Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w03 5/15 uku. 3
  • Maandishi Yenye Kuvutia Sana

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maandishi Yenye Kuvutia Sana
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Maandishi ya Noa Yana Maana Kwetu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Simulizi la Noa na Gharika Kuu—Je, Ni Hekaya Tu?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Noa Auhukumu Ulimwengu kwa Imani Yake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Safina ya Noa
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
w03 5/15 uku. 3

Maandishi Yenye Kuvutia Sana

KUANZIA mwaka wa 1928 hadi 1956 mvumbuzi Richard E. Byrd alisafiri barani Antaktika mara tano. Kwa kuwa aliandika habari sahihi kuhusu safari zake, yeye na wenzake waliweza kujua mkondo wa upepo, wakachora ramani, na kukusanya habari nyingi kuhusu bara la Antaktika.

Safari za Byrd zinaonyesha umuhimu wa kuhifadhi maandishi kuhusu safari. Kwa kweli, marubani wanapaswa kuandika kuhusu safari za ndege, ilhali manahodha wanapaswa kuandika kuhusu safari za meli. Baadaye, habari hizo zinaweza kutumiwa kuchunguza mambo yaliyotukia au kuchanganua habari zinazoweza kutumiwa wakati ujao.

Maandiko yana masimulizi yenye kuvutia kuhusu Gharika ya siku za Noa. Gharika hiyo ilichukua muda unaozidi mwaka mmoja. Ili kujitayarisha kwa ajili ya Gharika hiyo, Noa, mke wake, na watoto wake watatu wa kiume, pamoja na wake zao, walijenga safina kwa muda wa miaka 50 au 60. Safina hiyo ilikuwa na ukubwa wa meta 133.5 x 22.3 x 13.4. Ilikuwa ya kazi gani? Ya kuhifadhi wanadamu na wanyama wasiharibiwe na Gharika.—Mwanzo 7:1-3.

Kitabu cha Biblia cha Mwanzo kina maandishi ya Noa kuhusu mambo yaliyotukia tangu Gharika ilipoanza hadi yeye na familia yake walipotoka ndani ya safina. Je, maandishi hayo yana maana yoyote kwetu leo?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki