Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 8/88 uku. 3
  • Matangazo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Matangazo
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1988
Huduma Yetu ya Ufalme—1988
km 8/88 uku. 3

Matangazo

● Toleo la fasihi kwa Agosti na Septemba: Kimoja cha broshua zifuatazo zenye kurasa 32 ukubwa wa gazeti: Furahia Maisha Milele Duniani! Jina la Mungu Litakaloendelea Milele, Serikali Itakayoleta Paradiso, Mashahidi wa Yehova Katika Karne ya Ishirini. Oktoba: Andikisho la mwaka mmoja la ama Amkeni! ama Mnara wa mlinzi ama yote mawili. Novemba: New World Translation pamoja na kitabu “Ufalme Wako Uje.”

● Kila kundi litapokea fomu tatu za Hesabu ya Vitabu na linapaswa kuhesabu halisi vitabu vya kampeni. Tafadhalini jazeni fomu kikamili na kutupelekea nakala ya kwanza si baada ya Septemba 6, 1988. Wekeni nakala ya kaboni katika faili zenu. Tunawapelekeeni nakala ya tatu ili muitumie kama karatasi ya kufanyia kazi.

● Makundi yanapaswa kuanza kuagiza Kalenda ya Mashahidi wa Yehova ya 1989 pamoja na agizo lao la vitabu la Septemba. Kalenda zitapatikana katika Kiingereza na Kifaransa. Kalenda ni bidhaa za kuagizwa kwa kiasi nazo zitatozwa bei kwa hesabu ya vitabu kwa bei ya wahubiri. Mapainia, na watu wote wanaipokea kwa bei moja kama wahubiri. Msipeleke malipo pamoja na maagizo.

● Kikumbusho: Kila baraza la wazee tafadhali hakikisheni kwamba makala zote za funzo la Mnara wa Mlinzi za mwaka uliopita zinazungumzwa kundini; habari yoyote isikose kuzungumzwa kwa sababu ya kuwasili kwa magazeti bila mpango. Hasa makala zinazohusu Uzazi katika Mnara wa Mlinzi wa Machi 1, 1988 zinapasa kudarisiwa na kundi ikiwa hazikudarisiwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki