Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w05 11/1 uku. 15
  • “Mojawapo ya Siku Bora Maishani Mwangu”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Mojawapo ya Siku Bora Maishani Mwangu”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Habari Zinazolingana
  • Kukabiliana na Ugonjwa wa Asperger
    Amkeni!—2008
  • Mtoto Wako Atasema Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2005
  • Kutoka Mshuko wa Moyo Hadi Furaha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
w05 11/1 uku. 15

“Mojawapo ya Siku Bora Maishani Mwangu”

“KUSHUKA moyo ndilo tatizo kubwa zaidi la akili linalowakumba vijana ambalo huripotiwa mara nyingi,” lasema shirika la Beyondblue, linalodhaminiwa na serikali huko Australia. Uchunguzi unaonyesha kwamba vijana 100,000 hivi huko Australia hushuka moyo kila mwaka.

Hata vijana Wakristo hushuka moyo. Hata hivyo, imani katika Yehova imewasaidia wengi kushinda hisia za kushuka moyo na hivyo kufanikiwa wakiwa vijana. Kufanya hivyo kunakuwa na matokeo mazuri kwa wengine. Jinsi gani?

Fikiria hali ya Claire mwenye umri wa miaka 18. Yeye na mama yake ni wa kutaniko la Mashahidi wa Yehova la Melbourne. Baba yake alipowaacha, Claire alishuka moyo. Lakini imani yake iliendelea kuwa imara kwa Baba yake wa mbinguni, Yehova. Siku moja Lydia, ambaye ni daktari, alimtembelea Claire nyumbani ili kujua hali ya mama ya Claire ambaye alikuwa mgonjwa. Baadaye, alijitolea kumpeleka Claire madukani. Wakiwa njiani, alimuuliza Claire ikiwa ana rafiki mvulana. Claire akamweleza kwamba kwa kuwa yeye ni mmoja wa Mashahidi wa Yehova, hashirikiani na wavulana ili kujifurahisha tu. Daktari alishangaa. Kisha Claire akamweleza jinsi Biblia ilivyomsaidia kufanya maamuzi kwa hekima maishani. Hatimaye, Claire aliahidi kumpelekea daktari huyo kitabu kinachoifafanua Biblia ambacho kilimsaidia sana. Kitabu hicho ni Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi.

Siku tatu baada ya kupokea kitabu hicho, Lydia alimpigia simu mama ya Claire kumweleza jinsi alivyofurahia kukisoma. Kisha akaomba vitabu vingine sita kwa ajili ya wafanyakazi wenzake. Claire alipompelekea vitabu hivyo, daktari huyo alimweleza Claire jinsi alivyovutiwa na imani yake. Claire akajitolea kujifunza Biblia na daktari huyo, naye akakubali.

Kwa miezi kadhaa, Claire alijifunza pamoja na daktari huyo wakati wa mapumziko ya chakula cha mchana. Kisha, Lydia akamuuliza Claire ikiwa angependa kuhutubia mkutano unaozungumza kuhusu vijana walioshuka moyo. Claire alikubali ingawa alikuwa na wasiwasi. Zaidi ya watu 60 walihudhuria semina hiyo. Wataalamu wanne wa magonjwa ya akili ambao wote ni watu wazima waliwahutubia wasikilizaji. Kisha zamu ya Claire ikafika. Alionyesha jinsi ilivyo muhimu vijana kuwa na uhusiano pamoja na Mungu. Alieleza kwamba Yehova Mungu huwajali sana vijana na huwasaidia wale wote wanaomwendea ili kupata msaada na faraja. Isitoshe, alieleza usadikisho wake kwamba hivi karibuni Yehova ataondoa magonjwa yote ya kimwili na ya kiakili. (Isaya 33:24) Ushahidi huo mzuri ulikuwa na matokeo gani?

“Watu wengi walinijia baada ya semina hiyo kunieleza jinsi walivyovutiwa kusikia kijana akizungumza kumhusu Mungu,” akasema Claire. “Niliwaachia nakala 23 za kitabu Vijana Huuliza. Wasichana watatu waliohudhuria walinipa namba zao za simu. Mmoja wao sasa anajifunza Biblia. Hiyo ilikuwa mojawapo ya siku bora maishani mwangu.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki