Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w96 12/15 uku. 32
  • Manufaa za Moyo Mtulivu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Manufaa za Moyo Mtulivu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
w96 12/15 uku. 32

Manufaa za Moyo Mtulivu

SAYANSI ya kitiba ya kisasa imejua kwa muda mrefu kwamba hasira isiyodhibitiwa ina matokeo yenye kudhuru mwili wa kibinadamu. Miaka zaidi ya mia moja iliyopita, jarida The Journal of the American Medical Association (JAMA) lilisema hivi: “Mtu anaanguka na kufa akiwa na hasira-kali, kisha labda yasemwa kwamba alikuwa na moyo mdhaifu, ambao haukuweza kuvumilia mkazo uliowekewa na hali yake ya akilini. Hakuna aonekanaye kufikiri kwamba kifo chake ni mwisho tu wa mfululizo mrefu wa hasira-kali hizo za kichaa, ambao umesababisha udhaifu unaotajwa.”

Maneno yaliyo juu hayawashangazi wanafunzi wa Neno la Mungu, Biblia hata kidogo. Karne zipatazo 29 kabla ya jarida JAMA kusema waziwazi juu ya hatari za hamaki mbaya, Mfalme Sulemani alipuliziwa kuandika hivi: “Moyo ulio mzima [“mtulivu,” NW] ni uhai wa mwili.” (Mithali 14:30) Maneno hayo yangali kweli leo.

Kwa kudumisha mwelekeo mtulivu, twaepushwa na yale magonjwa mengi ambayo mara nyingi huhusiana na mkazo, kama vile msukumo wa damu ulioongezeka, maumivu ya kichwa, na matatizo ya kupumua. Hata hivyo, zaidi ya afya iliyoboreshwa, mahusiano yetu pamoja na wengine yatanufaika tukijitahidi ‘kukomesha hasira na kuacha ghadhabu.’ (Zaburi 37:8) Siku zote watu walivutwa kumwelekea Yesu kwa sababu ya tabia yake pole na hangaikio lake la moyoni kwa ajili yao. (Marko 6:31-34) Hali kadhalika, tutakuwa chanzo cha burudisho kwa wengine tukisitawisha moyo mtulivu.—Mathayo 11:28-30.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki