Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w98 3/1 uku. 29
  • Madaktari, Mahakimu, na Mashahidi wa Yehova

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Madaktari, Mahakimu, na Mashahidi wa Yehova
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
w98 3/1 uku. 29

Madaktari, Mahakimu, na Mashahidi wa Yehova

HUKO nyuma katika Machi 1995, Mashahidi wa Yehova walifadhili semina mbili katika Brazili. Kusudi lilikuwa nini? Kutafuta ushirikiano wa wafanyakazi wa kitiba na wa kisheria wakati ambapo mgonjwa wa hospitali ni mmoja wa Mashahidi wa Yehova na hawezi kukubali kutiwa damu mishipani.—Matendo 15:29.

Kwa kuhuzunisha, katika visa fulani madaktari wamepuuza mapenzi ya wagonjwa Mashahidi, wakatafuta amri ya mahakama ili kulazimisha utiaji-damu mishipani. Katika visa hivyo Mashahidi walitumia njia zozote za kisheria zilizokuwa halali ili kujilinda. Hata hivyo, walipendelea ushirikiano badala ya kukabiliana. Hivyo, hizo semina zilikazia kwamba kulikuwa na njia nyingine za matibabu badala ya matibabu ya kutia mishipani damu inayofanana na ya mgonjwa na kwamba Mashahidi wa Yehova hukubali kwa kuterema njia hizo za badala.a

Mkutano wa Baraza la Kitiba la Kimkoa la São Paulo tayari ulikuwa umeunga mkono msimamo wa Mashahidi. Januari 1995 wakati ambapo hilo baraza lilikutania Jimbo la São Paulo, liliamua kwamba ikiwa matibabu yaliyopendekezwa na daktari yakataliwa, mgonjwa ana haki ya kuyakataa na kumchagua daktari mwingine.

Kwa kustahili pongezi, sasa kuna mamia ya wataalamu wa kitiba katika jumuiya ya kitiba ya Brazili walio tayari kutumia matibabu yasiyo ya damu kwa wagonjwa wao wanaoomba matibabu hayo. Tangu semina za Machi 1995, ushirikiano kati ya madaktari, mahakimu, na Mashahidi wa Yehova katika Brazili umeboreka kwa njia yenye kutokeza. Mwaka wa 1997 gazeti la kitiba la Brazili Âmbito Hospitalar lilichapisha makala iliyosisitiza kuheshimiwa kwa haki za Mashahidi wa Yehova za kuwa na msimamo wao wenyewe juu ya suala la damu. Sasa yatambuliwa na wengi kwamba, kama ilivyotaarifiwa na Mabaraza ya Kitiba ya Kimkoa ya Jimbo la Rio de Janeiro na la São Paulo, “wajibu wa daktari wa kulinda uhai wa mgonjwa haupaswi kupita wajibu wake wa kutetea haki ya kuchagua ya mgonjwa.”

[Maelezo ya Chini]

a Ili kupata habari zaidi, ona broshua Damu Yaweza Kuokoaje Uhai Wako?, iliyochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki