Matangazo
● Toleo la Fasihi la Agosti: Broshua yoyote ya kurasa 32, isipokuwa broshua Shule. Septemba: Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation?, au Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia au Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani. Oktoba: Maandikisho ya ama Amkeni! ama Mnara wa Mlinzi ama magazeti yote mawili. Novemba: Biblia ya New World Translation of the Holy Scriptures pamoja na kitabu The Bible—God’s Word of Man’s?
● Kila mmoja anayeshirikiana na kundi apaswa kufanya upya uandikisho wake wa Mnara wa Mlinzi na Amkeni! kupitia kwa kundi. Itasaidia ikiwa maagizo yote ya fasihi na bidhaa nyingine yanatolewa kupitia kundi badala ya watu mmoja mmoja kuyapeleka kwa Sosaiti.
● Makundi yapaswa yaanze kuagiza 1992 Calendar of Jehovah’s Witnesses pamoja na agizo lao la fasihi la Septemba. Kalenda hiyo mpya itakuwa yenye kuvutia na yenye kuelimisha hasa, ikiunganisha picha za Nchi ya Ahadi na mandhari ya michoro ya Kibiblia inayohusiana nayo. Picha na matukio pia yatakuwa yenye maana zaidi kwetu. 1992 Calendar of Jehovah’s Witnesses itapatikana kwa Kiingereza na Kifaransa.
● Tokea Agosti 28 hadi Agosti 31, Sosaiti itakuwa ikifanya hesabu ya fasihi yote iliyo akibani katika Betheli. Kwa sababu ya hesabu hiyo, hakuna maagizo ya fasihi yatakayoshughulikiwa ili kupelekwa au kuchukuliwa wakati wa siku hizo.
● Kila kundi litapokea fomu tatu za Orodha ya Vitabu na lapasa kuhesabu kihalisi fasihi za kampeni. Tafadhali jazeni fomu hizo kikamili, na kupeleka ya awali kwetu, si baada ya Septemba 6, 1991. Tunzeni nakala ya kaboni kwa ajili ya faili zenu. Twawapelekea nakala ya tatu iwe nakala ya kufanyia kazi.
● Kila kundi linapelekewa kiasi cha kutosha cha fomu kwa ajili ya matumizi ya mwaka wa utumishi wa 1992. Fomu hizo hazipasi kutumiwa ovyoovyo. Zapasa kutumiwa kwa ajili tu ya kusudi lililonuiwa.
● Beji za mkusanyiko wa wilaya kwa 1991 katika Kiingereza na Kiswahili zitapelekwa na kutiwa pamoja na fasihi mtakazotumiwa karibuni. Haitakuwa lazima kuziagiza. Ikitegemea ukubwa wa kila kundi, mtapelekewa kwa mafungu ya 25. Hesabu ya fasihi itatozwa kwa kulingana. Ikiwa beji za ziada zahitajiwa na kundi, zapasa kuagizwa katika fomu ya Agizo la Vitabu (S-14-SW). Itakuwa lazima kuagiza vifuniko vya beji kwa wowote kundini wanaovihitaji.
● Marekebisho katika kitabu Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!:
Ukurasa 30, safu 1, fungu la 11, mstari 8: Badilini: 2 Petro 3: Liwe: 2 Petro 2:
Ukurasa 147, safu 2, fungu la 19, mstari wa 10: Badilini: katika 1918 na Uwe: katika 1917 na
Ukurasa wa 190, safu ya 2, wa fungu la 15, mistari ya 6-9: Badilini: 1916, askari-jeshi 420,000 wa Uingereza walikufa, pamoja na 200,000 wa Ufaransa na 450,000 wa Ujeremani—zaidi ya vifo 1,000,000! Iwe: 1916, kulikuwako majeruhi 420,000 wa Uingereza pamoja na 194,000 wa Ufaransa na 440,000 wa Ujerumani—majeruhi zaidi ya 1,000,000!
● Vichapo Vipya Vinavyopatikana:
Damu Yaweza Kuokoaje Uhai Wako? —Kiarabu
“Tazama! Mimi Nafanya Vitu Vyote Kuwa Vipya” (Broshua) —Urdu
How to Find the Road to Paradise (kwa ajili ya Waislamu) —Kifaransa