Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w96 10/15 uku. 3
  • Je, Kuna Uhai Baada ya Kifo?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Kuna Uhai Baada ya Kifo?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Swali la Muda Mrefu
  • Kuchunguza kwa Makini Mapokeo Fulani Kuhusu Kifo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
  • Kuna Sababu ya Kuwaogopa Wafu?
    Amkeni!—2009
  • Kwa Nini Sisi Huogopa Kifo?
    Amkeni!—2007
  • Ni Nini Hutokea Tunapokufa?
    Furahia Maisha Milele!—Masomo ya Kujifunza Biblia
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
w96 10/15 uku. 3

Je, Kuna Uhai Baada ya Kifo?

MASWALI mawili yamewasumbua wanadamu kwa mileani kadhaa: Mbona ni lazima tuzeeke na hatimaye tufe? Je, kuna aina yoyote ya uhai wenye fahamu baada ya kifo?

Swali la kwanza limewasumbua watu wengi kwa sababu hata sayansi ya kitiba ya kisasa, ikiwa na mavumbuzi yayo yote yenye kuvutia, haijaweza kutokeza jibu mkataa au lenye kuridhisha.

Swali la pili limekuwa na wingi wa majibu yanayotofautiana. Hata hivyo, kwa ujumla majibu juu ya ikiwa kuna uhai wenye fahamu baada ya kifo yamegawanyika kati ya wale waonao kwa hakika kuwa uhai sio uu huu tu na wale wanaoshikilia sana kwamba uhai wenye fahamu huishia kwenye kifo. Walio wengi wa kikundi hicho cha pili hutuambia kwamba hakuna shaka akilini mwao kwamba muda wa uhai wa mwanadamu ulio mfupi ndiyo yote awezayo kutazamia. Mara nyingi, majibizano yoyote ya kupinga yatolewayo hupata jibu hili la kinaya, “Hakuna yeyote ambaye amerudi kutuambia, sivyo?”

Sawa na maswali mengine yenye ubishi, kuna wengi ambao bado hawajafanya uamuzi—wakionyesha kwamba sikuzote wako tayari kushawishwa kuelekea upande mmoja au mwingine. Lakini wengine watajibu hivi, labda kwa kukosa staha, “Tutalazimika kungoja tuone wakati ufikapo!”

Swali la Muda Mrefu

Swali la mapema juu ya uhai baada ya kifo lilizushwa miaka ipatayo 3,500 iliyopita na yule mtu wa Mashariki ajulikanaye sana Ayubu, aliye maarufu kwa sababu ya subira yake ajapoteseka. Hivi ndivyo Ayubu alivyouliza swali lake: “Mwanadamu hufa na huzikwa chini; hupumua mara yake ya mwisho naye hayupo tena. Kama vile maji yapoteavyo kutoka baharini au bonde la mto likosavyo maji na kukauka, ndivyo mtu alalavyo asiamke . . . Mtu akifa, je, ataishi tena?”—Ayubu 14:10-14, New International Version.

Lakini Ayubu hakuwa peke yake katika kuuliza juu ya uhai baada ya kifo. Kichapo Encyclopædia of Religion and Ethics chini ya kichwa “Hali ya Wafu” chatoa habari hii yenye kuelimisha: “Hakuna habari ihusianayo na uhai wa nafsi yake ambayo imeshughulisha sana akili ya mwanadamu kama ile juu ya hali yake baada ya kifo. Kwa ujumla [wenyeji] katika sehemu zote za ulimwengu wana dhana zilizo wazi na dhahiri juu ya ulimwengu wa roho—uhai wao, sifa zao, na mandhari yao—na jambo hilo hudokeza kufikiriwa sana kwa habari hiyo. Kuwahofu wafu kulikoenea huelekeza kwenye wazo la kikale sana kwamba hali ya wafu haikuwa ile ya mwisho wa uhai. Kifo kilikuwa kimekatiza nishati; hilo lilikuwa wazi vya kutosha; lakini je, hakukuwa na nishati nyingine zenye kufanya kazi, au je, nishati hizo hazingeweza kujionyesha kwa njia ya hila, ya kifumbo? Mwanzoni watu wawe waliamini katika roho, nafsi, au mzuka, ulio mbali na mwili, au la, yaonekana kuna kila sababu ya kuamini kwamba waliwaona wafu kuwa bado waliendelea kuwako kwa njia fulani.”

Huenda ukafaana na kikundi kimoja kati ya vile vitatu vilivyotajwa hapo juu: huna uhakika juu ya kile kinachotukia baada ya kifo; mwenye kusadiki kwamba kuna uhai wa aina fulani baada ya kifo; au mwenye kusadiki kwamba uhai ndio uu huu tu. Liwalo lote, twakualika uchunguze kwa uangalifu makala ifuatayo. Ona ikiwa ndani yayo utaona ithibati ya Kibiblia yenye kusadikisha ya kwamba kuna taraja la ajabu la uhai wenye furaha baada ya kifo, jinsi utakavyokuja, wapi, na lini.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki