Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 8/93 kur. 5-6
  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1993
Huduma Yetu ya Ufalme—1993
km 8/93 kur. 5-6

Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi

Pitio vitabu vikiwa vimefungwa la habari iliyozungumziwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa majuma ya Mei 3 hadi Agosti 23, 1993. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Unabii uliofanywa zaidi ya miaka 300 kimbele, kwamba Yosia angevunja-vunja madhabahu ya Yeroboamu kule Betheli, ulikuwa na utimizo wenye kutokeza. [si-SW uku. 68 fu. 25]

2. Wafalme wa Pili chahusisha kipindi cha kuanzia utawala wa Sulemani katika 1037 K.W.K. hadi karibu 580 K.W.K. [si-SW uku. 69 fu. 2]

3. Baada ya kusoma Andiko, ili kufanya matumizi kwa kawaida kunatosha kulizungumzia tu. [sg-SW uku. 129 fu. 20]

4. Ingawa kurudia ni muhimu katika ufundi wa kufundisha, kurudia kusiko kwa lazima kutaifanya hotuba iwe yenye maneno mengi mno na isiyopendeza. [sg-SW uku. 131 fu. 11]

5. Utakapojua kusema kutokana na muhtasari wa habari, utakuwa umefanya maendeleo makubwa kama msemaji wa watu wote. [sg-SW uku. 140 fu. 10]

6. Haiwezekani kufanya usomaji wa sauti wa mafungu uwe kama usemi wa bila kutazamia. [sg-SW uku. 146 fu. 21]

7. Kutiwa kwa mkazo kunatia ndani kufahamu maneno yale yaliyo na maana na kuyafanya yawe tofauti na maneno yanayoyazunguka. [sg-SW uku. 159 fu. 3]

8. Virembesho vya macho havikujulikana wakati wa Biblia. [Usomaji Biblia kila juma; ona g77-E 9/22 uku. 20.]

9. Uthibitisho wa kiakiolojia unaunga mkono kwa nguvu habari ya Biblia kwenye 2 Wafalme 17:6-18 jinsi Ashuru ilivyoharibu ufalme wa kaskazini wa Israeli. [Usomaji Biblia kila juma; ona gm-SW kur. 47-8.]

10. Maneno ya Daudi kwenye 1 Mambo ya Nyakati 16:31 hutoa kielezi cha kwamba ingawa utawala wa Yehova unaanzia tangu mwanzo wa uumbaji, wakati mwingine amekuwa akifanyiza maonyesho ya utawala wake ambao unamruhusu kutajwa “ametamalaki” (‘amekuwa Mfalme’) wakati fulani. [Usomaji Biblia kila juma; ona w85-SW 12/15 uku. 11.]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Mwenye nyumba anaposoma andiko, unaweza kukaziaje mambo makuu? [sg-SW uku. 128 fu. 13]

12. Ikiwa msemaji ana tatizo la mazoea ya kutoa ishara za mwili kupita kadiri, anapaswa kufanya nini? [sg-SW uku. 133 fu. 20]

13. Unaweza kufanya nini urekebishe ukosefu wa ufasaha wa kusema katika kusoma? [sg-SW uku. 143 fu. 7]

14. Ni kwa nini Mambo ya Nyakati kiliandikwa? [si-SW uku. 75 fu. 2]

15. Ni njia gani ya msingi ya kutolea hoja, au kutoa sababu? [sg-SW uku. 151 fu. 11]

16. Ule “Ushuhuda” kwenye 2 Wafalme 11:12 ulikuwa nini? [Usomaji Biblia kila juma; ona w91-SW 2/1 uku. 31.]

17. Kupatana na 2 Wafalme 19:32, 33, mfalme wa Ashuru alizuiwaje kuja Yerusalemu? [Usomaji Biblia kila juma; ona w88-SW 2/15 uku. 28.]

18. Tunaweza kujifunza nini kutokana na ono la Daudi na Hanuni kwenye 1 Mambo ya Nyakati 19:2-4? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w73-E uku. 478.]

19. Migawanyiko ya kikuhani 24 inatusaidiaje kuelewa cheo cha “wazee” wanaotajwa kwenye Ufunuo 4:4? (1 Nya. 24:4) [Usomaji Biblia kila juma; ona w73-SW uku. 480 au w73-E uku. 62.]

20. Tunaelewaje 1 Mambo ya Nyakati 29:5 kuwa na utimizo miongoni mwa watu wa Yehova leo? [Usomaji Biblia kila juma; ona w90-SW 7/1 uku. 31.]

Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

21. Kila hotuba yahitaji _________________________ ili kuipa njia na kuunganisha sehemu zake zote pamoja katika njia yenye kupendeza. [sg-SW uku. 133 fu. 1]

22. Msemaji ambaye ni stadi hapotezi _________________________ na wasikilizaji kwa kutazama maandishi yake kwa muda mrefu sana au kwa wakati usiofaa. [sg-SW uku. 138 fu. 1]

23. Kuonyesha kwamba Yehova havumilii utovu wa heshima kuelekea watumishi wake rasmi, yeye alilipiza kisasi kwa upesi juu ya wale wavunja sheria walipomdhihaki _________________________ akiwa nabii wa Yehova. [si-SW uku. 74 fu. 34]

24. Ukiwa msemaji una wajibu sikuzote wa kuweza kujibu ulizo _________________________ [sg-SW uku. 155 fu. 7]

25. Mathayo na Luka walitumia nasaba za _____________________________ kuthibitisha waziwazi kwamba Yesu alikuwa Mesiya. [si-SW uku. 78 fu. 23]

26. Katika hotuba nyingi, kushikamana kwataka _________________________ kutoka jambo moja kwenda kwa jingine. [sg-SW uku. 149 fu. 2]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:

27. Baada ya kuweka kichwa cha hotuba yako, hatua ifuatayo ni kuchagua (maandiko; vielelezo; mambo makuu) unayokusudia kutumia. [sg-SW uku. 135 fu. 9]

28. Ili uendeleze msingi wa hoja katika hotuba, ni lazima (useme waziwazi kabisa; ukumbuke maoni ya wasikilizaji; uwe mwenye idili). [sg-SW uku. 156 fu. 17]

29. “Mwaka wa ishirini wa Yothamu” wamaanisha mwaka wa 20 wa (maisha yake; utawala wake hususa; kipindi ambacho kilikuwa kimepita tangu awe mfalme.) (2 Fal. 15:30) [Usomaji Biblia kila juma; ona w80-E 9/15 uku. 8.]

30. Wale waliokuja ‘kumsaidia Daudi’ walikuwa (wakichochewa na choyo; wakichagua kuunga mkono ufalme wa Daudi; wakifuata mwendo usio na ukinzani mwingi). (1 Nya. 12:22) [Usomaji Biblia kila juma; ona w83-SW 8/1 uku. 10 au w83-E 3/1 uku. 18.]

Linganisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

1 Fal. 22:19-22; 2 Fal. 1:2, 7, 8; 5:1-5; 25:27-30; 1 Nya. 9:26, 27

31. Jinsi tunavyovaa kwaweza kutufananisha na kikundi au cheo fulani. [Usomaji Biblia kila juma; ona w73-SW uku. 163 au w72-E uku. 666.]

32. Watunza-malangoni Walawi walikuwa na ofisi ya itibari isiyo na kifani. [Usomaji Biblia kila juma; ona w88-SW 12/1 uku. 21.]

33. Ijapokuwa wazee huenda wakahisi kwamba wanajua jinsi ya kushughulikia hali mbalimbali, wanapaswa kujifunza kutokana na mfano wa Yehova na kusikiliza yale ambayo wengine wanasema na kuyaweka moyoni. [Usomaji Biblia kila juma; ona w75-SW uku. 33 au w74-E uku. 436.]

34. Akiolojia inaunga mkono ukweli wa kwamba mfalme Myudea aliyetekwa Babuloni aliachiliwa kutoka gerezani na akapewa posho la chakula. [Usomaji Biblia kila juma; ona gm-SW uku. 48.]

35. Watoto wanaweza kuwasukuma watu wazima kutenda. [Usomaji Biblia kila juma; ona w75-SW uku. 3-4 au w74-E uku. 402.]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki