Ratiba ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi ya 1990
MAAGIZO
Wakati wa 1989, ufuatao utakuwa ndio mpango wa kuongozea Shule ya Huduma ya Kitheokrasi.
VITABU VYA MAFUNDISHO: Biblia, “All Scripture Is Inspired of God and Beneficial” [si], Vichwa vya Mazungumzo ya Biblia [tdSW], na Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani [peSW] vitakuwa ndio msingi wa migawo.
Shule itaanza kwa wimbo, sala, na maneno ya kukaribisha, kisha itaendelea hivi:
MGAWO NA. 1: Dakika 15. Huu wapasa uongozwe na mzee au mtumishi wa huduma mwenye kustahili. Mgawo huu utategemea “All Scripture Is Inspired of God and Beneficial.” Mgawo huu umepasa utolewe kuwa hotuba ya maagizo ya dakika 10 kufika 12 pamoja na pitio la mdomo kwa dakika 3 kufika 5, kwa kutumia maswali ya sehemu hiyo yaliyochapwa. Lengo la hotuba hii si kusimulia tu habari hiyo, bali ni kuvuta fikira juu ya faida inayoweza kutumika ya habari hiyo inayozungumzwa, kukazia yatakayokuwa yenye msaada zaidi kwa kundi. Mahali inapohitajiwa, kichwa kimepasa kichaguliwe. Wote wanatiwa moyo kutangulia kujitayarisha kwa uangalifu ili wanufaike kikamilifu na habari hiyo.
Akina ndugu wenye kupewa mgawo wa hotuba hii wamepaswa wafuate wakati wao kwa uangalifu. Shauri la faragha limepasa kutolewa iwapo lazima.
MAMBO MAKUU KUTOKANA NA KUSOMA BIBLIA: Dakika 6. Mgawo huu umepasa uongozwe na mwangalizi wa shule au mzee mwingine mwenye kustahili au mtumishi wa huduma aliyegawiwa na mwangalizi wa shule. Huku kusiwe kusimulia tu sehemu zilizogawiwa kusomwa. Baada ya kutoa utangulizi mfupi wa mambo yaliyomo katika sura zilizogawiwa, wasaidie wasikilizaji wafahamu kwa nini na jinsi gani habari hiyo ni yenye faida kwetu. Chunguza matoleo ya Mnara wa Mlinzi upate habari zaidi za kukaziwa. Ndipo wanafunzi wataruhusiwa na mwangalizi wa shule waende kwenye madarasa yao mbalimbali.
HOTUBA NA. 2: Dakika 5. Huku ni kusoma Biblia juu ya habari iliyogawiwa itakayotolewa na ndugu. Hii itakuwa hivyo katika shule kubwa na pia vikundi vidogo vya shule. Kwa kawaida migawo ya kusoma ni mifupi kutosha kuruhusu mwanafunzi atoe habari yenye maelezo katika utangulizi na maelezo yake ya kumalizia, na hata katika mambo makuu ya katikati. Mandhari ya nyuma ya kihistoria, maana ya kiunabii au ya kimafundisho na jinsi kanuni zinavyohusu, yanaweza kutiwa ndani. Mistari yote iliyogawiwa yapasa isomwe kabisa.
HOTUBA NA. 3: Dakika 5. Hotuba hii watagawiwa akina dada. Habari za hotuba hii zitatolewa kwa matumizi ya zamu kwa zamu ya vitabu viwili, Vichwa vya Mazungumzo na Kuishi Milele, na habari za kutoka kitabu hicho cha pili watagawiwa hasa wanafunzi wachanga au wapya. Mwanafunzi aliyegawiwa amepaswa awe anaweza kusoma. Wakati wa kutoa hotuba hizo, mwanafunzi anaweza kuwa ama ameketi katika kiti ama amesimama. Msaidizi mmoja atapangwa na mwangalizi wa shule, lakini wasaidizi zaidi wanaweza kutumiwa. Ni afadhali vikao vitie ndani utumishi wa shambani au kutoa ushuhuda wa vivi hivi. Anayetoa hotuba anaweza yeye mwenyewe kuanzisha mazungumzo ili kuweka kikao ama aache msaidizi au wasaidizi wake wafanye hivyo. Jambo la kufikiriwa kwanza ni habari inayotolewa, si kikao. Mwanafunzi amepaswa atumie kichwa kilichoonyeshwa.
HOTUBA NA. 4: Dakika 5. Igawiwe ndugu au dada. Hotuba hii itategemea Vichwa vya Mazungumzo. Anapogawiwa ndugu, apaswa ahutubie wasikilizaji wote. Ili hotuba yake iwe yenye kuelimisha na yenye kunufaisha kweli kweli wale wanaoisikia, kwa kawaida itakuwa bora ndugu atayarishe kwa kufikiria wasikilizaji katika Jumba la Ufalme. Lakini, ikiwa habari inahusu sana hali nyingine au kikao kingine chenye kufaa, ndugu anaweza kuchagua kukuza hotuba yake kulingana na kikao cha hali hiyo. Mwanafunzi amepaswa atumie kichwa kilichoonyeshwa.
Dada anapogawiwa hotuba hii, apaswa kuitoa kama Hotuba Na. 3 inavyoelezwa itolewe.
SHAURI NA MAELEZO: Baada ya kila hotuba ya mwanafunzi, mwangalizi wa shule atatoa shauri linalohusu, si lazima afuate mpango wa shauri lenye kuendelea kama ilivyoandikwa katika kikaratasi cha Shauri la Usemi. Badala ya kufanya hivyo, anapaswa kukaza fikira juu ya sehemu zile ambazo mwanafunzi anahitaji kufanyia maendeleo. Kama mhutubu-mwanafunzi anastahili kuandikiwa “V” tu na hakuna sifa nyingine ya usemi iliyotiwa alama “M” au “T,” basi mshauri amepaswa atie duara kuzunguka sifa ya usemi ambayo mwanafunzi atatengeneza safari nyingine, afanye hivyo katika kisanduku ambamo kwa kawaida alama hizi “V” “M” au “T” zingewekwa. Atamwarifu mwanafunzi jambo hili jioni hiyo na pia aonyeshe sifa hiyo ya usemi penye kikaratasi cha Mgawo wa Shule ya Huduma ya Kitheokrasi (S-89) kitakachofuata cha mwanafunzi huyo. Wale wanaotoa hotuba wamepaswa wakalie viti vya mbele karibu na jukwaa. Hiyo itaokoa wakati, na pia itamwezesha mwangalizi wa shule ampe kila mwanafunzi shauri lake moja kwa moja. Wakati unaporuhusu baada ya kutolewa kwa shauri la mdomo linalohitajiwa, maelezo yaweza kutolewa na mshauri juu ya mambo yenye kuelimisha na yanayofaa kutumiwa ambayo wanafunzi hawakuyazungumza. Imempasa mwangalizi wa shule aangalie asije akatumia zaidi ya jumla ya dakika mbili akitoa shauri na maelezo baada ya kila hotuba ya mwanafunzi. Ikiwa ule utoaji wa mambo makuu ya Biblia uliacha nje jambo fulani la maana, shauri la faragha laweza kutolewa.
KUTAYARISHA HOTUBA: Ndugu wenye kugawiwa hotuba Na. 1 wamepaswa wachague kichwa inapohitajiwa. Wanafunzi wenye kugawiwa hotuba ya pili wachague kichwa kitakachoruhusu mazungumzo ya sehemu kubwa zaidi ya mambo yaliyo katika habari. Wanafunzi wenye kugawiwa hotuba ya tatu na ya nne wamepaswa watumie kichwa kilichoonyeshwa. Kabla ya kutoa hotuba, wanafunzi watataka warudie kusoma habari ya Kiongozi cha Shule iliyo na sifa ya usemi inayoendelea kutengenezwa.
KUFUATA WAKATI: Kusiwe hotuba ya kuzidi wakati uliopewa. Wala shauri na maelezo ya mshauri yasizidi wakati. Hotuba Na. 2 mpaka 4 zimepasa zikatizwe kwa busara ikiwa wakati unakwisha. Aliyepewa mgawo wa kutoa “ishara ya kuacha” amepaswa kufanya hivyo mara hiyo. Ndugu wanaoshughulika na Mgawo 1 wanapozidi wakati wao wamepaswa washauriwe kwa faragha. Wote wamepaswa wafuate wakati wao kwa uangalifu. Jumla ya dakika za programu yote ya shule ni: Dakika 45 bila kuhesabu dakika za wimbo na sala.
PITIO LA KUANDIKA: Pindi kwa pindi pitio la kuandika linatolewa. Katika kujitayarisha, pitia migawo ya habari na kumaliza ratiba ya kusoma Biblia. Biblia pekee ndiyo inayoruhusiwa kutumiwa wakati wa pitio hili la dakika 25. Wakati unaobaki utatumiwa kwa mazungumzo ya maswali na majibu. Kila mwanafunzi atasahihisha karatasi yake mwenyewe. Mwangalizi wa shule atasoma majibu yote na kukaza fikira juu ya maswali ambayo ni magumu zaidi, akiwasaidia wote wayafahamu majibu vizuri. Ikiwa, kwa sababu fulani, hali za kwenu zinalazimisha pitio la kuandikwa lisifanywe juma lililopangwa laweza kufanywa juma moja baada ya lile linaloonyeshwa katika ratiba.
MAKUNDI MAKUBWA NA MADOGO: Labda makundi yenye wanafunzi 50 au zaidi walioandikwa yatapenda kufanya mpango ili vikundi vya ziada vya wanafunzi vitoe mbele ya washauri wengine hotuba zilizoratibiwa. Bila shaka, watu wasio wakfu wanaoishi kupatana na kanuni za Kikristo wanaweza pia kujiandikisha katika shule hii na kupokea migawo.
WANAFUNZI WASIOKUWAPO: Wote katika kundi wanaweza kuonyesha uthamini kwa shule hii kwa kuhudhuria kila kipindi cha kila juma, kwa kutayarisha vizuri migawo yao, na kwa kushiriki vipindi vya maswali. Inatumainiwa kwamba wanafunzi wote watatimiza migawo yao kwa dhamiri. Mwanafunzi asipokuwapo wakati amepangwa kwenye ratiba, mtu mwingine anaweza kujitolea kuchukua mgawo huo, akionyesha matumizi yoyote ya habari kwa kadiri awezavyo katika huo muda mfupi wa kuarifiwa. Au, mwangalizi wa shule anaweza kuzungumza habari hiyo kwa ushirika unaofaa wa wasikilizaji.
RATIBA
Jan. 1 Kusoma Biblia: Luka 2 na 3
Na. 1: Utangulizi kwa Wagalatia (si kur. 216-17 maf. 1-6)
Na. 2: Luka 3:7-22
Na. 3: Yesu Aliweka Kielelezo Katika Kuheshimu Jina la Mungu (peSW sura 22 maf. 1-4)
Na. 4: Kusudi na Ubora wa Ufalme wa Mungu (tdSW 42A)
Jan. 8 Kusoma Biblia: Luka 4 na 5
Na. 1: Wagalatia 1:1 hadi 3:29 (si kur. 217 maf. 7-10)
Na. 2: Luka 4:16-30
Na. 3: Mambo Ambayo Ufalme wa Mungu Utafanyia Aina ya Wanadamu (tdSW 42B)
Na. 4: Maana ya “Mwisho wa Ulimwengu” (tdSW 40A)
Jan. 15 Kusoma Biblia: Luka 6 na 7
Na. 1: Wagalatia 4:1 hadi 6:18 (si kur. 217-18 maf. 11-13)
Na. 2: Luka 6:20-38
Na. 3: Kwa Nini Tumelichukua Jina Mashahidi wa Yehova (peSW sura 22 maf. 5, 6)
Na. 4: Inatupasa Tuwe Macho Kuona Ishara za “Siku za Mwisho” (tdSW 40B)
Jan. 22 Kusoma Biblia: Luka 8 na 9
Na. 1: Utangulizi kwa Waefeso (si kur. 219-20 maf. 1-8)
Na. 2: Luka 9:1-17
Na. 3: Maadui Wangali Watendaji Wakati Ufalme Unapoanza Kufanya Kazi (tdSW 42C)
Na. 4: Matukio Yenye Kuonekana Yanaonyesha Siku za Mwisho Zilianza Katika 1914 (tdSW 40C)
Jan. 29 Kusoma Biblia: Luka 10 na 11
Na. 1: Waefeso 1:1 hadi 3:21 (si uku. 220 maf. 9-11)
Na. 2: Luka 11:1-20
Na. 3: Ni Nani Pekee Ambao Wanahubiri Ufalme Wa Mungu Leo? (peSW sura 22 maf. 7-9)
Na. 4: Kristo Hakupewa Mamlaka Kamili Awe Mfalme Wakati wa Pentekoste (tdSW 42D)
Feb. 5 Kusoma Biblia: Luka 12 na 13
Na. 1: Waefeso 4:1 hadi 6:24 (si kur. 220-1 maf. 12-15)
Na. 2: Luka 12:32-48
Na. 3: Ufalme wa Mungu Haumo ‘Mioyoni mwa Watu’ (tdSW 42E)
Na. 4: Tarehe Zinaonyesha Kwamba Siku za Mwisho Zilianza Katika 1914 (tdSW 40D)
Feb. 12 Kusoma Biblia: Luka 14 hadi 16
Na. 1: Utangulizi kwa Wafilipi (si kur. 222-3 maf. 1-7)
Na. 2: Luka 14:16-35
Na. 3: Dini ya Kweli Inaheshimu Neno la Mungu (peSW sura 22 maf. 10-13)
Na. 4: Kusudi la Agano la Torati (tdSW 38A)
Feb. 19 Kusoma Biblia: Luka 17 na 18
Na. 1: Wafilipi 1:1 hadi 2:30 (si uku. 223 maf. 8, 9)
Na. 2: Luka 17:5-21
Na. 3: Amri Kumi Ziliondolewa Mbali Pamoja na Sehemu Nyingine Yote ya Agano la Torati (tdSW 38B)
Na. 4: Uhai ni Zawadi ya Mungu kwa Utumishi wa Uaminifu (tdSW 51A)
Feb. 26 Kusoma Biblia: Luka 19 na 20
Na. 1: Wafilipi 3:1 hadi 4:23 (si uku. 223 maf. 10, 11)
Na. 2: Luka 20:21-40
Na. 3: Dini ya Kweli Inajitenga na Ulimwengu (peSW sura 22 maf. 14, 15)
Na. 4: Wanadamu Watiifu Wanahakikishiwa Uhai wa Milele (tdSW 51B)
Mac. 5 Kusoma Biblia: Luka 21 na 22
Na. 1: Utangulizi kwa Wakolosai (si kur. 224-5 maf. 1-5)
Na. 2: Luka 22:7-23
Na. 3: Ili Kupata Uhai, Haitoshi Kutii Amri Kumi Tu (tdSW 38C)
Na. 4: Mungu Ameahidi Kuwapa Watu Uhai wa Mbinguni na wa Duniani Pia (tdSW 51C)
Mac. 12 Kusoma Biblia: Luka 23 na 24
Na. 1: Wakolosai 1:1 hadi 2:7 (si uku. 225 maf. 6-8)
Na. 2: Luka 24:36-53
Na. 3: Upendo Miongoni Mwao Wenyewe Unatambulisha Wale Walio na Dini ya Kweli (peSW sura 22 maf. 16-18)
Na. 4: Uhai wa Kimbingu ni wa Washiriki wa Mwili wa Kristo Peke Yao (tdSW 51D)
Mac. 19 Kusoma Biblia: Yohana 1 hadi 3
Na. 1: Wakolosai 2:8 hadi 4:18 (si kur. 225-6 maf. 9-11)
Na. 2: Yohana 1:1-18
Na. 3: Amri Kumi ni Zenye Uadilifu Lakini Si Lazima Wakristo Wazishike (tdSW 38D)
Na. 4: Watu Wasio na Hesabu Wameahidiwa Uhai wa Milele (tdSW 51E)
Mac. 26 Kusoma Biblia: Yohana 4 na 5
Na. 1: Utangulizi kwa 1 Wathesalonike (si uku. 227 maf. 1-5)
Na. 2: Yohana 4:16-38
Na. 3: Kwa Nini Kunaweza Kuwa na Dini Moja Tu ya Kweli (peSW sura 22 maf. 19, 20)
Na. 4: Mashahidi wa Yehova Hawafaidiki kwa Kugawanya Fasihi ya Biblia (tdE 37A)
Apr. 2 Kusoma Biblia: Yohana 6 na 7
Na. 1: 1 Wathesalonike 1:1 hadi 3:13 (si uku. 228 maf. 6-8)
Na. 2: Yohana 6:52-71
Na. 3: Kusoma Fasihi ya Biblia Hakuvurugi Akili (tdE 37B)
Na. 4: Ndoa ni Mpango Mtakatifu Ulianzwa na Mungu (tdSW 32A)
Apr. 9 Kusoma Biblia: Yohana 8 na 9
Na. 1: 1 Wathesalonike 4:1 hadi 5:28 (si kur. 228-9 maf. 9-12)
Na. 2: Yohana 8:31-47
Na. 3: Sababu kwa Nini Tunajua Mungu Ana Tengenezo Lionekanalo (peSW sura 23 maf. 1-3)
Na. 4: Huenda Fasihi ya Kanisa Isiweze Kutimiza Uhitaji wa Funzo la Jamaa (tdE 37C)
Apr. 16 Kusoma Biblia: Yohana 10 na 11
Na. 1: Utangulizi kwa 2 Wathesalonike (si uku. 230 maf. 1-4)
Na. 2: Yohana 10:1-18
Na. 3: Si Fasihi Zote Humpa Mtu Vifaa vya Kukabiliana na Hatari Inayokuja (tdE 37D)
Na. 4: Lazima Muungano wa Ndoa Uheshimike (tdSW 32B)
Apr. 23 Kusoma Biblia: Yohana 12 na 13
Na. 1: 2 Wathesalonike 1:1 hadi 3:18 (si kur. 230-1 maf. 5-9)
Na. 2: Yohana 13:21-35
Na. 3: Ni Nini Kinachoonyesha Kwamba Mungu Aliwaongoza Watumishi Wake Katika Njia Iliyopangwa Kitengenezo? (peSW sura 23 maf. 4-6)
Na. 4: Kukataza Kusoma Fasihi Yenye Kufariji ni jambo Lisilo la Akili (tdE 37E)
Apr. 30 Pitio la Kuandika. Maliza Luka 2 hadi Yohana 13
Mei 7 Kusoma Biblia: Yohana 14 na 16
Na. 1: Utangulizi kwa 1 Timotheo (si kur. 232 maf. 1-6)
Na. 2: Yohana 15:1-19
Na. 3: Kuamua Kitu cha Kusoma ni Daraka la Kila Mmoja (tdE 37F)
Na. 4: Lazima Wakristo Waheshimu Kanuni ya Ukichwa (tdSW 32C)
Mei 14 Kusoma Biblia: Yohana 17 na 18
Na. 1: 1 Timotheo 1:1 hadi 3:16 (si uku. 233 maf. 7-10)
Na. 2: Yohana 17:1-19
Na. 3: Mungu Anatumia Tengenezo Moja Tu kwa Wakati Mmoja (peSW sura 23 maf. 7-9)
Na. 4: Daraka la Wazazi Wakristo kwa Watoto (tdSW 32D)
Mei 21 Kusoma Biblia: Yohana 19 hadi 21
Na. 1: 1 Timotheo 4:1 hadi 6:21 (si kur. 233-4 maf. 11-14)
Na. 2: Yohana 21:9-23
Na. 3: Fasihi Nyingi Imetangazwa kwa Chapa; Kuwa Mwenye Kuchagua ni Jambo Lenye Mafaa (tdE 37G)
Na. 4: Inawapasa Wakristo Waoe au Waolewe na Wakristo Tu (tdSW 32E)
Mei 28 Kusoma Biblia: Matendo 1 hadi 3
Na. 1: Utangulizi kwa 2 Timotheo (si uku. 235 maf. 1-4)
Na. 2: Matendo 2:22-36
Na. 3: Wakristo wa Karne ya Kwanza Walikuwa Wamepangwa Kitengenezo (peSW sura 23 maf. 10-12)
Na. 4: Maandiko Yanakataza Kuoa Wake Zaidi ya Mmoja (tdSW 38F)
Juni 4 Kusoma Biblia: Matendo 4 hadi 6
Na. 1: 2 Timotheo 1:1 hadi 2:26 (si uku. 236 maf. 5, 6)
Na. 2: Matendo 5:17-32
Na. 3: Ili Kufanya Maendeleo, Lazima Mmoja Asome Misaada ya Kujifunzia Biblia Ambayo Anayo (tdE 37H)
Na. 4: Mke wa Kaini Alikuwa Dada Yake (tdSW 32G)
Juni 11 Kusoma Biblia: Matendo 7 na 8
Na. 1: 2 Timotheo 3:1 hadi 4:22 (si uku. 236 maf. 7-9)
Na. 2: Matendo 8:25-40
Na. 3: Baraza Linaloongoza Linaelekeza Kazi Ya Kutoa Ushuhuda Leo (peSW sura 23 maf. 13-16)
Na. 4: Mariamu, Mama ya Yesu, Si Mama ya Mungu (tdE 39A)
Juni 18 Kusoma Biblia: Matendo 9 na 10
Na. 1: Utangulizi kwa Tito (si kur. 237-8 maf. 1-4)
Na. 2: Matendo 10:30-48
Na. 3: Pesa Hazihitajiwi Ili Kupata Ukweli (tdE 37I)
Na. 4: Mariamu, Bikira, Akawa Mama ya Yesu (tdE 39B)
Juni 25 Kusoma Biblia: Matendo 11 hadi 13
Na. 1: Tito 1:1 hadi 3:15 (si uku. 238 maf. 5-7)
Na. 2: Matendo 12:1-17
Na. 3: Jinsi Kazi ya Kufundisha Inavyoendeshwa Leo (peSW sura 23 maf. 17-21)
Na. 4: Mariamu, Hakuwa “Bikira Milele” (tdE 39C)
Jul. 2 Kusoma Biblia: Matendo 14 na 16
Na. 1: Filemoni: Utangulizi na Yaliyomo (si kur. 239-40 maf. 1-6)
Na. 2: Matendo 15:13-29
Na. 3: Sala Zinazoelekezwa kwa Mungu Lazima Zipitie kwa Kristo (tdE 39D)
Na. 4: Wakristo Wanaadhimisha Mlo wa Bwana wa Jioni (tdE 40A)
Jul. 9 Kusoma Biblia: Matendo 17 hadi 19
Na. 1: Waebrania: Iliandikwa na Paulo na Imevuviwa (si uku. 241 maf. 1-5)
Na. 2: Matendo 17:22-34
Na. 3: Makusudi Yanayotimizwa na Mikutano Yetu Mbalimbali (peSW sura 23 maf. 24-28)
Na. 4: Misa ya Kikatoliki Haipatani na Maandiko (tdE 40B)
Jul. 16 Kusoma Biblia: Matendo 20 na 21
Na. 1: Waebrania: Kiliandikwa Wakati Gani na kwa Nini (si kur. 241-2 maf. 6-9)
Na. 2: Matendo 20:17-35
Na. 3: Uandalizi wa Ufalme wa Mungu Unafaidi Wanadamu Wote (tdSW 53A)
Na. 4: Sababu ya Wakristo Kupingwa (tdSW 47A)
Jul. 23 Kusoma Biblia: Matendo 22 hadi 24
Na. 1: Waebrania 1:1 hadi 4:16 (si uku. 242 maf. 10-12)
Na. 2: Matendo 24:9-23
Na. 3: Kwa Nini Tunaadhimisha Mlo wa Bwana wa Jioni na Wakati Gani (peSW sura 23 maf. 29, 30)
Na. 4: Wasio Wakristo Wana Fursa ya Kuokolewa Sawasawa na Wakristo (tdE 53B)
Jul. 30 Kusoma Biblia: Matendo 25 na 26
Na. 1: Waebrania 5:1 hadi 7:28 (si uku. 243 maf. 13-16)
Na. 2: Matendo 26:8-23
Na. 3: Mababa Wayahudi Waliutumainia Ufalme (tdSW 53C)
Na. 4: Wakristo Hawapaswi Kuogopa Mnyanyaso (tdSW 47B)
Ago. 6 Kusoma Biblia: Matendo 27 na 28
Na. 1: Waebrania 8:1 hadi 10:39 (si kur. 243-4 maf. 17-19)
Na. 2: Matendo 28:17-31
Na. 3: Kuwa kwa Yehova na Tengenezo Lionekanalo Kunatutaka Tufanye Nini? (peSW sura 23 maf. 31, 32)
Na. 4: Magonjwa ya Kipuku na Ukosefu wa Kutii Sheria, Alama za Siku za Mwisho (rsSW uku. 299 hadi uku. 300 fu. 1)
Ago. 13 Kusoma Biblia: Warumi 1 hadi 3
Na. 1: Waebrania 11:1 hadi 13:25 (si uku. 244 maf. 20-22)
Na. 2: Warumi 1:8-23
Na. 3: Alama za Siku za Mwisho: Kazi ya Kuhubiri na Mnyanyaso wa Wakristo wa Kweli (rsSW uku. 301 maf. 1, 2)
Na. 4: Siku za Mwisho Zinaelekeza Kwenye Nini, na Wanahistoria Wana Maoni Gani Juu ya Siku za Mwisho? (rsSW uku. 302 maf. 1, 3, 4)
Ago. 20 Kusoma Biblia: Warumi 4 hadi 6
Na. 1: Yakobo: Kiliandikwa na Nani? (si uku. 246 maf. 1-4)
Na. 2: Warumi 6:8-23
Na. 3: Sheria ya Musa Ilitolewa kwa Nani, na kwa Nini? (peSW sura 24 maf. 1-4)
Na. 4: Baadhi Wataokoka Mwisho wa Ulimwengu (rsSW uku. 303 maf. 1-4)
Ago. 27 Pitio la Kuandika. Maliza Yohana 14 hadi Warumi 6
Sept. 3 Kusoma Biblia: Warumi 7 hadi 9
Na. 1: Yakobo: Uasilia wa Kutungwa, kwa Nini Kiliandikwa (si kur. 246-7 maf. 5-7)
Na. 2: Warumi 8:26-39
Na. 3: Kwa Nini Mungu Ameruhusu Uovu kwa Muda Mrefu Sana (rsSW uku. 303 fu. 5 hadi uku. 304 maf. 1, 2)
Na. 4: Kujibu Vipingamizi vya Hizi Kuwa Siku za Mwisho (rsSW uku. 304 fu. 4 hadi uku. 305 fu. 1)
Sept. 10 Kusoma Biblia: Warumi 10 hadi 12
Na. 1: Yakobo 1:1 hadi 2:26 (si uku. 247 maf. 8-10)
Na. 2: Warumi 12:1-16
Na. 3: Kwa Kuwa Kristo Alikomesha Sheria ni Nini Kinafuata (peSW sura 24 maf. 5-9)
Na. 4: Jinsi Kusudi la Mungu Linavyoweza Kutimizwa (rsSW uku. 341 fu. 4; uku. 342 maf. 3, 4)
Sept. 17 Kusoma Biblia: Warumi 13 hadi 16
Na. 1: Yakobo 3:1 hadi 5:20 (si kur. 247-8 maf. 11-14)
Na. 2: Warumi 15:1-16
Na. 3: Hatukuwa Tuishi Miaka Michache Tu na Kufa (rsSW uku. 343 maf. 1-3)
Na. 4: Je! Maisha Yetu Yalikuwa Yawe Taabu Tu? (rsSW uku. 343 fu. 5 hadi uku. 344 fu. 2)
Sept. 24 Kusoma Biblia: 1 Wakorintho 1 hadi 3
Na. 1: Utangulizi kwa 1 Petro (si uku. 249 maf. 1-5)
Na. 2: 1 Wakorintho 3:1-15
Na. 3: Ni Sheria Gani Zinazowahusu Wakristo? (peSW sura 24 maf. 10, 11)
Na. 4: Kuna Msingi Gani wa Kuwa na Tumaini la Uhai wa Wakati Ujao? (rsSW uku. 344 maf. 5-7)
Okt. 1 Kusoma Biblia: 1 Wakorintho 4 hadi 6
Na. 1: 1 Petro 1:1 hadi 3:22 (si uku. 250 maf. 6-8)
Na. 2: 1 Wakorintho 6:1-11, 15-20
Na. 3: Mataraja ya Uhai wa Wakati Ujao Yatatimizwaje? (rsSW uku. 344 fu. 8 hadi uku. 345 fu. 1)
Na. 4: Sababu Matakwa ya Kisheria Lazima Yatimizwe Katika Ndoa (rsSW uku. 241 fu. 2 hadi uku 242 fu. 2)
Okt. 8 Kusoma Biblia: 1 Wakorintho 7 hadi 9
Na. 1: 1 Petro 4:1 hadi 5:14 (si uku. 250 maf. 9, 10)
Na. 2: 1 Wakorintho 9:11-27
Na. 3: Sheria Ya Kristo Ambayo Wakristo Wanahitaji Kutimiza ni Gani? (peSW sura 24 maf. 12-14)
Na. 4: Ndoa ya Wake Wengi Si kwa Wakristo Hata Kama Ni ya Kisheria (rsSW uku. 243 maf. 1, 2)
Okt. 15 Kusoma Biblia: 1 Wakorintho 10 hadi 12
Na. 1: Utangulizi kwa 2 Petro (si uku. 252 maf. 1-3)
Na. 2: 1 Wakorintho 10:1-13, 31-33
Na. 3: Sababu Ndoa ya Wake Wengi, Ilikubaliwa Wakati Mmoja, Haikubaliwi kwa Wakristo (rsSW uku. 243 fu. 3 hadi uku. 244 fu. 1)
Na. 4: Je! Kutengana Kunaruhusiwa Ndoa Iwapo Ngumu? (rsSW uku. 244 fu. 2)
Okt. 22 Kusoma Biblia: 1 Wakorintho 13 na 14
Na. 1: 2 Petro 1:1 hadi 2:22 (si uku. 252 maf. 4, 5)
Na. 2: 1 Wakorintho 13:1-13
Na. 3: Ulimwengu Ambao Lazima Wakristo Wajitenge Nao ni Upi? (peSW sura 25 maf. 1-4)
Na. 4: Misingi Pekee ya Talaka Inayoruhusu Kufunga Ndoa Tena (rsSW uku. 244 fu. 3 hadi uku. 245 fu. 3)
Okt. 29 Kusoma Biblia: 1 Wakorintho 15 na 16
Na. 1: 2 Petro 3:1-18 (si uku. 253 maf. 6, 7)
Na. 2: 1 Wakorintho 15:20-34
Na. 3: Sababu Mungu Aliruhusu Ndoa Kati ya Ndugu na Dada Hapo Mwanzo (rsSW uku. 245 maf. 4, 5)
Na. 4: Ndoa Yaweza Kufanywaje Iwe Bora? (rsSW uku. 246 Na. 1, 2)
Nov. 5 Kusoma Biblia: 2 Wakorintho 1 hadi 4
Na. 1: 1 Yohana: Iliandikwa na Nani? (si uku. 254 maf. 1-3)
Na. 2: 2 Wakorintho 3:1-6, 12-18
Na. 3: Ni Sehemu Gani Tatu Kubwa za Ulimwengu wa Shetani? (peSW sura 25 maf. 5-9)
Na. 4: Ndoa Yaweza Kufanywaje Iwe Bora? (rsSW uku. 246 Na. 3, 4)
Nov. 12 Kusoma Biblia: 2 Wakorintho 5 hadi 8
Na. 1: 1 Yohana: Kwa Nini Iliandikwa? (si kur. 254-5 maf. 4, 5)
Na. 2: 2 Wakorintho 6:3-18
Na. 3: Ndoa Yaweza Kufanywaje Iwe Bora? (rsSW uku. 246 Na. 5, 6)
Na. 4: Twaweza Kujifunza Nini Kutokana na Habari ya Biblia juu ya Mariamu (rsSW uku. 172 Na. 1, 2, 5)
Nov. 19 Kusoma Biblia: 2 Wakorintho 9 hadi 13
Na. 1: 1 Yohana 1:1 hadi 3:24 (si uku. 255 maf. 6-8)
Na. 2: 2 Wakorintho 9:1-15
Na. 3: Kwa Nini Lazima Tujilinde Dhidi ya Ulimwengu wa Shetani (peSW sura 25 maf. 10, 11)
Na. 4: Ndoa Yaweza Kufanywaje Iwe Bora? (rsSW uku. 246 Na. 7, 8)
Nov. 26 Kusoma Biblia: Wagalatia 1 hadi 3
Na. 1: 1 Yohana 4:1 hadi 5:21 (si uku. maf. 9, 10)
Na. 2: Wagalatia 3:15-29
Na. 3: Mariamu Alikuwa Bikira Kikweli Alipozaa Yesu (rsSW uku. 173 maf. 2, 3)
Na. 4: Mariamu Hakuendelea Kuwa Bikira Sikuzote (rsSW uku. 174 fu. 1)
Des. 3 Kusoma Biblia: Wagalatia 4 hadi 6
Na. 1: 2 Yohana: Utangulizi na Yaliyomo (si uku. 256-7 maf. 1-4)
Na. 2: Wagalatia 5:13-26
Na. 3: Jinsi ya Kutokuwa Sehemu ya Ulimwengu (peSW sura 25 maf. 12-14)
Na. 4: Mariamu Hakuwa Mama ya Mungu (rsSW uku. 174 maf. 2-4)
Des. 10 Kusoma Biblia: Waefeso 1 hadi 3
Na. 1: 3 Yohana: Utangulizi na Yaliyomo (si uku. 258 maf. 1-4)
Na. 2: Waefeso 3:8-21
Na. 3: Ubaya wa Dini Bandia Hauhakikishi Hakuna Dini ya Kweli (tdSW 5H)
Na. 4: Mariamu Hakupanda Mbinguni Akiwa na Mwili (rsSW uku. 175 fu. 3 hadi uku. 176 fu. 1)
Des. 17 Kusoma Biblia: Waefeso 4 hadi 6
Na. 1: Utangulizi kwa Yuda (si uku. 259 maf. 1-4)
Na. 2: Waefeso 5:15-33
Na. 3: Kwa Nini Wakristo Hawasherekei Krismasi (peSW sura 25 fu. 15)
Na. 4: Biblia Haionyeshi Mariamu Kuwa Muombezi (rsSW uku. 176 maf. 2, 3)
Des. 24 Kusoma Biblia: Wafilipi 1 hadi 4
Na. 1: Yuda 1-25 (si kur. 259-60 maf. 5-7)
Na. 2: Wafilipi 4:4-20
Na. 3: Kielelezo Alichoweka Yesu cha Kutoheshimu Mariamu Kipekee (rsSW uku. 177. maf. 3, 4)
Na. 4: Aliyomaanisha Yesu Aliposema: “Huu Ni Mwili Wangu (rsSW uku. 201 fu. 2 hadi uku. 202 fu. 3)
Des. 31 Pitio la Kuandika: Maliza Warumi 7 hadi Wafilipi 4