Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w97 8/1 uku. 30
  • Vitabu, Vitabu, Vitabu!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Vitabu, Vitabu, Vitabu!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
w97 8/1 uku. 30

Vitabu, Vitabu, Vitabu!

“Hakuna mwisho wo wote wa kutunga vitabu vingi,” aliandika Mfalme Sulemani mwenye hekima wa zamani. (Mhubiri 12:12) Katika 1995 kwa wastani kitabu kimoja kipya kilichapishwa katika Uingereza kwa kila watu 580 kati ya wakazi wa huko, ikifanya nchi hiyo iwe inayoongoza ulimwenguni pote katika kuchapisha vitabu vipya. China, nchi iliyo na wakazi wengi zaidi, ilikuwa ya pili ikiwa na chapa 92,972 zikilinganishwa na zile 95,015 za Uingereza. Ujerumani ilifuata (vitabu 67,206), kisha Marekani ikafuata (49,276), ikifuatiwa na Ufaransa (41,234). “Sababu ya Uingereza kuongoza ulimwenguni pote ni kwa kuwa Kiingereza hutumiwa sana,” laandika gazeti la habari The Daily Telegraph la London.

Ripoti zaonyesha kwamba uuzaji wa vitabu umekuwa ukipungua kwa miaka kadhaa, na sasa ni asilimia 80 tu ya watu wazima katika Uingereza wanaonunua kitabu kimoja au zaidi kila mwaka. Lakini je, watu husoma vitabu vyote wanavyonunua?

Kitabu kimoja kinachoendelea kugawanywa sana na kusomwa sana ni Biblia, inayopatikana sasa ikiwa sehemu au yote nzima katika lugha zaidi ya 2,120. Ikiwa huna nakala bado, wasiliana na ofisi ya Watch Tower Society iliyo karibu zaidi nawe ili upate moja. Ikiwa una Biblia, ichukue na kuchunguza marejezo ya Kimaandiko yanayopatikana katika makala zilizo katika gazeti hili. Kwa kufanya hivyo, utavumbua ujuzi wa Biblia upao uhai.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki