Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gf somo la 12 uku. 20
  • Ni Nini Hutokea Wakati wa Kifo?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ni Nini Hutokea Wakati wa Kifo?
  • Wewe Unaweza Kuwa Rafiki ya Mungu!
  • Habari Zinazolingana
  • Ni Nini Hutokea Tunapokufa?
    Furahia Maisha Milele!—Masomo ya Kujifunza Biblia
  • Wazazi Wetu wa Kale Wako Wapi?
    Je, Umeipata Barabara Inayoongoza Kwenye Uhai wa Milele?
  • Biblia Inasema Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
  • Kuna Sababu ya Kuwaogopa Wafu?
    Amkeni!—2009
Pata Habari Zaidi
Wewe Unaweza Kuwa Rafiki ya Mungu!
gf somo la 12 uku. 20

SOMO LA 12

Ni Nini Hutokea Wakati wa Kifo?

Kifo ni kinyume cha uhai. Kifo ni kama usingizi mzito. (Yohana 11:11-14) Wafu hawawezi kusikia, kuona, kusema, wala kuwaza lolote. (Mhubiri 9:5, 10) Dini isiyo ya kweli hufundisha kwamba wafu huenda katika ulimwengu wa roho ili waishi na babu zao wa kale waliokufa. Biblia haifundishi hivyo.

Wafu hawawezi kutusaidia, wala hawawezi kutudhuru. Kwa kawaida, watu hufanya matambiko na kutoa dhabihu ambazo wanaamini kuwa zitawafurahisha wafu. Mambo hayo yanamchukiza Mungu kwa sababu yanategemea mojawapo ya uwongo mbalimbali wa Shetani. Vivyo hivyo, mambo hayo hayawezi kuwapendeza wafu, kwa kuwa hawana uhai. Hatupaswi kuogopa wala kuabudu wafu. Tunapaswa kumwabudu Mungu peke yake.—Mathayo 4:10.

Wafu wataishi tena. Yehova atawaamsha wafu warudi kwenye uhai katika dunia paradiso. Jambo hilo litatendeka wakati ujao. (Yohana 5:28, 29; Matendo 24:15) Mungu aweza kuwaamsha watu ambao wamekufa kama vile wewe uwezavyo kumwamsha mtu kutoka usingizini.—Marko 5:22, 23, 41, 42.

Wazo la kwamba sisi hatufi ni uwongo ambao Shetani Ibilisi anaeneza. Shetani na roho wake waovu hufanya watu wafikiri kwamba roho za wafu ziko hai nazo husababisha magonjwa na matatizo mengine. Shetani huwadanganya watu, nyakati nyingine kupitia ndoto na maono. Yehova huwashutumu wale wanaojaribu kuongea na wafu.—Kumbukumbu la Torati 18:10-12.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki