Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w08 2/1 uku. 10
  • Mchungaji Anayejali

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mchungaji Anayejali
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Habari Zinazolingana
  • Mchungaji Mwenye Upendo
    Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Mahali pa Kupata Faraja
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Wasaidieni Kondoo Waliopotea
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • “Mimi Mwenyewe Nitawatafuta Kondoo Wangu”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2020
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
w08 2/1 uku. 10

Mkaribie Mungu

Mchungaji Anayejali

Mathayo 18:12-14

‘JE, Mungu ananijali?’ Huenda umejiuliza swali hilo. Wengine pia wamejiuliza. Wengi wetu tumekabili hali ngumu na matatizo, na nyakati nyingine huenda tukajiuliza ikiwa Muumba wa ulimwengu huu mkubwa anatujali. Tunapaswa kupata jibu la swali hili, Je, Yehova Mungu anatujali tukiwa watu mmoja-mmoja? Alipokuwa duniani, Yesu, ambaye anamjua Yehova vizuri, alitoa mfano ambao unafunua jibu lenye kutia moyo la swali hilo.

Akimfananisha Yehova na mchungaji, Yesu alisema: “Mtu akiwa na kondoo 100 na mmoja apotee, je, hatawaacha wale 99 milimani na kuondoka kwenda kumtafuta yule anayepotea? Naye akimpata, hakika ninawaambia ninyi, yeye humshangilia huyo zaidi kuliko wale 99 ambao hawakupotea. Vivyo hivyo Baba yangu aliye mbinguni hatamani kwamba mmoja wa wadogo hawa aangamie.” (Mathayo 18:12-14) Acha tuone Yesu anavyofafanua vizuri jinsi Yehova anavyomjali na kumpenda kila mmoja wa waabudu Wake.

Mchungaji alihisi ana wajibu kumwelekea kila mmoja wa kondoo zake. Ikiwa kondoo angepotea, mchungaji angejua ni kondoo gani aliyepotea. Alijua kila kondoo kwa jina alilokuwa amempa. (Yohana 10:3) Mchungaji anayejali hangepumzika hadi ampate kondoo aliyepotea na kumrudisha katika kundi. Kwa kwenda kumtafuta kondoo aliyepotea, hawahatarishi wale kondoo wengine 99 anaowaacha. Kwa kawaida, wachungaji walikaa pamoja na kuwaacha kondoo wao wachangamane.a Hivyo, mchungaji aliyeenda kumtafuta kondoo aliyepotea, angewaacha wachungaji wenzake wawachunge wale kondoo wengine. Alipompata yule kondoo aliyepotea akiwa mzima, mchungaji alikuwa na sababu ya kushangilia. Angembeba kiumbe huyo mwenye wasiwasi mabegani mwake na kumrudisha kwenye mazingira salama kundini.—Luka 15:5, 6.

Akitumia mfano huo, Yesu alisema kwamba Mungu hataki “mmoja wa wadogo hawa aangamie.” Mapema, Yesu alikuwa amewaonya wanafunzi wake wasimkwaze ‘mmoja wa wale wadogo wanaomwamini.’ (Mathayo 18:6) Hivyo basi, mfano wa Yesu unatufundisha nini kumhusu Yehova? Yeye ni Mchungaji anayejali sana kila mmoja wa kondoo zake, kutia ndani ‘wale wadogo’—wale ambao huenda ulimwengu ukawaona kuwa hawana thamani. Ndiyo, machoni pa Mungu, kila mmoja wa waabudu wake ni wa pekee na wa thamani.

Ikiwa unataka kuhakikishiwa kwamba una thamani machoni pa Mungu, mbona usijifunze mengi kumhusu Mchungaji Mkuu, Yehova Mungu, na jinsi unavyoweza kumkaribia? Ukifanya hivyo, utakuwa na uhakika kama ule wa mtume Petro, ambaye hapana shaka alimsikia Yesu akitoa ule mfano kuhusu kondoo aliyepotea. Petro aliandika hivi baadaye: ‘Tupeni mahangaiko yenu yote juu ya Mungu, kwa sababu yeye anawajali ninyi.’—1 Petro 5:7.

[Maelezo ya Chini]

a Haikuwa vigumu kuwatenganisha kondoo, kwa sababu kondoo walitambua na kufuata sauti ya mchungaji wao mwenyewe.—Yohana 10:4.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki