Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 2/91 uku. 4
  • Sanduku la Swali

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Sanduku la Swali
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1991
  • Habari Zinazolingana
  • Waangalizi Wanaoongoza—Mwandishi
    Huduma Yetu ya Ufalme—1998
  • Sanduku La Swali
    Huduma Yetu ya Ufalme—1994
  • Je, Unahama?
    Huduma Yetu ya Ufalme—1999
  • Sehemu ya 3: Changia Maendeleo ya Wengine
    Huduma Yetu ya Ufalme—1991
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—1991
km 2/91 uku. 4

Sanduku la Swali

● Mhubiri anapohamia eneo lingine, ni nini lapasa kufanywa ili kusaidia ahamie kundi hilo jipya?

Mara mhubiri akiisha kuwasili kutoka kundi lingine, mwandishi wa kundi apaswa kupata kutoka kwa mhubiri huyo jina la kundi aliloshirikiana nalo hapo kwanza pamoja na jina na anwani ya mwandishi wa kundi hilo. Kisha apaswa amwandikie mwandishi wa kundi hilo la hapo kwanza, aombe kadi ya Maandishi ya Mhubiri wa Kundi pamoja na barua ya kumjulisha. Mwandishi anayepokea ombi hilo apaswa kujibu bila kukawia.—Ona Tumefanywa Tengenezo Tutimize Huduma Yetu, kurasa 104-5.

Mhubiri anayeondoka aweza kusaidia kwa kuhakikisha kwamba ana jina sahihi la kundi analoondoka na jina na anwani ya mwandishi. Ndipo, mara awasilipo katika lile kundi jipya, habari hiyo yaweza kupewa mwandishi wa kundi ili aweze kufuatia jambo hilo mara moja. Ripoti za utumishi wa shambani zilizotolewa kwa kundi hilo jipya zaweza kuwekwa mpaka kadi ya maandishi ipokewe. Baada ya hapo utendaji wa mhubiri waweza kuwekwa kwenye kadi ya maandishi na kutiwa pamoja na ripoti ya kundi ya kila mwezi inayofuata.

Katika visa fulani huenda mhubiri akawa tayari anajua jina na anwani ya mwandishi wa kundi analohamia. Ikiwa ndivyo, hakungekuwa na uhitaji wa wazee kungojea wapelekewe ombi. Maandishi ya utendaji wa mhubiri huyo na barua ya kumjulisha vyaweza kupelekwa kwa posta mara moja kwa mwandishi wa kundi ambalo mhubiri huyo atashirikiana nalo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki