Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w04 5/15 kur. 2-3
  • Jitihada ya Wanadamu ya Kumpendeza Mungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jitihada ya Wanadamu ya Kumpendeza Mungu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Habari Zinazolingana
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2004
  • Unaweza Kuyapata Wapi Mafundisho ya Kweli?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2000
  • Ni Nini Hutokea Wakati wa Kifo?
    Wewe Unaweza Kuwa Rafiki ya Mungu!
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
w04 5/15 kur. 2-3

Jitihada ya Wanadamu ya Kumpendeza Mungu

“SIKUZOTE imani katika Mungu imekuwa muhimu katika jamii zote za kibinadamu. Kwa kawaida Mungu huonwa kuwa Muumba mwenye kuudhibiti ulimwengu wote. Imekuwa hivyo hata katika jamii zisizoamini kwamba kuna Mungu,” asema John Bowker katika kitabu chake God—A Brief History. Kwa njia fulani, jitihada ya kumtafuta Mungu na kupata kibali chake imekuwa jambo la kawaida kati ya wanadamu. Ulimwenguni pote, watu wengi hutaka kwa unyoofu kumpendeza Mungu. Bila shaka, njia ambazo wao hutumia ili kufanya hivyo zinatofautiana kulingana na imani zao.

Baadhi yao huamini kwamba jambo muhimu zaidi ili kupata kibali cha Mungu ni kuishi maisha ya unyoofu. Wengine hufikiri kwamba wanaweza kupata kibali cha Mungu kwa kutoa misaada kwa walio maskini. Isitoshe, sherehe na desturi za kidini ni muhimu kwa watu wengi.

Kwa upande mwingine, kuna wale wanaoamini kwamba haiwezekani kumfikia Mungu, yaani, yuko mbali sana na wanadamu au ni mwenye shughuli nyingi asiweze kuwafikiria watu wa kawaida. Yaelekea Epicurus, mwanafalsafa wa nchi ya kale ya Ugiriki, aliamini kwamba ‘miungu iko mbali sana isiweze kuathiri mambo ya wanadamu kwa njia yoyote ile.’ Hata hivyo, wengi walio na maoni kama hayo ni watu wa dini. Wengine huenda hata wakatoa dhabihu na kufanya matambiko wakitumaini kuwatuliza wazazi wao wa kale waliokufa.

Unaonaje? Je, ni kweli kwamba Mungu hutambua jitihada tunayofanya ili kupata kibali chake? Je, inawezekana kugusa hisia za Mungu na kumpendeza?

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 2]

COVER: Courtesy of ROE/Anglo-Australian Observatory, photograph by David Malin

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki