Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • wp18 Na. 2 uku. 3
  • Kutabiri Kuhusu Wakati Ujao

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutabiri Kuhusu Wakati Ujao
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2018
  • Habari Zinazolingana
  • Sababu Waweza Kuutumaini Unabii wa Biblia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Unabii Ambao Umetimia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2018
  • Kutafuta Matabiri Yanayotumainika
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Je, Inawezekana Kujua Wakati Ujao?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2018
wp18 Na. 2 uku. 3
Mtabiri wa hali ya hewa anatabiri hali itakavyokuwa katika siku 7 zijazo

Kutabiri Kuhusu Wakati Ujao

Je, umewahi kujiuliza maisha yako na ya familia yako yatakuwaje wakati ujao? Je, unafikiri utapata ufanisi, au utakumbwa na umaskini? Je, utapata watu wanaokupenda, au utakuwa mpweke? Je, utaishi muda mrefu, au maisha yako yatakatika ghafla? Wanadamu wamejiuliza maswali hayo kwa maelfu ya miaka.

Leo, wataalamu huchunguza jinsi hali zinavyoendelea duniani na kutumia habari hizo kutabiri mambo yatakavyokuwa. Ingawa baadhi ya mambo wanayotabiri hutokea, mengine huwa kinyume kabisa na matarajio yao. Kwa mfano, katika mwaka wa 1912, Guglielmo Marconi, mvumbuzi wa teknolojia ya kurusha mawimbi hewani bila kutumia nyaya alitabiri hivi: “Enzi mpya inayokuja ya kurusha mawimbi bila kutumia nyaya, itakomesha vita.” Na ajenti wa kampuni fulani ya kurekodi (Decca Record Company), ambaye aliwagomea wanamuziki wa kikundi cha the Beatles katika mwaka wa 1962, aliamini kwamba vikundi vya kucheza gitaa vilikuwa vinaelekea mwisho wake.

Watu wengi hugeukia wale wanaowasiliana na roho ili kutafuta habari kuhusu wakati ujao. Baadhi yao hutafuta ushauri kutoka kwa wanajimu, na makala za utabiri wa nyota zinapatikana kwa ukawaida kwenye magazeti mengi. Wengine nao hutafuta habari kwa wabashiri wanaodai kwamba wanaweza “kujua” wakati ujao wa mtu kwa kusoma kadi za kubashiri, namba, au alama za viganja vya mikono.

Wakiwa na hamu ya kujua mambo yangekuwaje baadaye, baadhi ya watu walioishi nyakati za kale walienda kwa waaguzi, wa kiume au wa kike, ambao waliwapatia habari kutoka kwa miungu waliyodai kuiwakilisha. Kwa mfano, inasemekana kwamba Mfalme Croesus wa Lydia alituma zawadi zenye thamani kubwa kwa mwaguzi aliyeishi Delphi, Ugiriki, na kumwomba amweleze matokeo yangekuwaje ikiwa atapigana na Koreshi wa Uajemi. Mwaguzi huyo alisema kwamba Croesus akienda kupigana na Koreshi, “milki kubwa” itaangushwa. Croesus alienda vitani akiwa na uhakika kwamba angeshinda vita hiyo, lakini kwa kusikitisha milki yake kubwa ndiyo iliyoanguka!

Utabiri huo haukuwa na maana yoyote kwa sababu ungeonekana kuwa wa kweli bila kujali ni nani ambaye angeshinda vita hiyo. Croesus alipoteza kila kitu kwa sababu ya kutegemea habari za uwongo. Je, wale wanaotumia njia za kisasa ili kujua kuhusu wakati wao ujao, wamepata mafanikio yoyote?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki