Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • te sura 28 kur. 115-118
  • Mchungaji Mwenye Upendo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mchungaji Mwenye Upendo
  • Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
  • Habari Zinazolingana
  • Mahali pa Kupata Faraja
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Yesu Anajali Kondoo Wake
    Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo—2018
  • Yehova Ni Mchungaji Wetu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • “Aliyepotea Nitamtafuta”
    Mrudie Yehova
Pata Habari Zaidi
Kumsikiliza Mwalimu Mkuu
te sura 28 kur. 115-118

Sura ya 28

Mchungaji Mwenye Upendo

JE! UMEPATA kujiona upweke? Unataka kujua ikiwa yeyote akupenda?—

Au umepata kupotea?— Ulionaje?— Inaweza kukuogofya, sivyo?—

Siku moja Mwalimu Mkuu alisimulia hadithi juu ya mmoja aliyepotea. Lakini hakuwa mtoto aliyepotea. Alikuwa kondoo.

Unajua kondoo alivyo, sivyo?— Ni mnyama mdogo ambaye kwake wanadamu wanapata sufu. Katika njia fulani wewe uko kama kondoo. Hilo likoje?

Basi, kondoo si wakubwa au si wenye nguvu sana. Nao wanaogopa wakati wanapopotea. Wanataka upendo na huruma. Tena wanataka mtu fulani awaangalie na kuwalinda, kama wewe unavyohitaji. Mtu ambaye anaangalia kondoo anaitwa mchungaji.

Katika hadithi yake Yesu alisimulia juu ya mchungaji aliyekuwa na kondoo 100. Lakini ndipo mmoja wa kondoo akapotea. Pengine alikuwa akishughulika na kula majani wakati wengine walipoondoka. Au pengine alitaka kuona kulikuwa nini upande mwingine wa kilima. Lakini mbele ya kondoo huyo kujua, akawa mbali na wengine. Waweza kuwazia namna mdogo huyo alivyojiona alipotazama huku na huku akaona alikuwa peke yake?

Wakati mchungaji angeona kondoo mmoja hakuwapo, angefanyaje? Je! angesema lilikuwa shauri la kondoo hivyo asingehangaika naye? Au angewaacha wale 99 mahali pa salama aende kumtafuta yule mmoja? Je! kondoo mmoja angestahili kutaabikiwa sana hivyo?— lkiwa wewe ungekuwa kondoo huyo aliyepotea, ungetaka mchungaji akutafute?—

Mchungaji aliwapenda sana kondoo wake wote, hata yule aliyepotea. Basi alikwenda kumtafuta mmoja aliyepotea.

Fikiri namna kondoo aliyepotea alivyofurahi alipomwona mchungaji wake akija. Naye Yesu alisema kwamba mchungaji alifurahi kwa vile amemwona kondoo wake. Alimfurahia zaidi kuliko wale kondoo 99 ambao hawakupotea.

Sasa, ni nani aliye kama mchungaji huyo katika hadithi ya Yesu? Nani anayetuangalia sana kama mchungaji yule alivyofanya kwa kondoo wake?— Yesu alisema ni Baba yake wa mbinguni. Na Baba yake ni Yehova Mungu.

Yehova ni Mchungaji Mkuu wa watu wake. Yeye awapenda wote wanaomtumikia, hata wadogo kama wewe. Yeye hataki ye yote wa sisi aumizwe au kuharibiwa. Je! si jambo zuri kujua kwamba Mungu anatuangalia sana?— —Mathayo 18:12-14.

Je! kweli unamwamini Yehova Mungu?— Je! wewe unasadiki yeye ni Mtu aliyeko?—

Ni kweli kwamba hatuwezi kumwona Yehova. Hii ni kwa sababu yeye ni Roho. Yeye ana mwili usioonekana kwa macho yetu. Lakini yeye ni Mtu aliyeko, naye aweza kutuona sisi. Anajua tunapotaka msaada. Nasi twaweza kusema na yeye katika sala, kama vile usemavyo na baba na mama yako. Yehova anataka tufanye hivi.

Basi, ikiwa wakati wo wote unajiona mwenye huzuni au mpweke, imekupasa ufanye nini? — Sema kwa Yehova. Mkaribie yeye. Naye atakufariji na kukusaidia. Kumbuka kwamba Yehova akupenda, hata unapojiona kana kwamba uko peke yako.

Sasa, na tuchukue Biblia zetu. Tutasoma pamoja jambo fulani ambalo litachangamsha mioyo yetu. Fungua Zaburi 23, na tutaanzia na mstari wa kwanza.

Hapo panasema hivi: “[Yehova] ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya; kwa maana Wewe upo pamoja nami, gongo lako na fimbo yako vyanifariji.”

Ndivyo watu wanavyojiona ikiwa Mungu wao ni Yehova. Je! ndivyo uonavyo?—

Kama vile mchungaji mwenye upendo anavyoangalia kundi lake, vivyo Yehova anaangalia vizuri watu wake. Anajiona kuburudishwa kwa sababu ya mambo mazuri ambayo anawafanyia. Yeye anawaonyesha kwenda katika njia ya haki, na wanafuata kwa furaha. Hata wanapozungukwa na taabu, hawaogopi. Mchungaji anatumia fimbo yoke kulinda kondoo na wanyama ambao huenda wakawaumiza. Na watu wa Mungu wanajua kwamba yeye atawalinda. Wanajiona salama kwa sababu Mungu yuko pamoja nao.

Kwa kweli Yehova awapenda kondoo wake, naye anawaangalia kwa upole. Biblia inasema: ‘Ataongoza kondoo wake kama mchungaji. Atawakusanya pamoja wanakondoo kwa mikono yake. Wachanga atawasaidia kwa uangalifu.’—lsaya 40:11.

Je! inakufurahisha kujua kwamba Yehova yuko hivyo? Unataka uwe mmoja wa kondoo wake?—

Kondoo wanasikiliza sauti ya mchungaji wao. Wanakaa karibu naye. Wewe unamsikiliza Yehova? Je! unakaa karibu naye? Basi si lazima kabisa uogope. Yehova atakuwa nawe.

(Kwa upendo Yehova anawaangalia wamtumikiao. Someni pamoja ambayo Biblia inasema juu ya hili katika Zaburi 37:25; 55:22; Isaya 41:10; Luka 12:29-31.)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki