Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w08 9/1 uku. 3
  • Je, Unamfahamu Baba Yako wa Mbinguni?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Unamfahamu Baba Yako wa Mbinguni?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Habari Zinazolingana
  • Yehova, Baba Yetu, Anatupenda Sana
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2020
  • Je, Unamwona Yehova Kuwa Baba Yako?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Mungu Ni Nani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu Wote)—2019
  • ‘Mwana Anapenda Kumfunua Baba’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
w08 9/1 uku. 3

Je, Unamfahamu Baba Yako wa Mbinguni?

UNAMFAHAMU baba yako vizuri kadiri gani? Huenda swali hilo likakushangaza ikiwa umelelewa katika familia yenye upendo. Huenda ukajibu hivi: ‘Bila shaka ninamfahamu sana!’ Ndiyo, watu wengi wanajua kile ambacho baba yao anapenda na kile anachochukia, jinsi anavyotenda katika hali fulani, na jinsi anavyoitunza familia.

Hata hivyo, huenda wakati fulani ulishangazwa kuona baba yako akitenda kwa njia ambayo hukutazamia. Kwa mfano, mtoto anaweza kumfahamu baba yake kuwa mnyamavu na mpole, hadi kunapokuwa na hali ya dharura. Ghafula, anamwona baba yake akiilinda familia kwa uthabiti na akiwa imara.

Namna gani Muumba wetu? Tunaambiwa hivi kumhusu: “Kupitia kwake tuna uhai na tunaenda na kuwako.” (Matendo 17:28) Mungu ndiye chanzo cha uhai wetu; kwa hiyo yeye ni Baba ya watu wote. (Isaya 64:8) Labda unahisi hivyo kumhusu Mungu, na hilo ni jambo zuri na linalofaa. Hata hivyo, ili tufaidike na tuwe na furaha, kuna mambo mengi kumhusu ambayo tunaweza kujifunza na kugundua.

Hisia zako kumwelekea baba yako wa kidunia na jinsi unavyomwonyesha heshima zinategemea unamfahamu vizuri kadiri gani. Vivyo hivyo, unapoendelea kumfahamu Mungu vizuri zaidi, uhusiano wako pamoja naye utakuwa wa kibinafsi zaidi. Mungu anaweza kukusaidia kukabiliana na majaribu na vishawishi maishani ikiwa utamfahamu vizuri na kujifunza kufanya mapenzi yake.

Mungu ana utu wa aina gani? Sifa zake zinapaswa kuwa na uvutano gani kuelekea jinsi unavyohisi kumhusu? Je, kumfahamu kunakupa madaraka yoyote? Utapata majibu ya maswali haya katika habari inayofuata.

[Blabu katika ukurasa wa 3]

Hisia zako kuelekea wengine huenda zikategemea kadiri unavyowafahamu

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki