Matangazo
● Toleo la fasihi la Septemba: Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation? au Kuishi Milele au Hadithi za Biblia ambako kitabu Creation hakipatikani katika lugha inayotumiwa katika eneo. Oktoba: Andikisho la ama Amkeni! au Mnara wa Mlinzi au yote mawili. Novemba: New World Translation of the Holy Scriptures na Should You Believe in the Trinity? au “Tazama! Mimi Ninafanya Vitu Vyote Kuwa Vipya.” Desemba: Kitabu Hadithi za Biblia au Kuishi Milele.
● Mwangalizi msimamizi au mtu mwingine aliyepewa mgawo naye apaswa kukagua hesabu ya kundi Septemba 1 au upesi iwezekanavyo baada ya hapo.
● Orodha ya Bei Mpya imetayarishwa na kila kundi linapelekewa nakala nne. Zapasa kugawanywa kwa mwandishi na kwa wale ndugu wanaoangalia fasihi, magazeti, na hesabu.
● Wakati wa mzunguko ufuatao wa ziara kuanzia Septemba 1990, mwangalizi wa mzunguko atatumia wakati fulani pamoja na mwandishi wa kundi na mtumishi wa hesabu wazungumzie utaratibu wa kufanya hesabu. Usaidizi huu wa kibinafsi upande wa mwangalizi wa mzunguko utasaidia kuhakikisha kwamba hesabu za kundi zinashughulikiwa ifaavyo kulingana na maagizo ya Sosaiti juu ya kutunza maandishi ya kundi.
● Vichapo Vipya Vitakavyopatikana Akibani Karibuni:
“All Scripture Is Inspired of God and Beneficial,” chapa ya 1990 —Kiingereza
Wenye Umoja Katika Ibada ya Mungu wa Pekee wa Kweli —Kinyarwanda
Je! Mungu Anajali?—Kihindi
Kiingereza:
Watchtower Publications Index 1986-1989
Watchtower Bound Volumes 1975-79
Watchtower Bound Volumes 1989
Awake! Bound Volumes 1989
Vijitabu:
“Habari Njema Hizi za Ufalme”
Wakati Ujao Salama—Jinsi Unavyoweza Kuuona
Je! Mungu Anajali?
● Kuanzia Septemba 1990 uangalizi wa kazi katika Ushelisheli utahamishwa kutoka Kenya uwe chini ya tawi la Mauritius.
● Wakati wa miezi kadhaa iliyopita kumekuwako uhitaji wa kuwapa msaada ndugu zetu katika baadhi ya maeneo yenye njaa. Twashukuru makundi yote na ndugu mmoja mmoja ambao hutuma upaji kwa ajili ya makusudi ya kutoa misaada.
● Tumalizapo mwaka wa utumishi tutathamini kupata ripoti zote za utumishi wa shambani kwa wakati wake kutoka kwenu wahubiri wapendwa.