Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w00 12/15 uku. 32
  • “Jambo Linalopasa Kumfurahisha Kila Mtu”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Jambo Linalopasa Kumfurahisha Kila Mtu”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
w00 12/15 uku. 32

“Jambo Linalopasa Kumfurahisha Kila Mtu”

TUVALU, nchi nzuri ambayo imefanyizwa na visiwa tisa katika Pasifiki Kusini, ina watu wapatao 10,500. Hata hivyo, wakitambua kwamba “mapenzi [ya Mungu] ni kwamba watu wa namna zote waokolewe na kuja kwenye ujuzi sahihi wa kweli,” Mashahidi wa Yehova wa nchi hiyo walitamani sana kuwa na vichapo vinavyotegemea Biblia katika lugha yao wenyewe. (1 Timotheo 2:4) Jambo hilo lilikuwa gumu kwa sababu hakukuwa na kamusi ya lugha hiyo. Mwaka wa 1979, mishonari mmoja wa Mashahidi wa Yehova aliyekuwa akitumikia huko Tuvalu, alikubali kufanya kazi hiyo ngumu. Yeye na mkewe waliishi pamoja na familia fulani ya wenyeji, wakajifunza lugha hiyo, na hatua kwa hatua wakaandika faharasa ya maneno ya Kituvalu. Mwaka wa 1984, kitabu Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani kilichapishwa katika Kituvalu na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

Dakt. T. Puapua, aliyekuwa waziri mkuu wa Tuvalu, aliandika barua ya kushukuru kwa ajili ya kitabu Kuishi Milele. Aliandika hivi: “Kitabu hiki ni ‘urithi’ mwingine mpya na muhimu kwa Tuvalu. Mwapaswa kufurahia sana sehemu mliyotimiza—sehemu iliyo muhimu sana katika kujenga hali ya kiroho ya watu wa taifa hili. Ni matumaini yangu kwamba kitabu hiki kitatiwa ndani ya historia ya Tuvalu inayohusu kuchapisha vitabu vya elimu. . . . [Utimizo] huo ni jambo linalopasa kumfurahisha kila mtu.”

Orodha ya maneno iliyokusanywa na mtafsiri huyo iliwezesha kuchapishwa kwa kamusi ya Kituvalu-Kiingereza mwaka wa 1993. Ilikuwa kamusi ya kwanza kupatikana kwa umma katika lugha hiyo. Hivi majuzi, Baraza la Kitaifa la Lugha Nchini Tuvalu liliomba idhini ya kutumia kamusi hiyo ili kutayarisha kamusi yao ya kwanza ya lugha ya kienyeji.

Tangu Januari 1, 1989, toleo la kila mwezi la gazeti Mnara wa Mlinzi limekuwa likichapishwa katika Kituvalu. Ikiwa unasoma gazeti hili katika lugha yako ya pili, mbona usiangalie ukurasa wa 2 na kuona ikiwa lugha yako ya kwanza imetiwa ndani katika lugha ambazo Mnara wa Mlinzi huchapishwa? Bila shaka kulisoma katika lugha yako ya mama kutafanya ufurahi hata zaidi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki