Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w96 4/1 uku. 31
  • Imani Ilimsukuma Kutenda

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Imani Ilimsukuma Kutenda
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
w96 4/1 uku. 31

Imani Ilimsukuma Kutenda

YEHOVA alipomwagiza Musa aongoze taifa la Israeli kutoka utumwa wa Kimisri, mwanzoni Musa alitoa udhuru, akisema: “Ee Bwana, mimi si msemaji, tokea zamani, wala tokea hapo uliposema na mtumishi wako; maana mimi si mwepesi wa kusema, na ulimi wangu ni mzito.” (Kutoka 4:10) Naam, Musa alihisi hastahili kupewa mgawo huo mzito.

Vivyo hivyo leo, nyakati nyingine wengi wa watumishi wa Yehova huhisi wamepungukiwa katika kutimiza wajibu wao ambao wamegawiwa. Kwa kielelezo, mwangalizi mmoja Mkristo aitwaye Theodore asimulia: “Kati ya mambo yote ambayo Yehova aniambia nifanye, huduma ya shambani ndilo jambo gumu zaidi. Nilipokuwa mchanga, nilitembea haraka hadi mlangoni, nikijisingizia kupiga kengele ya mlango, na kwenda zangu kimya, nikitumaini hakuna mtu atanisikia au kuniona. Nilipokuwa mkubwa, niliacha kufanya hivyo, lakini wazo la kwenda mlango kwa mlango lilinifanya niwe mgonjwa kihalisi. Hata leo hii, mimi huwa mgonjwa kabla ya kwenda kwenye huduma, lakini mimi huenda hata iweje.”

Ni nini lililomfanya Musa na Mashahidi wa siku ya kisasa kama vile Theodore wakabiliane na woga kama huo? Biblia hujibu: “Kwa imani [Musa] akatoka Misri, . . . maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana.”—Waebrania 11:27.

Kwa kweli, kwa kudhihirisha imani katika Yehova, Musa aliweza kushinda hisia zake za kupungukiwa na kutimiza mgawo wake aliopewa alipokuwa hakimu, nabii, kiongozi wa taifa, mpatanishi wa agano la Sheria, kamanda, mwanahistoria, na mwandikaji wa Biblia.

Vivyo hivyo, tunapokuwa na imani kama ya Musa, tutatembea kama ‘tumwonaye asiyeonekana.’ Imani kama hiyo huchochea moyo mkuu, ikituwezesha kutimiza madaraka yetu ya Kikristo—hata tukihisi kwamba tumepungukiwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki