Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w05 3/15 uku. 32
  • Tukio Linalopaswa Kukumbukwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Tukio Linalopaswa Kukumbukwa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
w05 3/15 uku. 32

Tukio Linalopaswa Kukumbukwa

NI TUKIO gani hilo? Ni kifo cha mtu aliyekufa karibu miaka 2,000 iliyopita. Alisema hivi: “Ninaitoa nafsi yangu, ili nipate kuipokea tena. Hakuna mtu ambaye ameichukua kutoka kwangu, bali ninaitoa kwa uamuzi wangu mwenyewe.” (Yohana 10:17, 18) Mtu huyo alikuwa Yesu Kristo.

Yesu aliwaagiza wafuasi wake waadhimishe Ukumbusho wa kifo chake cha kidhabihu. Tukio hilo pia huitwa “Mlo wa Jioni wa Bwana,” au “chakula cha Bwana.” (1 Wakorintho 11:20; UV) Ukumbusho ambao Yesu alianzisha ili kuadhimisha kifo chake utaadhimishwa na Mashahidi wa Yehova na marafiki wao Alhamisi, Machi 24, 2005, baada ya jua kutua.

Hotuba inayotegemea Biblia itafafanua maana ya mkate usiotiwa chachu na divai nyekundu inayotumiwa wakati wa tukio hilo. (Mathayo 26:26-28) Pia hotuba hiyo itajibu maswali kama haya: Wakristo wanapaswa kuadhimisha tukio hilo mara ngapi? Ni nani wanaostahili kula mkate na kunywa divai? Ni nani wanaofaidika na kifo cha Yesu? Maadhimisho hayo muhimu yatawasaidia wote waelewe kusudi la maisha na kifo cha Yesu.

Utakaribishwa kwa uchangamfu kwenye Ukumbusho wa kifo cha Yesu. Tafadhali waulize Mashahidi wa Yehova wanaoishi katika eneo lenu kuhusu saa na mahali hususa pa kukutania.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki