Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w05 7/1 kur. 3-4
  • Jitihada za Kutafuta Amani ya Akili

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jitihada za Kutafuta Amani ya Akili
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Habari Zinazolingana
  • Kuridhika na Kuwa Mkarimu
    Amkeni!—2018
  • Furaha—Vigumu Kuipata
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Je, Mali Zaweza Kukufanya Uwe Mwenye Furaha?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Imani Katika Mungu—Je, yapaswa kuhitaji Muujiza?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
w05 7/1 kur. 3-4

Jitihada za Kutafuta Amani ya Akili

ALBERT alikuwa na ndoa yenye furaha na watoto wawili wazuri. Lakini alihisi kwamba anakosa kitu fulani maishani. Wakati fulani alipokuwa akijitahidi kupata kazi, alijiunga na siasa na kuunga mkono usoshalisti. Hata alipata kuwa mwanachama mwenye bidii wa chama cha Ukomunisti katika eneo lao.

Hata hivyo, Albert alikatishwa tamaa na Ukomunisti. Aliacha siasa na kujitolea kabisa kwa familia yake, akiwa na lengo la kuifanya iwe na furaha zaidi. Lakini bado Albert alihisi amekosa kitu fulani. Hakupata amani ya kweli ya akili.

Simulizi la Albert si la kushangaza. Mamilioni wamejaribu kufuata maoni mbalimbali ya kisiasa, ya kifalsafa, na ya kidini ili kupata kusudi la maisha. Harakati za mabadiliko za miaka ya 1960 katika nchi za Ulaya na Amerika Kaskazini zilikuwa uasi dhidi ya utamaduni na viwango vya jamii. Vijana walitafuta furaha na kusudi la maisha kwa kutumia dawa za kulevya zinazoharibu akili na kwa kufuata falsafa za harakati hizo zilizofundishwa na walimu na viongozi wao wa dini. Hata hivyo, harakati hizo hazikuleta furaha halisi. Badala yake, zilitokeza wazoefu wa dawa za kulevya na vijana waliopotoka, hivyo kufanya jamii ivurugike zaidi kimaadili.

Kwa karne nyingi, watu wengi wametafuta furaha kwa kujitahidi kupata mali, mamlaka, au elimu. Mwishowe jitihada hizo zote huvunja moyo. Yesu alisema hivi: “Hata wakati mtu ana vitu vingi uzima wake hautokani na vitu alivyo navyo.” (Luka 12:15) Kwa kawaida, kufuatilia sana mali hakuleti furaha. Biblia inasema hivi: “Wale ambao wameazimia kuwa matajiri huanguka katika jaribu na mtego na tamaa nyingi za kijinga na zenye kudhuru, ambazo hutumbukiza watu katika maangamizi na uharibifu. Kwa maana kupenda pesa ni chanzo cha mambo mabaya ya namna zote, na kwa kujitahidi kufikia upendo huo wengine . . . wamejichoma wenyewe kila mahali kwa maumivu mengi.”—1 Timotheo 6:9, 10.

Basi, mtu anawezaje kupata amani ya akili na kusudi la maisha? Je, hilo ni jambo la kujaribu-jaribu tu kama kulenga shabaha gizani? La. Kama tutakavyoona kwenye makala inayofuata suluhisho ni kutosheleza uhitaji muhimu na wa pekee sana wa mwanadamu.

[Picha katika ukurasa wa 3]

Je, kujitahidi kupata mali, mamlaka, au elimu kutakusaidia kupata amani ya akili?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki