Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w03 10/1 uku. 32
  • Je, Wewe ‘Unapiga Teke Michokoo’?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wewe ‘Unapiga Teke Michokoo’?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
w03 10/1 uku. 32

Je, Wewe ‘Unapiga Teke Michokoo’?

KATIKA nyakati za Biblia, mchokoo, yaani, fimbo ndefu ya chuma, ambayo kwa kawaida ilikuwa na ncha kali, ilitumiwa kuwasukuma na kuwaelekeza wanyama wenye kuvuta mizigo. Ingekuwaje kama mnyama angekataa kabisa kwenda hata baada ya kuchomwa-chomwa kwa mchokoo? Badala ya kupunguza maumivu, mnyama huyo angeumia hata zaidi.

Yesu Kristo aliyefufuliwa alitaja michokoo alipomtokea mtu aitwaye Sauli, aliyekuwa njiani kwenda kuwakamata baadhi ya wanafunzi wa Yesu. Katikati ya mwangaza mkali, Sauli alimsikia Yesu akisema: “Sauli, Sauli, kwa nini unaninyanyasa mimi? Kufuliza kupiga teke dhidi ya michokoo hufanya iwe vigumu kwako.” Kwa kuwanyanyasa Wakristo, Sauli alikuwa hasa anapigana na Mungu, jambo ambalo lingemdhuru tu.—Matendo 26:14.

Je, sisi pia tunaweza kuwa ‘tunapiga teke michokoo’ bila kujua? Biblia hulinganisha ‘maneno ya wenye hekima’ na michokoo ambayo hutuchochea kusonga mbele katika njia inayofaa. (Mhubiri 12:11) Tukikubali shauri la Neno la Mungu lililoandikwa kwa mwongozo wa roho yake, shauri hilo linaweza kutuchochea na kutuongoza kwa njia inayofaa. (2 Timotheo 3:16) Kukataa mwongozo huo kunaweza tu kutudhuru.

Sauli alitii maneno ya Yesu, akabadilika, na kuwa mtume Mkristo Paulo, aliyependwa sana. Kwa kutii shauri la Mungu, sisi pia tutabarikiwa milele.—Mithali 3:1-6.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]

L. Chapons/Illustrirte Familien-Bibel nach der deutschen Uebersetzung Dr. Martin Luthers

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki