Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w97 8/15 uku. 32
  • Walisimama Imara Katikati ya Mnyanyaso wa Nazi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Walisimama Imara Katikati ya Mnyanyaso wa Nazi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
w97 8/15 uku. 32

Walisimama Imara Katikati ya Mnyanyaso wa Nazi

UAMINIFU-MAADILI usio na hofu wa Mashahidi wa Yehova katika Ujerumani ya Nazi watokeza ukiwa tofauti kabisa na ule msimamo uliochukuliwa na makanisa ya Jumuiya ya Wakristo. Jambo hilo limeandikwa na profesa wa historia John Weiss katika kitabu chake Ideology of Death. Yeye aandika hivi:

“Katika 1934 kanisa la Kievanjeli lilisisitiza kwamba Wanazi lazima ‘wakaribishwe na Walutheri,’ na likashukuru ‘Bwana Mungu’ kwa kuwapa Wajerumani ‘kabaila mcha Mungu na mwenye kutumainika.’ . . . Askofu Mprotestanti aliwaandikia makasisi wake hivi, ‘[Hitler] ametumwa kwetu na Mungu.’” Weiss aendelea hivi: “Kanisa la Methodisti la Ujerumani . . . lilikubaliana na Askofu Dibelius kwamba Hitler alikuwa ameokoa Ujerumani kutoka katika mapinduzi ya Kibolsheviki, akileta amani na uthabiti . . . Kanisa la Mormon lilishauri waumini wake kwamba kumpinga Hitler kulikuwa kuvunja sheria ya Mormon.” Naye aongeza kusema hivi: “Wakatoliki waliambiwa kwamba kutii serikali mpya ya Nazi kulikuwa wajibu mtakatifu, wajibu ambao haukuondolewa kamwe hata baada ya machukizo ya mashariki kujulikana na makasisi.”

Lakini vipi juu ya Mashahidi wa Yehova? Profesa Weiss aonyesha kwamba “wakiwa kikundi, ni Mashahidi wa Yehova pekee waliowakinza Wanazi.” Maelfu yao walitiwa gerezani, aendelea Profesa Weiss, “ingawa Shahidi yeyote aliyepelekwa kwenye kambi ya mateso angaliweza kuachiliwa kwa kutia sahihi tu hati ya kukana imani yake.”

Kuhusu uaminifu-maadili wa Mashahidi wa Yehova, Profesa Weiss aeleza hivi: “Kielelezo chao chatolea kielezi kwa njia ya kipekee ule uvutano thabiti na wa kishujaa waliokuwa nao Wakristo wa mapema kabla kurasimishwa na kuhusika kwa Ukristo katika jamii hakujashinda kabisa ile tamaa ya maisha ya uaminifu-maadili. Kama vile padre Mprotestanti alivyoandika kuwahusu, ‘Si makanisa yatambuliwayo sana, bali watu hawa wachongewao na kudhihakiwa ndio waliosimama imara dhidi ya ghadhabu ya huyo roho mwovu wa Nazi, na waliojasiria kumpinga kulingana na imani yao.’”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki