Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w99 5/1 uku. 25
  • Soma Pamoja na Watoto Wako

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Soma Pamoja na Watoto Wako
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
w99 5/1 uku. 25

Soma Pamoja na Watoto Wako

Kulingana na gazeti Veja la Brazili, watoto ambao wazazi wao husoma kwa bidii wana mwelekeo mkubwa zaidi wa kupenda vitabu kuliko watoto wasio na kielelezo kama hicho cha kusoma nyumbani. “Kusoma pamoja huimarisha uhusiano kati ya wazazi na watoto na humsaidia mtoto aelewe yaliyomo katika kitabu kwa njia bora,” ataarifu Martha Hoppe, mtaalamu wa ukuzi wa watoto.

Kusomea watoto wako kwa sauti pia hukupa wewe fursa ya kujibu maswali. Unaweza kujadili picha zinazoandamana na maandishi. “Kadiri mtoto aelewavyo yaliyomo katika vitabu,” asema Hoppe, “ndivyo atakavyochochewa zaidi kuvitafuta anapokuwa na tamaa ya kuvisoma.”

Wazazi wengi miongoni mwa Mashahidi wa Yehova hufurahia kusoma na watoto wao. Wao huenda wakasoma vichapo kama Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, Kumsikiliza Mwalimu Mkuu, na Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi.a Vitabu kama hivyo huwasaidia watoto wasome kwa ufasaha na pia husitawisha upendezi wao katika kitabu kinachouzwa kuliko vyote duniani—Biblia Takatifu. Kwa hiyo, ikiwa wewe ni mzazi, wawekee watoto wako mfano kwa kuwa msomaji mwenye bidii wa Neno la Mungu. (Yoshua 1:7, 8) Kwa vyovyote vile, tumia wakati ukiwasomea!

[Maelezo ya Chini]

a Kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki