Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • wp16 Na. 4 uku. 4
  • Biblia Iliokoka Kuharibika

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Biblia Iliokoka Kuharibika
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
  • Habari Zinazolingana
  • Je! Kweli Sisi Twazihitaji Nakala za Awali?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Ithibati ya Uhifadhi wa Kimungu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Hicho Kitabu Kiliokokaje?
    Kitabu kwa Ajili ya Watu Wote
  • Biblia​—Imedumu kwa Njia ya Pekee
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
wp16 Na. 4 uku. 4

HABARI KUU | JINSI BIBLIA ILIVYOOKOKA

Biblia Iliokoka Kuharibika

TATIZO: Waandishi wa Biblia na wanakili waliandika ujumbe wa Biblia kwenye ngozi na mafunjo.a (2 Timotheo 4:13) Vifaa hivyo vilihatarishaje Biblia?

Mafunjo huchanika, huchuja rangi na kuchakaa haraka. Wachimbuzi wa vitu vya kale huko Misri, Richard Parkinson na Stephen Quirke, walisema: “Karatasi za mafunjo zinaweza kuoza na kuwa udongo. Zinapohifadhiwa kwa kufukiwa ardhini, zinaweza kuharibika kwa sababu ya kuvu au kutu na zinaweza kuliwa na panya au wadudu, hasa mchwa.” Baada ya mafunjo fulani kupatikana, yaliharibika haraka kwa sababu ya unyevu au joto kali.

Ngozi hudumu kuliko mafunjo, hata hivyo, ikiwa ngozi itahifadhiwa kwenye mazingira yenye joto kali, unyevu, mwanga au isipotunzwa vizuri inaweza kuharibika.b Pia ngozi inaweza kuharibiwa na wadudu. Ndiyo sababu nakala nyingi za kale hazijadumu mpaka leo. Ikiwa Biblia ingeharibika, basi ujumbe wake haungekuwepo.

JINSI BIBLIA ILIVYOOKOKA: Sheria ya Wayahudi ilimwagiza kila mfalme ‘kujiandikia katika kitabu nakala ya sheria hii’ yaani, vitabu vitano vya kwanza vya Biblia. (Kumbukumbu la Torati 17:18) Kwa kuongezea, wanakili wenye ustadi walinakili hati nyingi hivi kwamba kufikia karne ya kwanza W.K, Maandiko yangeweza kupatikana katika masinagogi yote nchini Israeli na hata katika maeneo ya mbali ya Makedonia! (Luka 4:16, 17; Matendo 17:11) Baadhi ya hati hizo za kale ziliokoka jinsi gani hadi kufika wakati wetu?

1. Mtungi wa udongo; 2. Sehemu ya kitabu cha kukunjwa ya Bahari ya Chumvi

Hati zinazojulikana kama Vitabu vya Kukunjwa vya Bahari ya Chumvi zilidumu kwa miaka mingi kwenye mitungi ya udongo iliyohifadhiwa katika mapango yaliyo katika maeneo yenye ukame.

ango ambalo baadhi ya hati za kale za Biblia ziligunduliwa

Msomi wa Agano Jipya Philip W. Comfort alisema: “Wayahudi walikuwa na kawaida ya kuhifadhi hati-kunjo za Maandiko kwenye mitungi.” Inaonekana kwamba Wakristo waliendelea na desturi hiyo. Hivyo, baadhi ya hati za kale za Biblia zimepatikana kwenye mitungi ya udongo, mapango yenye giza na katika maeneo yenye ukame sana.

MATOKEO: Maelfu ya sehemu za hati za Biblia zilizo na zaidi ya miaka 2,000 hivi zimedumu kufikia sasa. Hakuna kitabu kingine chochote cha awali kilicho na hati nyingi za kale kama Biblia.

a Mafunjo ni karatasi ambazo hutengenezwa kutokana na mmea unaoota sehemu zenye maji uitwao mfunjo. Ngozi iliandaliwa kutokana na ngozi za wanyama.

b Kwa mfano, nakala rasmi ya U.S. Declaration of Independence iliandikwa katika ngozi. Kufikia sasa hati hiyo ambayo hata haijafikia miaka 250, imechuja rangi hivi kwamba maandishi yake hayawezi kusomeka.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki