Matangazo
● Machi: Revelation—Its Grand Climax at Hand! au “Ufalme wako uje” katika Kiswahili. Aprili na Mei: Uandikishaji wa Mnara wa Mlinzi kwa mwaka mmoja. Uandikishaji wa Amkeni! unaweza kutolewa kwa msingi ule ule. Maandikisho ya miezi sita na mwaka mmoja ya chapa za kila mwezi ni nusu ya bei ya mwaka mmoja. Juni: Amani ya Kweli na Usalama wa Kweli—Unawezaje Kuupata? au “Ufalme wako uje” katika Kiswahili.
● Mwangalizi msimamizi au mmoja aliyechaguliwa naye apasa kukagua hesabu ya kundi Machi 1 au upesi baada ya hapo.
● Kwa kujitayarishia mwadhimisho wa Ukumbusho, wote watataka kufuata ratiba ya usomaji wa Biblia iliyoandaliwa kwenye kalenda ya 1989, kuanzia Ijumaa, Machi 17.
● Michango ambayo makundi yanapelekea Sosaiti kwa kusongeza mbele kazi ya Ufalme na pia michango ya kipekee kwa makusudi mengine yanayotajwa, hushukuriwa kwenye stetimenti ya Sosaiti ya kila mwezi kwa makundi. Shukrani hizo hutia ndani maelezo mafupi ya uthamini. Mwangalizi msimamizi anapasa kuangalia shukrani hizo na kundi lijulishwe kila mwezi ripoti ya hesabu inapotolewa. Sosaiti inataka akina ndugu wajue kwamba michango yao imepokewa na kwamba inathaminiwa.
● Sasa Sosaiti inakubali maagizo ya mabuku yaliyojalidiwa ya Mnara wa Mlinzi ambayo yamechapwa upya katika Kiingereza kwa miaka 1970 hadi 1974. Makundi na watu mmoja mmoja wanaopenda kuwa na mabuku haya kwa maktaba yao wanapasa kuamua jumla ya hesabu ya mabuku wanayohitaji kwa kila mwaka na kupeleka maombi yao kupitia kundi. Jumla ya mabuku yapasa kuingizwa kwenye fomu ya Kuagiza Vitabu (S-14) na KUPELEKWA WAKATI WA MWEZI WA MACHI 1989. Uchapaji wa tatu wa mfululizo wa mabuku yaliyojalidiwa ya Mnara wa Mlinzi katika Kiingereza ya miaka mitano utaanza karibuni. Tafadhali msipeleke maagizo kwa miaka mingine isipokuwa 1970 hadi 1974 mpaka mwelekezo wa baadaye utakapotokea kwenye Huduma ya Ufalme Yetu. Kwa kuwa Sosaiti haitaweka akibani mabuku haya yaliyochapishwa upya, tunawasihi wote wafikirie jambo hili kwa uangalifu na kutoa maagizo ya mabuku ya 1970 hadi 1974 yanayohitajiwa. Maagizo ya baadaye yatajazwa tu kulingana na akiba zilizopo. Mabuku haya yanayochapwa upya ni vifaa vya kuagizwa kwa kiasi nayo yatalipiwa mara yanapopokewa.
● Painia yeyote wa kawaida ambaye angependezwa kutumikia akiwa painia wa pekee wa muda katika eneo lisilogawiwa mtu wakati wa kampeni ya Julai-Septemba lazima aombe kwa kuandikia Afisi ya Tawi barua si baada ya Aprili 1989. Tungethamini kupata maelezo mafupi kutoka kwa mwangalizi msimamizi kuhusu kupatikana na uwezekano wa painia huyo mwishoni mwa barua.
Ratiba iliyodokezwa ya Usomaji wa Biblia kwa juma la Ukumbusho:
Ijumaa, Machi 17
Jumamosi, Machi 18
18, 19
Jumapili, Machi 19
Jumatatu, Machi 20
Jumanne, Machi 21
Jumatano, Machi 22