Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/89 uku. 7
  • Matangazo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Matangazo
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1989
Huduma Yetu ya Ufalme—1989
km 12/89 uku. 7

Matangazo

● Toleo la fasihi Desemba: Hadithi za Biblia au Kuishi Milele. Januari na Februari: Cho chote cha vitabu vya kurasa 192 kilichotangazwa kwa chapa kabla ya 1980 ambacho kundi linavyo akibani kwa nusu ya mchango wa kawaida, isipokuwa vifuatavyo: Maisha ya Jamaa, Mwalimu Mkuu, Uzima Ndio Uu Huu, Kweli, na Ujana. Kuna ugavi kidogo wa Commentary on James unaoweza kuagizwa. (Kuhusu kukopeshwa, wazee wapaswa kurejeza kwenye miongozo katika Huduma ya Ufalme ya Desemba 1988, ukurasa 3).

● Tarehe ya Ukumbusho kwa 1990 itakuwa ni Jumanne, Aprili 10, baada ya jua kutua.

● Mwangalizi msimamizi au mtu mwingine aliyeteuliwa naye apaswa kukagua hesabu za kundi Desemba 1 au upesi iwezekanavyo baada ya hapo.

● Makundi yapaswa kuanza kuagiza mabuku yaliyojalidiwa ya Mnara wa Mlinzi na Amkeni! kwa 1989 kwenye maagizo yao ya fasihi ya Desemba. Mabuku yaliyojalidiwa yatapatikana katika Kiingereza na Kifaransa. Mabuku yaliyojalidiwa ni bidhaa za kuagizwa kwa kiasi na yatatozwa kwa bei ya wote.

● Marekebisho fulani yatafanywa kwenye machapisho ya wakati ujao ya kitabu Kuishi Milele. Badiliko pekee kubwa ni kuhusiana na Wasodoma, kwenye kurasa 178 na 179. Badiliko hili lilitokea kwenye kitabu Revelation, ukurasa 273 na katika Mnara wa Mlinzi wa Juni 1, 1988, kurasa 30 na 31. Unaweza kuonyesha hivyo kwenye machapisho ya kwanza uliyo nayo.

● Ikiwa makundi yangali hayajafanya hivyo, yapasa kuanza kuagiza Kuyachunguza Maandiko Kila Siku—1990 pamoja na agizo lao la fasihi la Desemba. Vijitabu hivyo vitapatikana katika Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa na Kiswahili. Vijitabu Kuyachunguza Maandiko ni bidhaa za kuagizwa kwa kiasi na vitatozwa kwenye hesabu ya fasihi kwa bei ya mhubiri. Mapainia wa kawaida na wa pekee walioorodheshwa kabla ya Julai 1, 1989, waweza kupokea nakala moja ya bure na kupata nakala za ziada kwa bei ya painia. Kwenye fomu ya malipo ya kila mwezi (S-20) maandishi tofauti yapasa kuandikwa, yakionyesha nakala za bure kwa mapainia.

● Huduma ya Ufalme Yetu ya Aprili 1980, ukurasa 3, 4, chini ya Sanduku la Swali ilionyesha namna mbalimbali za kuita watu zinazopendekezwa kutumiwa kwenye mikutano ya kundi. Ndugu wanaoongoza mikutano wanatiwa moyo warudie na kutumia habari hiyo.

● Maswali yanayohusu jinsi ya kuhesabu wakati wa utumishi wa shambani kwa ajili ya funzo la Biblia la jamaa yamejibiwa kwenye Sanduku la Swali katika ukurasa 1 wa Huduma ya Ufalme Yetu ya Julai 1983.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki