Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w09 3/1 uku. 32
  • Tarehe Muhimu Zaidi Katika Historia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Tarehe Muhimu Zaidi Katika Historia
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
w09 3/1 uku. 32

Tarehe Muhimu Zaidi Katika Historia

Ni tarehe ambayo Yesu Kristo alikufa. Kwa nini kifo cha Yesu kilikuwa muhimu sana? Kwa sababu kadhaa.

Uaminifu wa Yesu hadi kifo ulithibitisha kwamba mwanadamu anaweza kudumisha utimilifu kwa Mungu.

Kifo cha Kristo kiliandaa nafasi kwa wanadamu fulani kutawala pamoja naye mbinguni. Isitoshe, kiliwafungulia wengine wengi njia ya kufurahia uzima wa milele kwenye paradiso duniani.

Jioni kabla ya kifo chake, Yesu alitumia mkate usiotiwa chachu na divai nyekundu kama mifano ya dhabihu yake yenye upendo akiwa mwanadamu. Naye aliwaambia wanafunzi wake: “Endeleeni kufanya hivi kwa kunikumbuka mimi.” (Luka 22:19) Je, wewe utakumbuka tukio hilo muhimu?

Mashahidi wa Yehova wanakualika kwa uchangamfu ujiunge nao katika kuadhimisha Ukumbusho wa kifo cha Yesu. Mwaka huu tarehe ya Ukumbusho huo ni Alhamisi, Aprili 9, baada ya jua kushuka. Unaweza kuhudhuria mwadhimisho huo katika Jumba la Ufalme lililo karibu nawe. Waulize Mashahidi wa Yehova walio karibu nawe saa na mahali hususa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki