Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w97 3/15 uku. 3
  • Imani Katika Mungu—Je, yapaswa kuhitaji Muujiza?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Imani Katika Mungu—Je, yapaswa kuhitaji Muujiza?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Sababu Inayofanya Miujiza Peke Yayo Isijenge Imani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Je, Kweli Miujiza Hutukia?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Ile Miujiza—Je! Kweli Ilitukia?
    Biblia—Neno la Mungu au la Binadamu?
  • Kwa Nini Upendezwe na Miujiza?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
w97 3/15 uku. 3

Imani Katika Mungu—Je, yapaswa kuhitaji Muujiza?

ALBERT alikuwa katika miaka yake ya mapema ya 20 alipoanza kumtafuta Mungu. Alijaribu dini kadha wa kadha lakini alibaki bila kuridhika. Akisoma visehemu vya Biblia, alijifunza jinsi Mungu alivyoshughulika na watu mmoja-mmoja kama vile Noa, Abrahamu, Sara, na Musa. Albert alijikuta akivutwa kwa Mungu wa Biblia. Hata hivyo, je, angeweza kuwa na hakika kwamba Mungu kwa kweli yuko?

Jioni moja Albert aliendesha gari hadi mahali palipo pekee ambapo alisali hivi, “Tafadhali Mungu, nipe ishara—yoyote ya kuthibitisha ya kuwa uko.” Albert alingoja na kungoja. Akumbuka kwamba wakati ambapo hakuna lolote lililofanyika, mataraja yake “yaligeuka kuwa kutamauka, kuwa utupu, kuwa hasira.”

Sawa na Albert, wengi huhisi kwamba wamemtafuta Mungu pasipo mafanikio. Huenda wakatatanishwa na mahubiri ya makasisi au kuzindushwa na kazi ya waeneza-evanjeli wa televisheni. Wakumbwapo na unafiki ulio dhahiri miongoni mwa majirani wao wengi, baadhi yao hawana hakika juu ya mambo ya kuamini. Hata hivyo, Mfalme Daudi wa Israeli la kale alimhakikishia mwanaye Solomoni hivi: “Ukimtafuta [Mungu], ataonekana nawe.”—1 Mambo ya Nyakati 28:9.

Hivyo basi, Mungu hujifunuaje? Je, wapaswa kutarajia ishara—jambo lililoonwa lisilo la kawaida litakalokuthibitishia kwamba Mungu yuko? Kulingana na hesabu za karibuni za watu waliotoa maoni yao zilizorekodiwa katika gazeti Time, zaidi ya thuluthi mbili za Wamarekani huamini katika miujiza. Makala hiyo ilionyesha pia kwamba “makanisa yenye kukua upesi zaidi katika Marekani ni yale makutaniko ya Karama na ya Pentekoste ambayo ibada yayo hukazia ‘ishara na maajabu.’”

Je, kwa kweli kuamini katika Mungu kwapaswa kuhitaji “ishara na maajabu”? Ametumia miujiza nyakati zilizopita. Kwa kutoa kielezi: Sauli wa Tarso, aliyekuwa akiwanyanyasa wafuasi wa Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, alijionea mambo yasiyo ya kawaida alipokuwa njiani kutoka Yerusalemu kuelekea Damasko. Kukabiliana huko kwa kimuujiza na Yesu aliyefufuliwa kuliongoza kwenye kugeuzwa imani kwa Sauli. (Matendo 9:1-22) Hivyo aliyekuwa mnyanyasaji zamani akawa mtume Paulo—mmoja wa wateteaji wa kwanza kabisa wa Ukristo!

Lakini je, miujiza huamsha itikio lenye kupendeza kama hilo sikuzote? Je, imani ya kweli katika Mungu inategemea kupata kwa mtu kujionea jambo fulani la kimuujiza?

[Picha katika ukurasa wa 3]

Mwana wa Mungu alizungumza kimuujiza na Sauli wa Tarso. Je, wapaswa kutarajia muujiza?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki