Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 4/93 kur. 5-6
  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1993
Huduma Yetu ya Ufalme—1993
km 4/93 kur. 5-6

Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Pitio vitabu vikiwa vimefungwa la habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa majuma ya Januari 4 hadi Aprili 19, 1993. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Katika kuongoza funzo la Biblia, huenda ikawa bora kutojibu maswali yote yanayoulizwa, bali kuacha mengine ili yachunguzwe wakati mwingine. [sg-SW uku. 94 fu. 14]

2. Mojawapo malengo makuu ya shule ya Huduma ya Kitheokrasi ni kutusaidia tuwe wenye kufaa zaidi katika huduma ya shambani. [sg-SW uku. 96 fu. 1]

3. Katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi, sikuzote shauri litatolewa juu ya sifa zile ambazo mwanafunzi aliarifiwa mapema azitengeneze. [sg-SW uku. 101 fu. 7]

4. Kufikia sasa kitabu cha 1 Wafalme hakijaungwa mkono na akiolojia. [si-SW uku. 65 fu. 4 (Chapa ya 1983, uku. 65 fu. 4)

5. Haitoshi mshauri kumwambia tu msemaji kwamba alifanya vema au kwamba ni lazima atengeneze tena sifa fulani ya usemi. [sg-SW uku. 103 fu. 15]

6. Mara nyingi udhaifu katika mahubiri ya mlango kwa mlango ni kwamba utangulizi ni mrefu mno, na mwenye nyumba anaanza kujiuliza ni wakati gani Shahidi atafikia maana yenyewe. [sg-SW uku. 115 fu. 14]

7. Ikiwa kundi lina vikuza-sauti, basi si lazima kushauri wanafunzi wasemaji kuhusu sauti. [sg-SW uku. 117 fu. 6]

8. Unapotoa hotuba ya mwanafunzi, vituo ni vya maana sana hivi kwamba inapendekezwa kwamba msemaji aweze hata kutia alama mahali hasa anapotaka kutua katika hati ya hotuba au muhtasari wake. [sg-SW uku. 120-1, maf. 20, 23]

9. Ubashiri wa mchawi katika Endori haukutimia kamwe. (1 Sam. 28:19) [Usomaji Biblia kila juma; ona w79-E 2/15 uku. 6]

10. Yaliyowapata Daudi na Bath-sheba yanapasa kuwakazia wazazi kwamba mwenendo wao unaweza kuwaadhiri sana watoto wao. (2 Sam. 12:13, 14) [Usomaji Biblia kila juma; ona w86-SW 3/15 uku. 31.]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Eli na Sauli walishindwa katika jambo gani? [si-SW uku. 57 fu. 27 (uku. 57 fu. 27)]

12. Unapoandika barua, unaweza kuonyeshaje kupendezwa na yule unayemwandikia? [sg-SW uku. 89 fu. 13]

13. Twaweza kwa kufaa kuwaelekezaje wasikilizaji wetu kwenye Biblia tunapotoa hotuba? [sg-SW uku. 122 fu. 3)

14. Ni nini linalomaanishwa kwenye 2 Samweli 18:8, linalosema: “Msitu ukala watu wengi kuliko wale walioliwa na upanga”? [Usomaji Biblia kila juma; ona w87-SW 3/15 uku. 31.]

15. Ni nani aliyemsababisha Daudi kuwahesabu Waisraeli? (2 Sam. 24:1) [Usomaji Biblia kila juma; ona w92-SW 7/15 uku. 5]

16. Kwenye 1 Wafalme 8:12, kwa nini Sulemani alitaarifu: “Bwana [Yehova, NW] alisema ya kwamba atakaa katika giza nene”? [Usomaji Biblia kila juma; ona w79-E 7/15 uku. 31.]

17. Kumethibitikaje kuwa kuna watu walio kama Malkia wa Sheba katika siku yetu? (1 Fal. 10:4, 7) [Usomaji Biblia kila juma; ona su-SW uku. 149 fu. 8.]

18. Ni uthibitisho gani wa akiolojia unaounga mkono usimulizi kwenye 1 Wafalme 14:25, 26? [Usomaji Biblia kila juma; ona ce uku. 212 fu. 31.]

19. Ni nini kinachomaanishwa na 1 Wafalme 15:14 linaposema kwamba ‘Asa hakuondosha mahali pa juu’? [Usomaji Biblia kila juma; ona w80-E 12/1 uku. 28 kielezi chini.]

Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

20. Wakati wa kuandika barua ili kutoa ushahidi, onyesha sikuzote nyuma ya bahasha. [sg-SW uku. 87 maf. 7, 8]

21. Ili kuepuka makisio ya kibinafsi unapotayarisha hotuba, vimepaswa vitumiwe na kutegemewa. [sg-SW uku. 111 fu. 13]

22. Ili kutimiza kusudi la hotuba, habari zaidi haipaswi itolewe kuliko . [sg-SW uku. 112 fu. 19]

23. 1 Samweli 25:37 inaposema ‘moyo wa Nabali ukafa ndani yake,’ linamaanisha kwamba kwa wazi alikuwa na . [Usomaji Biblia kila juma; ona pia w80-E 6/15 uku. 30.]

24. Agano linalosimuliwa katika 2 Samweli 7:12, 13 ni . [Usomaji Biblia kila juma; ona w89-SW 2/1 uku. 14.]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:

25. Yeremia bila shaka alimaliza kuandika kitabu cha 1 Wafalme katika (1040; 607; 580) K.W.K. [si-SW uku. 64 (uku. 64)]

26. Kitabu cha Samweli wa Pili kilihusisha kile kipindi cha kati ya (karibu 1180-1078; 1077-karibu 1040; 1040-911) K.W.K. [si-SW uku. 59 fu. 3 (uku. 59 fu. 3)]

27. Ni lazima kuwa waangalifu ili kutumia tu katika utangulizi (yale yanayowapendeza wasikilizaji; yale yanayokufanya uwe na shauku; yale yanayosaidia kusudi lako katika kusema). [sg-SW uku. 114 fu. 8]

28. Leo, Refaimu wa ki-siku hizi ni (tawala za kidikteta; makasisi; Umoja wa Mataifa). (2 Sam. 21:20) [Usomaji Biblia kila juma; ona w89-SW 1/1 uku. 20 fu. 8.]

29. Kulingana na 1 Wafalme 6:1, Sulemani alianza kujenga hekalu katika (1037; 1034; 1020) K.W.K. [Usomaji Biblia kila juma; ona si-SW uku. 285 fu. 8 (uku. 284 fu. 8).]

30. Kwenye 1 Wafalme 18:21-40, suala halisi lilikuwa ni mungu yupi (aliyekuwa na waamini wengi zaidi; aliyeungwa mkono na mamlaka zilizo kuu; anayepaswa kutumikiwa). [Usomaji Biblia kila juma; ona w84-E 7/15 kur. 8-9.]

Linganisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

2 Sam. 1:26; 6:6, 7; 13:14, 15; 1 Fal. 1:1; Ebr. 10:23-25

31. Kila mtu ana daraka la kibinafsi la kutoa maelezo kwenye mikutano. [sg-SW uku. 92 fu. 7]

32. Madhumuni mema hayabadili matakwa ya Mungu. [si-SW uku. 63 fu. 30 (uku. 63 fu. 30)]

33. Kuna kifungo cha upendo wenye umoja kilicho bora mno kati ya “kondoo wengine” na mabaki. (Yn. 10:16) [Usomaji Biblia kila juma; ona w89-SW 1/1 kur. 25-6.]

34. Kwa sababu tu mwanamume kijana ameonyesha kupendezwa na msichana kimapenzi na anasisitiza afanye ngono naye haimaanishi kwa lazima kwamba anampenda. [Usomaji Biblia kila juma; ona yy-SW uku. 141 fu. 22.]

35. Ni kawaida kwa wazee kuona vigumu kupata joto. [Usomaji Biblia kila juma; ona pia g82-E 6/8 uku. 22.]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki