Kisiwa Kidogo Kilicho Mbali Sana
MANENO ambayo hutumiwa mara nyingi kufafanua kisiwa cha St. Helena ni “kidogo” na “mbali sana.” Hilo lafaa, kwa kuwa kisiwa hiki, chenye urefu wa kilometa 17 na upana wa kilometa 10, kiko umbali wa kilometa 1,950 kutoka nchi kavu iliyo karibu zaidi, yaani pwani ya kusini-magharibi mwa Afrika. Hapa ndipo Napoléon Bonaparte aliishi maisha yake ya mwisho akiwa uhamishoni katika mwaka wa 1815 baada ya kushindwa.
Kutoka baharini kisiwa hicho hufanana na ngome ngumu sana. Kisiwa hicho hasa ni volkeno-zimwe yenye miinuko ya ghafula kutoka Atlantiki ifikiayo kimo cha meta 500 hadi 700. Mlima Actaeon ulio katikati yake, ndio sehemu kubwa ya kisiwa hicho chote ukiwa mwinuko wa meta 818. Kwa sababu ya pepo baridi za Atlantiki Kusini zivumazo daima, pamoja na mkondo wa bahari, kisiwa hicho kwa kawaida si chenye joto sana na tabia ya nchi ni yenye kupendeza. Lakini kutokea nyanda za mwambao hadi kwenye sehemu za ndanindani za milima, kuna namna-namna za halihewa na mimea.
Kisiwa cha St. Helena kimekuwa miliki ya Uingereza tangu mwisho-mwisho wa karne ya 17. Watu wachache wapatao 5,000 wana asili zenye mchanganyiko wa Kizungu, Kiasia, na Kiafrika. Lugha ya Kiingereza hutumiwa kote kisiwani, lakini hiyo huzungumzwa kwa lafudhi tofauti. Hakuna uwanja wa ndege hapa; ni meli tu inayokiunganisha na kisiwa hiki na ulimwengu mwingine, kukiwa na safari za kawaida kwenda Afrika Kusini na Uingereza. Kwa hakika, utangazaji wa televisheni ulikuja kuwapo tu katikati ya miaka ya 1990, ukifanikishwa na kiunganishi cha setilaiti.
Mapema katika miaka ya 1930, habari njema za Ufalme wa Mungu zilifika kwenye fuo hizo kwa mara ya kwanza. (Mathayo 24:14) Kwa miaka mingi, wakazi wengi wa kisiwa hicho wamepokea hazina hii ifanyayo utajiri wa vitu vya kimwili kuwa wenye umaana mdogo. (Mathayo 6:19, 20) Leo, kisiwa cha St. Helena kina uwiano mzuri wa Shahidi 1 kwa watu 31, uwiano bora kabisa ulimwenguni!
[Ramani katika ukurasa wa 24]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
St. Helena
JAMESTOWN
Levelwood
AFRIKA
BAHARI KUU ATLANTIKI
St. Helena