Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w01 11/15 kur. 2-4
  • Je, Kuna Tumaini Lolote la Wokovu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Kuna Tumaini Lolote la Wokovu?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Habari Zinazolingana
  • Dumisha ‘Tumaini Lako la Wokovu’!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Wokovu—Inachomaanisha kwa Kweli
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Jambo Ambalo Ni Lazima Tufanye Ili Tuokolewe
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Wokovu Ni Nini?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
w01 11/15 kur. 2-4

Je, Kuna Tumaini Lolote la Wokovu?

Karne ya 20 imetajwa kuwa mojawapo ya karne zenye mauaji mengi zaidi ambayo wanadamu wamewahi kushuhudia. Uhalifu, vita, vita kati ya makabila, matumizi mabaya ya dawa za kulevya, ukosefu wa unyofu, na jeuri vimeongezeka sana hasa katika miaka michache iliyopita. Isitoshe, kuna maumivu na mateso ambayo yamesababishwa na magonjwa, uzee, na kifo. Ni nani asiyetamani kuondolewa kwa matatizo hayo makubwa yaliyopo ulimwenguni leo? Tunapotazamia wakati ujao kwa hamu, je, kuna tumaini lolote la wokovu?

FIKIRIA maono aliyopewa mtume Yohana miaka 2,000 hivi iliyopita. Aliandika hivi: “Tazama! Hema la Mungu liko pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao, nao watakuwa vikundi vya watu wake. Na Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kabisa kila chozi kutoka katika macho yao, na kifo hakitakuwapo tena, wala ombolezo wala kupaaza kilio wala umivu halitakuwapo tena kamwe. Mambo ya zamani yamepitilia mbali.” (Ufunuo 21:3, 4) Vivyo hivyo, nabii Isaya alitabiri hivi: “Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo.”—Isaya 25:8.

Hebu wazia kile kitakachomaanishwa na kutimizwa kwa ahadi za Mungu! Wanadamu wataokolewa au kukombolewa kutokana na uonezi na jeuri, kutokana na mateso na taabu. Kwani, hata hatutasumbuliwa na magonjwa, uzee, na kifo! Neno la Mungu, Biblia, linaahidi uhai udumuo milele chini ya hali kamilifu duniani. (Luka 23:43; Yohana 17:3) Na uhai huo unapatikana kwa wote wanaoutamani. “Mapenzi [ya Mungu] ni kwamba watu wa namna zote waokolewe na kuja kwenye ujuzi sahihi wa kweli.”—1 Timotheo 2:3, 4.

Hata hivyo, ili tunufaike na ahadi za Mungu, lazima tuelewe daraka la Yesu Kristo katika wokovu wetu na kudhihirisha imani katika yeye. Yesu mwenyewe alisema hivi: “Mungu aliupenda ulimwengu sana hivi kwamba akatoa Mwana mzaliwa-pekee wake, ili kila mtu anayedhihirisha imani katika yeye asipate kuangamizwa bali awe na uhai udumuo milele.” (Yohana 3:16) Akitaja daraka muhimu la Yesu Kristo kuhusiana na wokovu, mtume Petro alisema: “Hakuna wokovu katika mwingine yeyote, kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu ambalo limepewa miongoni mwa watu ambalo kwalo lazima sisi tupate kuokolewa.” (Matendo 4:12) Mtume Paulo na mwenzake Sila walimshauri hivi mtu fulani aliyeuliza kwa unyofu: “Amini juu ya Bwana Yesu nawe utapata kuokolewa, wewe na watu wa nyumbani mwako.”—Matendo 16:30, 31.

Naam, Yesu Kristo ndiye “Wakili Mkuu wa uhai,” na wokovu unawezekana tu kupitia kwake. (Matendo 3:15) Lakini mtu mmoja anawezaje kuwa na daraka kubwa hivyo la kutuokoa? Kuelewa daraka lake kuhusiana na wokovu kutaimarisha tumaini letu la wokovu.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 2]

Ukurasa wa 3: Ndege za kurushia makombora: USAF photo; watoto wenye njaa: UNITED NATIONS/J. FRAND; meli ya kivita inayoteketea: U.S. Navy photo ▸

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki