Pitio la Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
Pitio vitabu vikiwa vimefungwa la habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa majuma ya Mei 2 hadi Agosti 22, 1994. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.
[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]
Jibu kila moja ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:
1. Neno “Seʹlah,” (NW) linalotokea mara 71 katika kitabu cha Zaburi, halihitaji kutamkwa wakati wa kusoma. [si-SW uku. 101 fu. 5]
2. Kulingana na Zaburi 15:4, Mkristo akigundua kwamba jambo aliloahidi si la kimaandiko, bado apaswa kulitimiza. [Usomaji Biblia kila juma; ona w89-SW 9/15 kur. 28-9.]
3. Kitabu cha Ayubu chatoa uthibitisho kwamba si Mungu anayesababisha taabu, ugonjwa, na kifo. [si-SW uku. 100 fu. 42]
4. Mwendo wa maisha ya Yesu ulithibitisha kwamba Adamu angaliweza kudumisha ukamilifu usio na kasoro kama angalitaka kufanya hivyo na pia ukathibitisha kwamba kazi ya Mungu ya uumbaji haikuwa na kasoro. [uw-SW uku. 52 fu. 11]
5. Mtumwa anayetajwa katika Luka 19:20-24, aliyepata mina moja na kuihifadhi katika leso, alikuwa na hatia ya kutotenda. [gt-SW sura 100]
6. Kwa kufanya kazi kwa bidii na kujitolea kabisa kwa Mungu, Mkristo wa kweli aweza kujipatia ustahili wa kupata uhai wa milele. [uw-SW uku. 36 fu. 13]
7. Wakorintho wa Kwanza 2:9 larejezea Paradiso ya kidunia ya wakati ujao. [uw-SW uku. 26 fu. 12 (3); ona w85-E 9/15 uku. 30.]
8. Hatuwezi kukubali kuuona mwenendo usio wa ushikamanifu kuwa si jambo zito hata ingawa umekuwa kawaida ya ulimwengu huu. [uw-SW uku. 53 fu. 13]
9. Zaburi 49:15 ni maneno ya kuonyesha imani katika tumaini la ufufuo. [Usomaji Biblia kila juma; ona w89-SW 3/1 uku. 22 fu. 13.]
10. Mara nyingine kishawishi cha kushiriki mwenendo wa kilimwengu kinatokana na mtu mwingine anayejidai kuwa anamtumikia Yehova. [uw-SW uku. 43 fu. 11]
Jibu maswali yafuatayo:
11. Zaburi ni nini? [si-SW uku. 101 fu. 2]
12. Zaburi 27:10 latupa uhakikisho gani mzuri ajabu? [Usomaji Biblia kila juma; ona w92-SW 3/15 uku. 22 fu. 17.]
13. Zaburi 10:13 lafunua maoni gani mabaya ya watenda-dhambi wasiotubu? [Usomaji Biblia kila juma; ona w91-SW 11/1 uku. 6.]
14. Kulingana na Kutoka 9:15, 16, ni jambo gani lililotimizwa na jinsi Yehova alivyoshughulika na Farao? [uw-SW uku. 57 maf. 6, 7]
15. Taja njia mbili zinazoweza kutusaidia kuchunguza yale tunayosoma katika Biblia. [uw-SW uku. 27]
16. Amri ya “Mbusuni Mwana” yamaanisha nini, kama inavyotajwa katika Zaburi 2:12, kielezi-chini? [Usomaji Biblia kila juma; ona w86-SW 8/15 uku. 20.]
17. Yesu alikuwa akizungumzia uhuru wa aina gani katika Yohana 8:32? [uw-SW uku. 40 fu. 6]
18. “Huyo mwanamke” katika Mwanzo 3:15 anafananisha nani? [uw-SW uku. 30 fu. 3]
19. Kwa nini Daudi angeweza kumwambia Yehova kwenye Zaburi 51:4, “Nimekutenda dhambi Wewe peke yako,” na hali alijua kwamba alifanya dhambi dhidi ya wanadamu wenzake? [Usomaji Biblia kila juma; ona w93-SW 3/15 uku. 11 fu. 13.]
20. Ni nini kilichokuwa “kitu cha kunyarafisha kinachosababisha uharibifu” katika karne ya kwanza, na hicho ni nini leo? (Mt. 24:15) [gt-SW sura 111]
Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:
21. Kwenye Ayubu 40:15, NW, inaonekana kwamba “Behemothi” larejezea ________________________, na kwenye Ayubu 41:1 NW, “Leviathani” lafaa kabisa _________________________ . [Usomaji Biblia kila juma; ona it-1 uku. 280 na it-2 uku. 240.]
22. Sauti halisi ya Yehova ilisikika wakati Yesu _________________________ , wakati wa _________________________ , na katika siku ya Nisani 10, 33 W.K., aliposali kwa Baba yake kwenye _________________________ katika Yerusalemu. [gt-SW sura 104]
23. Mafarisayo walichuja _________________________ kutoka katika divai yao kwa sababu hakuwa safi kidesturi, na huku walipuuza haki, rehema, na uaminifu, ambazo zaweza kulinganishwa na kumeza _______________________________ , ambaye pia hakuwa mnyama aliye safi kidesturi. [gt-SW sura. 109]
24. Kwa kuwa Shetani alitumia uongo ili aongoze wazazi wetu wa kwanza watende dhambi, Yesu alimwita ‘ _________________________ .’ [uw-SW uku. 53 fu. 13 (1)]
25. Yesu ni Mwana _______________________________ Mungu kwa sababu yeye pekee ndiye aliyeumbwa na Yehova binafsi. [uw-SW uku. 29 fu. 1]
Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:
26. Ayubu alimwona Mungu, kama ilivyoandikwa kwenye Ayubu 42:5, kwa njia ya kwamba (aliona njozi ya Mungu kwenye upepo mkali; aliona malaika akimtokea; alikuja kumjua Yehova kwa undani zaidi). [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 8/15 uku. 12 fu. 11.]
27. Mwanamke ambaye Yesu alirejezea kwenye Mathayo 26:13 alikuwa (Mariamu, dada ya Lazaro; Mariamu, mke wa Klopasi; Mariamu Magdalena). [gt-SW sura 101]
28. Misingi inayoharibika, kama ilivyoandikwa kwenye Zaburi 11:3, inarejezea (misingi ya hekalu katika Yerusalemu; Yesu Kristo akiwa Jiwe Kuu la Pembeni la Msingi; misingi ambayo hutegemeza jamii, kama vile haki, sheria, na utaratibu). [Usomaji Biblia kila juma; ona w86-SW 8/15 uku. 20.]
29. Yesu aliwaita mitume hao (Petro na Andrea; Filipo na Bartholomayo; Yakobo na Yohana) “Wana wa Ngurumo” kwa sababu ya mwelekeo wao motomoto. [gt-SW sura 98]
30. Suala kuu lililozushwa na Shetani alipotilia shaka haki ya Mungu ya kutawala na njia Yake ya kutawala hasa lilihusisha (haki za kibinadamu; suala la kwamba ni nani aliye na nguvu zaidi; enzi kuu ya Ulimwenguni wote mzima wa Mungu). [uw-SW uku. 46 fu. 1]
Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:
Mwa. 3:1-5; Zab. 24:1; Mdo 8:32-38; Ebr. 10:26, 27; 1 Pet. 4:3, 4
31. Kutambua kwamba mwanadamu na dunia ni viumbe vya Mungu na kwamba kila kitu ni cha Yehova kwapasa kutusaidie kuwa wanyenyekevu na watiifu. [uw-SW uku. 39 fu. 4]
32. Twapaswa kuwa waangalifu sana tuepuke kuingia katika mazoea ya kufanya jambo lolote tunalojua kuwa halimpendezi Yehova. [uw-SW uku. 33 fu. 8 (3) na 8 (4)]
33. Ujuzi sahihi wa Biblia na uthamini wa ujumbe wayo husukuma watu wenye mfano wa kondoo wabatizwe. [uw-SW uku. 32 fu. 7]
34. Ingawa unaweza kufanya kazi na watu wasioamini au kwenda shuleni pamoja nao, utaonyesha kwamba huwachagui kuwa washiriki wako kwa kuepuka ushirika wote nao usio wa lazima. [uw-SW uku 44 fu. 13]
35. Ni jambo la muhimu kwamba tuepuke kufikiri kwa njia ya kilimwengu inayovutia watu waamini kwamba wananyimwa ikiwa hawawezi kujiwekea viwango vyao wenyewe maishani. [uw-SW uku. 46 fu. 1]