Matangazo
◼ Fasihi ya kutumiwa wakati wa Mei: Andikisho la Mnara wa Mlinzi. Juni: Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation? au Kuokolewa Kuingia Katika Dunia Mpya. Julai: Muunganisho wa vijitabu vitatu vya kurasa 32. Hivyo vijitabu vya kurasa 32 vyaweza kuombwa kutoka kwa Sosaiti au zile depo mbalimbali. TAARIFA: Makutaniko yatakayohitaji vifaa vya kampeni vilivyotajwa juu yapaswa kuviomba katika Agizo la Fasihi la kila mwezi litakalofuata (S-14-SW).
◼ Kabla ya kuanza mradi wa ujenzi wa Jumba la Ufalme, wazee wapaswa kupashana habari na Halmashauri ya Ujenzi ya Kimkoa ya eneo lao. Halmashauri za kimkoa zimeandaliwa habari ziwezazo kusaidia makutaniko kufanya maamuzi ya hekima. Ni jambo la busara kufikiria madokezo yatolewayo na halmashauri za kimkoa kabla ya kufanya maamuzi makubwa, kama mahali au ukubwa wa kiwanja au hata kukubali rasmi kugawiwa kiwanja, au kuamua vifaa vya kujengea au mahitaji ya wafanyakazi. Halmashauri za kimkoa ziko tayari kutoa madokezo kuhusiana na muundo, njia za kujenga, na uchanganuzi wa gharama.
◼ Vichapo Vitarajiwavyo Karibuni:
Kiarabu: “Ufalme Wako Uje”; “Habari Njema Hizi za Ufalme”; Wenye Umoja Katika Ibada ya Mungu wa Pekee wa Kweli; Ni Nini Lililo Kusudi la Uhai?—Wewe Waweza Kulipataje? Kiingereza: Watch Tower Publications Index 1991-1992; Kifaransa: Mabuku yaliyojalidiwa ya Mnara wa Mlinzi 1975, 1976; New World Translation of the Holy Sciptures (Dilaksi; DLbi12). Kigujarati: Mashahidi wa Yehova Wanaamini Nini? (Trakti Na. 14); Uzima Katika Ulimwengu Mpya Wenye Amani (Trakti Na. 15); Kuna Tumaini Gani kwa Wapendwa Waliokufa? (Trakti Na. 16). Kipunjabi: Mashahidi wa Yehova Wanaamini Nini? (Trakti Na. 14); Uzima Katika Ulimwengu Mpya Wenye Amani (Trakti Na. 15); Kuna Tumaini Gani kwa Wapendwa Waliokufa? (Trakti Na. 16).
◼ Audiokaseti Zitarajiwazo Karibuni:
Kiingereza: Kufanya Yaliyo Sawa Machoni pa Yehova (Drama). Kifaransa: Kutoka, Hesabu, Mambo ya Nyakati cha Kwanza, Mambo ya Nyakati cha Pili; Kuhifadhi Uhai Wakati wa Njaa (Drama); Kufanya Mapenzi ya Mungu kwa Bidii (Drama).
◼ Videokaseti Zitarajiwazo Karibuni:
Lugha ya Ishara ya Kiamerika (ASL): “Tazama! Mimi Ninafanya Vitu Vyote Kuwa Vipya.”