Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w97 10/15 uku. 31
  • Ndoa ya Kibikira?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ndoa ya Kibikira?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
w97 10/15 uku. 31

Ndoa ya Kibikira?

KATIKA kujaribu kupatanisha ubikira wa Maria unaodaiwa kuwa wenye kudumu na kuolewa kwake na Yosefu, wachoraji na wachongaji wengi wa sanamu wamemwonyesha Yosefu kuwa mwanamume mzee-mzee. Walisababu kwamba Yosefu alikuwa kwa kweli kama mlezi kuliko kuwa mume wa Maria. Lakini hivi majuzi Papa John Paul wa Pili alitetea maoni tofauti juu ya jambo hilo. Yeye adokeza kwamba Yosefu “hakuwa mwanamume mzee-mzee wakati huo.” Badala ya hivyo, “ukamilifu wake wa ndani, uliotokana na zawadi kutoka kwa Mungu, ulimwongoza kuishi maisha yake ya ndoa pamoja na Maria bila tamaa ya kingono.”

Ikiwa Maria alinuia kubaki bikira milele, kwa nini alichumbiwa? “Huenda ikadhaniwa,” ajibu papa, “kwamba wakati wa uchumba wao kulikuwa na makubaliano kati ya Yosefu na Maria juu ya mpango wa kuishi akiwa bikira.”

Hata hivyo, Biblia hueleza jambo hilo kwa njia tofauti. Simulizi la Mathayo lasema kwamba Yosefu “hakufanya ngono naye hadi alipozaa mwana.” (Mathayo 1:25, New American Bible ya Katoliki, italiki ni zetu.) Baada ya kuzaliwa kwa Yesu, muungano wa kindoa wa Yosefu na Maria haukuwa kwa vyovyote wa kibikira. Ithibati moja juu ya jambo hilo ni kwamba baadaye katika simulizi la Gospeli, Yesu anaonyeshwa kuwa na ndugu na dada.—Mathayo 13:55, 56.

Hivyo, ingawa Biblia hutaarifu kwamba Maria alikuwa bikira alipomzaa Yesu, hakuna msingi wa kudai kwamba aliishi akiwa bikira maisha yake yote pamoja na Yosefu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki