Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/93 uku. 7
  • Kueneza Manufaa za Shule ya Mazoezi ya Kihuduma

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kueneza Manufaa za Shule ya Mazoezi ya Kihuduma
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1993
Huduma Yetu ya Ufalme—1993
km 12/93 uku. 7

Kueneza Manufaa za Shule ya Mazoezi ya Kihuduma

1 Kitabu-Mwaka cha 1993 (Kiingereza) kwenye kurasa 26 na 27 kiliandaa ripoti fupi juu ya mpango wa kueneza manufaa za Shule ya Mazoezi ya Kihuduma hadi mabara mengine. Ilisisimua kusoma juu ya mabara mbalimbali ambako madarasa yameongozwa hivi karibuni. Huko nyuma katika Aprili wakati wa kuwekwa wakfu kwa jengo la ofisi mpya ya tawi katika Zambia, mipango ilitangazwa ya kuanza shule hiyo katika bara hilo. Kwa hiyo tunafurahi sana kutangaza kwamba manufaa hizo zitapatikana pia katika Kenya na sehemu nyinginezo za Afrika Mashariki. Darasa la kwanza la Shule ya Mazoezi ya Kihuduma kwa ajili ya eneo letu litafanywa katika Nairobi. Tarehe ya kujiandikisha kwa ajili ya darasa hilo ni Machi 3, 1994.

2 Wazee na watumishi wa huduma wasiooa wanaopendezwa kuhudhuria shule hiyo waweza kuhudhuria mkutano pamoja na waangalizi wa mzunguko na wa wilaya wakati wa mkusanyiko wa mzunguko. Wakati huo wao wapokea habari zaidi juu ya kusudi la shule hiyo na pia baadhi ya matakwa ambayo ni lazima yatimizwe ili kustahili kuandikishwa.

3 Tangu kuanzishwa kwa shule hiyo katika 1987, Kitabu-Mwaka katika miaka ya karibuni imekuwa na ripoti fupi-fupi juu ya shule hiyo. Ripoti hizo zimeonyesha maendeleo ya kuongoza shule hiyo katika mabara na lugha mbalimbali na zimeonyesha jinsi shule hiyo inavyowafanya wale wanaohitimu wawe tayari zaidi kushughulikia madaraka na migawo yao. Katika eneo letu twaweza kutazamia sasa kufurahia manufaa za Shule ya Mazoezi ya Kihuduma.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki