Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w97 4/15 uku. 32
  • Ugavi wa Chakula wa Kutosha Ulimwenguni Wahakikishwa—Vipi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ugavi wa Chakula wa Kutosha Ulimwenguni Wahakikishwa—Vipi?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
w97 4/15 uku. 32

Ugavi wa Chakula wa Kutosha Ulimwenguni Wahakikishwa—Vipi?

“HUENDA jitihada zetu zilizo bora zaidi zisitoshe kudumisha ugavi wa chakula wa kutosha ambao tumepata kwa sehemu iliyo kubwa ya karne hii,” adai Lester Brown, msimamizi wa Worldwatch Institute katika Washington, D.C. Kulingana na gazeti New Scientist, mwanzoni mwa 1995, akiba za nafaka za ulimwengu zilishuka hadi tani milioni 255 kiwango cha chini zaidi kupata kutokea—nafaka ya kutosha kulisha ulimwengu kwa siku 48 tu. Katika miaka ya nyuma wakati akiba za nafaka zingeweza kulisha ulimwengu kwa siku 60 au chache, ugavi uliweza kurudia hali ya kawaida. Lakini sasa Worldwatch halina uhakika juu ya uwezo wa dunia wa kupata tena ugavi ambao imepoteza.

Baada ya miaka mitatu ya mavuno mabaya na kukiwa na nchi nyingi zaidi zinazositawi zikitumia nafaka kwa ajili ya kulisha mifugo, kuna nafaka kidogo zaidi ipatikanayo kwa ajili ya maskini wenye kuihitaji kuwa sehemu ya msingi wa mlo wao. Gazeti New Scientist laonya kwamba ikiwa hii hali haitapokea uangalifu mara moja, watu bilioni moja wanaotumia angalau asilimia 70 ya mapato yao kwa chakula huenda wakaanza kufa njaa.

Biblia ilitabiri kwamba wakaao duniani katika wakati wetu wangepatwa na “upungufu wa chakula.” (Luka 21:11) Hata hivyo Mungu hapuuzi hilo tatizo. Kwa kweli, hangaiko lake kwa ajili ya hali mbaya ya mwanadamu mwishowe litaonyeshwa Ufalme wake utakapoongoza mambo ya dunia. Wakati huo ‘nchi itatoa mazao yake.’ ‘Kutakuwa na wingi wa nafaka katika ardhi juu ya milima.’ (Zaburi 67:6; 72:16) Kisha maneno haya ya unabii kuhusu Muumba yatatimizwa: “Umeijilia nchi na kuisitawisha, . . . Mabonde yamepambwa nafaka.”—Zaburi 65:9, 13.

Je, ahadi hiyo ya ajabu inakuvutia? Je, ungependa kujua jinsi uwezavyo kuwa sehemu yayo? Basi waulize Mashahidi wa Yehova wakueleze zaidi juu ya Paradiso hiyo iliyoahidiwa wakutembeleapo wakati ujao. Ikiwa ungependa mtu fulani aje nyumbani kwako ili aongoze funzo la Biblia pamoja na wewe bila malipo, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani ihusuyo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 2.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]

Picha-ndani: Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki