Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 4/94 kur. 4-5
  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1994
Huduma Yetu ya Ufalme—1994
km 4/94 kur. 4-5

Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Pitio vitabu vikiwa vimefungwa la habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa majuma ya Januari 3 hadi Aprili 18, 1994. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu kila moja ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Watu ambao wana upendeleo wa Mungu hawapatwi na maafa. [Usomaji Biblia kila juma; ona w92-SW 9/15 uku. 4.]

2. Kulingana na Nehemia 10:34, matoleo ya kuni yaliamuriwa katika Torati. [Usomaji Biblia kila juma; ona w86-SW 2/15 uku. 22 au w86-E 2/15 uku. 26.]

3. Maneno ya Ayubu ya kujitetea katika Ayubu 31:1 yanapatana na yale Yesu alifundisha katika Mathayo 5:27, 28. [Usomaji Biblia kila juma; ona w78-E 12/15 uku. 32.]

4. Zaidi ya miaka 1,500 kabla ya Kristo, Ayubu alieleza juu ya tumaini katika ufufuo. [Usomaji Biblia kila juma; ona Ayubu 14:13 na w93-SW 4/15 uku. 11.]

5. Mafarisayo na waandishi walitumia usemi wa Kiebrania ʽam ha·ʼaʹrets, “watu wa ardhi [dunia],” ili kurejezea watu wa kawaida, ambao walitendewa kama mavumbi. [gt-SW sura 85]

6. Habari katika Esta 1:10-12 yaweza kusaidia mtu mtambuzi kuthamini kwamba kujitiisha na kuwa mtiifu ni kwenye thamani kubwa kuliko kuwa na urembo. [Usomaji Biblia kila juma; w79-SW 9/15 uku. 10 au w79-E 3/15 uku. 14.]

7. Ujitoaji kimungu huonyesha ushikamano wa upendo kwa Yehova kwa sababu ya kumthamini yeye na njia zake. [uw-SW uku. 19 fu. 15]

8. Habari katika Biblia kwenye Luka 16:19-31 juu ya tajiri na Lazaro ni hadithi halisi. [gt-SW sura 88]

9. Yesu alitaja “mali ya udhalimu” katika Luka 16:9, alikuwa akisema juu ya utajiri unaopatikana katika njia isiyo halali. [gt-SW sura 87]

10. Kwenye Luka 17:34, 35, ‘kuchukuliwa’ kunamaanisha uharibifu. [gt-SW sura 93]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Ni maswali gani mawili yaliyo muhimu ambayo kitabu cha Ayubu chajibu? [si-SW uku. 95 fu. 1]

12. Taarifa katika Ayubu 1:8 inatusaidiaje kujua wakati wa majaribu ya Ayubu? [si-SW uku. 95 fu. 4]

13. Yesu alimaanisha nini aliposema kwamba wafuasi wake wanapaswa ‘kuchukia’ watu wao wa ukoo? (Lk. 14:26) [gt-SW sura 84]

14. Maneno ya Yesu katika Yohana 11:26 yatakuwa kweli katika maana halisi sana lini na kuelekea nani? [gt-SW sura 90]

15. Kwa nini kufufuliwa kwa Lazaro kutoka kwa wafu kulikuwa pigo kubwa hasa kwa Masadukayo? [gt-SW sura 91]

16. Tueleweje jibu la Yesu kwa Mafarisayo aliposema: “Ufalme wa Mungu umo katikati yenu”? (Lk. 17:21) [gt-SW sura 93]

17. Ni mwelekeo gani wa Mafarisayo ambao Wakristo wanapaswa kuepuka, kama inavyoonyeshwa katika Luka 18:11, 12? [gt-SW sura 94]

18. Kwa sababu Yesu alikuwa mtu mkamilifu ambaye hakufanya dhambi, kwa nini alikataa mtawala kijana tajiri kumwita “mwema”? (Mk. 10:17, 18) [gt-SW sura 96]

19. Ni mambo gani makuu mawili yanayosaidia kuwe na umoja wa Kikristo wa kweli? [uw-SW uku. 8 fu. 8]

20. Mtu anaposema kwamba anaamini katika Utatu, kwa nini ni jambo la hekima kumruhusu ajieleze mwenyewe juu ya habari hiyo kabla ya kupinga Utatu? [uw-SW uku. 16 fu. 10]

Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

21. “Maganjoni” yanayorejezewa katika Ayubu 3:14 yalikuwa _________________________ . [Usomaji Biblia kila juma; ona w79-E 4/15 uku. 31.]

22. Kama vile Wayahudi wa siku za Esta, kwa kufaa Mashahidi wa Yehova wanaendea _________________________ ziwalinde na maadui. [Usomaji Biblia kila juma; ona w86-SW 3/15 uku. 22 au w86-E 3/15 uku. 25.]

23. Ingawa “waandishi” wa kibinadamu wapatao _________________________ walitumiwa kuandika Biblia, _________________________ mwenyewe ndiye Mwenye kuitunga. [uw-SW uku. 20 fu. 2]

24. Roho ya kujitegemea ilitokana na _________________________ . [uw-SW uku. 10 fu. 10]

25. Nehemia amalizia kitabu chake na ombi sahili na la unyenyekevu: _________________________ . [Usomaji Biblia kila juma]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya kati ya taarifa zifuatazo:

26. Wanafunzi wa Yesu ni chumvi ya dunia katika maana ya kwamba (ni lazima wavumilie mateso; waseme kwa upole; wana uvutano wenye hifadhi juu ya watu). [gt-SW sura 84]

27. Andiko katika Yohana 1:1 yarejezea mtu au watu (moja; wawili; watatu). [uw-SW uku. 16 fu. 11 (3)]

28. Kulingana na Zaburi 9:10, kujua jina la Mungu kwamaanisha (kujua tu jina Yehova; kuwa na ujuzi fulani juu ya makusudi yake; kuheshimu mamlaka yake na kutii amri zake). [uw-SW uku. 18 fu. 14]

29. Lazaro, Martha, na Mariamu waliishi (Yerusalemu; Bethlehemu; Bethania). [gt-SW sura 89]

30. Katika Mwanzo 1:1 na 1:26, neno la Kiebrania linalotafsiriwa “Mungu” ni (ʼAdho·naiʹ; ’Elo·himʹ; Shad·daiʹ). [uw-SW uku. 17 fu. 11 (4)]

Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

Neh. 13:23-27; Esta 1:17-20; Ayu. 14:14, 15; 26:7; Mit. 3:5, 6

31. Hakuna tegemeo lolote lenye kuonekana linaloshikilia dunia. [Usomaji Biblia kila juma; ona w92-SW 5/15 uku. 5.]

32. Waabudu wa Mungu wa kweli wanaotafuta mwenzi wanapaswa kuoa tu mwamini mwenzao ambaye yumo katika uhusiano uliowekwa wakfu kwa Yehova. [Usomaji Biblia kila juma; ona w89-SW 6/1 uku. 14.]

33. Yehova atamani sana kufufua wafu. [Usomaji Biblia kila juma; ona w90-SW 5/1 uku. 7.]

34. Mwendo wetu wote wa maisha umepasa ushuhudie kwamba kufikiri kwetu na makusudi yetu ni yenye kumwelekea Mungu. [uw-SW uku. 10 fu. 11]

35. Kutoonyesha staha kwa mamlaka ifaayo kwaweza kuwa na athari mbaya kwa wengine. [Usomaji Biblia kila juma; ona w79-SW 9/15 uku. 10 au w79-E 3/15 uku. 14.]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki