimwengu vikazuka. Vilisababisha vifo na uharibifu mkubwa zaidi kuliko vile vya kwanza. Miaka 20 ya maendeleo ya kiteknolojia yalifanya wanadamu waboreshe sana ustadi wao wa kuwaua watu wengi. Vita vya Pili vya Ulimwengu vilipokuwa vikikaribia kwisha, viongozi ulimwenguni pote walitambua kwamba kulikuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa vita kutokea.

Mnamo 1945, Jenerali wa Marekani, Douglas MacArthur, alisema hivi: “Tumepata nafasi ya mwisho ya kumaliza vita. Tukishindwa kupata mfumo bora na unaofaa zaidi, Har–Magedoni itakuwa mlangoni.”

Jenerali MacArthur alijua matokeo mabaya ya bomu mbili za atomu zilizoangushwa huko Nagasaki na Hiroshima siku za mwisho za Vita vya Pili vya Ulimwengu. Uharibifu mbaya wa majiji hayo mawili ya Japani yalimfanya alipe neno “Har–Magedoni” maana mpya, yaani, maangamizi makubwa ya nyuklia ambayo yanaweza kuangamiza kabisa watu katika sayari yetu.

Wasiwasi kuhusu uwezekano wa maangamizi ya nyuklia unaendelea kuwakumba wanadamu. Kufikia miaka ya 1960, mataifa yenye nguvu zaidi ulimwenguni yalitumia mbinu ya “uhakikishiano wa kuangamizana.” Lengo lao lilikuwa kuwa na makombora ya kutosha ya nyuklia au njia za kurusha makombora hayo ambazo zitahakikisha kwamba asilimia 25 ya raia na asilimia 50 ya viwanda vya adui zao vimeangamizwa haidhuru ni nani aliyeanzisha vita hivyo. Watu wachache tu ndio waliofikiri kwamba mbinu hiyo ingedumisha amani ulimwenguni.

Leo, silaha za nyuklia zinazidi kuongezeka na vita katika maeneo mbalimbali vinaendelea kusababisha vifo vingi. Bado wanadamu wanakabili tisho la maangamizi makubwa ya nyuklia. Ingawa watu wanatamani kuona vita vikikomeshwa, ni wachache wanaoamini kwamba vita fulani au mbinu nyingine itavikomesha.

Hata hivyo, Biblia inaeleza kuhusu vita vya pekee vitakavyokomesha vita vyote. Inaita vita hivyo “Har–Magedoni,” neno ambalo mara nyingi watu wanalihusianisha na maangamizi makubwa ya nyuklia. Kwa kweli, Har–Magedoni itakomesha vita jinsi gani? Habari inayofuata itajibu swali hilo.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

DTRA Photo

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 4]

Nagasaki, Japan, 1945: USAF photo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki